Kukumbushana jamani kupo kila lililo na Mwanzo halikosi kuw ana mwisho......

Just a stage in human existence! Live fully today because there is like no tommorow. Be good guys
 
Nalia ninapokumbuka, ifikapo siku yangu

Udongo utanifunika, tuta liwe juu yangu


nisiweze tena kutoka, nibakie peke yangu



Hiyo ndio siku yangu, nitapoiaga dunia!

nikifikiria mauti, hutetema moyo wangu
Na ufikapo wakati, nitauaga ulimwengu
zitakoma zangu kunuti, swalati na dua zangu
itanitoka roho yangu, nitapoiaga dunia!

Nitaiaga dunia, nijitenge na wenzangu
Sina nitachokichukua, ila ni amali yangu
Hesabu yaningojea, sijui mezani yangu
Una hofu moyo wangu, nitapoiaga dunia!

Nyumba iliyo nyembamba, itakua makao yangu
Kiza kitachonikumba, mbele ya macho yangu
Siwezi tena kuomba, ningoje hukumu yangu
Hayuko mtetezi wangu, nitapoiaga dunia!

Ardhi ndio tandiko, itakua malazi yangu
Hakuna ataekuwako, aitulize khofu yangu
Kwa hiyo misukosuko, nitahimili peke yangu
nitabakia peke yangu, nitapoiaga dunia!

Wote watanikimbia, swahiba na watu wangu
Udongo nitaolalia, utakua ni mto wangu
Maringo yashanishia, sina tena cheo changu
utakwisha ubosi wangu, nitapoiaga dunia!

utakuwapi wa murua?
, chaguo la moyo wangu
Naye atanikimbia, aniwache peke yangu
Vya ajabu vitanijia, viumbe vya bwana Mungu
Wenye ya moto marungu, wajapo kunihujia!

Ya Rabi nijaalia, nipasi hesabu yangu
Siku hiyo ikiwadia, usamehe dhambi zangu
Pepo yako niridhie, iwe masikani yangu
Uniweke kwenye fungu, la waja wako radhia
nitabakia peke yangu, nitapoiaga dunia!

Tamati tuikumbuke, siku hiyo ya machungu
Bure tusipumbazike, kwa raha za ulimwengu
Dini yetu tuishike, tumogope Bwana Mungu
Una kicho moyo wangu, nitapoiaga dunia
(musinisahau kwa dua Zenu)
 
duh! hii sijui PakaJimmy kaiona? bora nimeiona asubuhi mmh!

Nchi nzuri yametametaaaa
huonekana kule mbaliiii
naye yYesu hutuongozaa
Tukafike na sisi hukoooo
//:si mbalii, si mbalii
karibu karibu
tutaimba na sisi hukoooo
si mbalii simballi karibu karibu tutaimba na sisi huko.


Huko tutawaona wengi wengi
wapendwao na Bwana Yesu
tutafurahia daima itakuwa furaha tele

repeat chorous.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom