Kukuku Hadija yule.. kwako wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukuku Hadija yule.. kwako wapi?

Discussion in 'Entertainment' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 25, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Well.. kuna michezo mbalimbali ya utoto ambayo ilikuwa ni burudani, vituko na wakati fulani ilizaa urafiki wa kudumu sana. Michezo ambayo watoto wetu leo hii wanaweza kuona kuwa haina maana tena na wamebakia kucheza na computer, TV na gameboards..

  Kombolela
  Kioo kioo
  Ukuti ukuti
  Kuruka kamba
  Hiki na Hoko
  Namtafuta rafiki
  Tiari bado (mchezo huu ungepigwa marufuku!!!)
  Kitambaa changu cheupe
  Tukuone maringo yako!
  Watoto wangu eh

  Upi uliupenda na kwanini?
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Huo wa maringo yako ndo mtoto anashika kiuno anaanza kubingiribingi mpaka chini :)
  niliucheza Tabora miaka ileeeeeeeeeeee
   
 3. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Sisi kijijini ilikuwa kuchunga ng'ombe
   
 4. Companero

  Companero Platinum Member

  #4
  Mar 25, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  aah, wachunga ng'ombe wote wana mchezo wa kupigana kwa fimbo au sio!
   
 5. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  hiyo kwenye blue mimi ndio ilikuwa inanisuuza roho yangu, ukuti ukuti tulikuwa tunacheza ile mida ya saa moja kasoro hivi jioni kagiza ndio kanaingia saa hiyo unaitwa ukaoge unaona kama unazulumiwa basi hapo kilio ndio huanzia
   
 6. Companero

  Companero Platinum Member

  #6
  Mar 25, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mimi nilikuwa naupenda ule mchezo wa:

  Nampenda nampenda...nani...kijana mmoja....nani...mweusi kidogo...nani...
   
 7. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,427
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Tiari bado ilikuwa inanikosha roho mkuu na zaidi kipengele cha kuwa baba nilikuwa nakipenda. Nadhani hali ile ilikuwa inajenga utayari wa kukabiliana na majukumu ya sasa ya ubaba.
   
 8. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ilikuwa inanikosha roho kabisa
   
 9. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mi nilipenda kuwinda ndege kwa manati.....
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hahahahah ...napata picha kamili
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Sawia, na kuchonganisha ng'ombe wapigane
   
 12. Kibuja

  Kibuja JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2010
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 510
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mimi niliupenda wa tiyari bado;)
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Mar 25, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Du kumbe na wewe babu ulicheza michezo hii. Mimi hiyo kwenye bluu niliipenda zaidi!
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mimi kombolela bwana!najificha na mdada wa watu up to two hours:D:D
   
 15. Koiya

  Koiya Member

  #15
  Mar 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu umeusahau mchezo wa Kipande.
   
 16. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  jamni mnatukumbusha mbali!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! watoto wetu tunawafungia ndani hawajui nyimbo hizi
   
 17. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #17
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,019
  Likes Received: 23,747
  Trophy Points: 280
  Hivi ule wa baba na mama unaitwaje vile? Ulikuwa my favourite.
   
 18. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa najishindia kanisani mwanakwetu huku nikipewa hadithi za mitume na manabii wa ukweli.

  Hiyo michezo yenu ambayo mwisho wa siku zinazuka ndundi niliisikia kwenye bomba tu.
   
 19. Q

  Qsm JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 400
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  mie kujipikilisha, kujificha (tiari bado) na kucheza rede (ready)
   
 20. senator

  senator JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Tuko pamojah mwana hapa!! dah nilikuwa napenda sana kuwa baba..nusura niwe nduguye BABAYE KING MSWATI
   
Loading...