Kukubalika kwa Lowassa: Pesa, Ujinga, Upumbavu au kuichukia CCM?

Wewe chagua jibu kati ya yote tuliyoyauliza. Mimi na familia yangu tuna akili timamu na tumeamua kwamba lowassa anatosha na tutampa kura zetu.....poleni ila mmechelewa maamuzi yashafanyika.
 
Tumegundua janja ya Nyani ya "kutukaririsha" kwamba EL ni mwizi na fisadi pekee NJI hii wakati majambazi mengine yanazurura na V8 huku mitaani; magari ndio yanaitwa KILIMO KWANZA; Kilimo Kwanza Uhuru na Mandela road?! wana wazimu hawa!
Never again; Kwa sasa Hatutafuti kumchagua Mfalme Suleiman au Baba Mtakatifu hapa; we are seeking one of our own; a simple fallible human being to lead us to the promised land; Ni rahisi kuomuokoa Mwizi mmoja anayeingia kwenye kundi la watakatifu; ataacha! kuliko kumuokoa mtakatifu mmoja anyeingia kwenye chaka la wezi, mafisadi na majangili; atajiunga nao; upo hapo?

best wishes with your sacred plan but then again you need to proceed carefully,,,
 
Any successful REVOLUTION calls for SACRIFICES; When the going gets tough; the tough get going ma boy! Cowardice and procrastination is for laggards, opportuinits and the faint hearted; afterall; The higher the risk; the higher the returns!!
do not sit back and wait to reap where you did not sow! join the bandwagon; VUGUVUGU LA MABADILIKO liko njia moja; get on board!
 
Ccm hatuitaki sio kwasababu tu tunaichukia... Hatuitaki kwasababu wameshindwa kuleta maendeleo yanayolingana na muda waliokaa madarakani ukilinganisha na rasilimali tulizonazo hapa nchini na hii ni ikiwemo rasilimali watu... Vilevile ni lazima tujipime na mataifa ambayo tulikuwa nao sawa au tumewazidi wakati tunapata uhuru na sasa wametuzidi kimaendeleo...

Sasa wakati kama huu ni vizuri tujadiliane juu ya kipi sisiem wameweza kufanya na kipi wameshindwa ili tuweze kufanya maamuzi sahihi wakati wa uchaguzi..

Tatizo ni kwamba kuna watu hapa wao kazi yao ni kuleta siasa za maji taka hawana points, kazi kukishabikia chama au mtu tu....

Ninachopenda kuwaambie ndugu zangu ccm mwaka huu hatumchagui mtu/chama kwa ushabiki tunaangalia takwimu za kimaendeleo kama nyie mlipewa nafasi mkalala sasa watanzania tumeamka, tumehamasika na tumewachoka...

Well said mkuu!!!
 
Tumegundua janja ya Nyani ya "kutukaririsha" kwamba EL ni mwizi na fisadi pekee NJI hii wakati majambazi mengine yanazurura na V8 huku mitaani; magari ndio yanaitwa KILIMO KWANZA; Kilimo Kwanza Uhuru na Mandela road?! wana wazimu hawa!
Never again; Kwa sasa Hatutafuti kumchagua Mfalme Suleiman au Baba Mtakatifu hapa; we are seeking one of our own; a simple fallible human being to lead us to the promised land; Ni rahisi kuomuokoa Mwizi mmoja anayeingia kwenye kundi la watakatifu; ataacha! kuliko kumuokoa mtakatifu mmoja anyeingia kwenye chaka la wezi, mafisadi na majangili; atajiunga nao; upo hapo?

Big up sana boss!!!
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Tatizo lako wewe licha ya muelekeo mzuri wa kujenga hoja bado umeishia kama ulivyoanza kwa kuuliza Swali! Hutoi majibu, maoni huna, je tatizo lako ni nini haswaaa?! Umepigwa na butwaa, ujinga, upumbavu au kuipenda CCM sana?!

Lowassa sio fisadi, kama una ushahidi wa ufisadi wake nenda mahakamani, koma lalamo za mvunguni mwa kitanda, stand up an be counted, you either put up or shut up, period.
Mkuu,
Mimi nimeweka hoja mezani na kama unadhani ina mapungufu, ni wajibu wako pia kuyajazia hayo mapungufu.

Kuhusu suala la ufisadi wa Lowassa, hakuna maneno niliyoweka mimi. Hata quotetion ya mwanzo wa hoja yangu inatoka kwa mdau wa hapa Jamiiforums lakini kubwa zaidi, waliotuambia kwa sauti kubwa na nyingi kuwa Lowassa ni Fisadi ni viongozi wakuu wa CHADEMA.

Kuniomba mimi ushahidi wa ufisadi wa Lowassa ni kunionea kwa sababu ni viongozi wa CHADEMA waliotuambia kama Lowassa ni fisadi. Nadhani ingekuwa vizuri ukawauliza viongozi wakuu wa CHADEMA.
 
That being the case stop parroting the ccm hype, think ou of the box!! CDM "waliowambia" have turned the corner baada ya kuigundua janja ya Nyani ya CCM ya kukaririsha watu kuhusu ufisadi wa Lowassa; wakati wao wanaendelea kufisidi NJI kwa kwenda mbele!
 
njaa kitu kibaya sana.ukiacha tumbo likufanyie maamuzi, haya ya chadema na lowassa lazima yawe mambo ya kawaida kwako.
Mkuu,
Bado sijayameza yanayotokea katika siasa kwa sasa nchini.

Kila siku ninaendelea kujifunza mengi.

Kweli siasa za Tanzania sio kama nizijuavyo!
 
Kilicho sahihi hapo ni moja kununuliwa kwa watu,uzezeta wa watu na wengi kufuata mkumbo hayo ndio mtaji hasa wa lowassa, inasikitisha sana watu kumuona fisadi mwema kwamwamvuli wa kuiondoa ccm hapo malengo ni madaraka na si kuikomboa tz
 
unahoja yoyote na jembe lako begani, wewe ni shabiki wa ccm period,,,tuondolee makando ya ccm
Mkuu,
Unapoweka siasa katika mzani wa ushabiki ni kuonesha jinsi usivyofahamu maana ya siasa na athari zake katika nchi.

Siasa siyo kama vilabu vya michezo bali ni msingi wa maisha ya wananchi.

Kama mimi ni shabiki wa CCM, wewe ni shabiki wa nini?
 
attachment.php

Comment ya huyu Mdau anayeenda kwa jina la Pasco wa Jamiiforums ambaye fikra zake kuhusu Lowassa haziteteleki imenipelekea kufikirisha ubongo wangu kuhusu Tanzania ya leo na kesho na kuanza kujiuliza maswali mengi!

Hii ni comment yake,

Wakati wa kumkaribisha Lowassa kuwa mwanachama wa CHADEMA, Nilishangaa kidogo kusikia Tundu Lissu na Mbowe wakisema mbele ya wananchi, ‘’Lowassa ana tatizo la kimaadili ndiyo maana tulimtaja katika kundi la mafisadi (list of shame) pale Mwembeyanga’’.

Nikajiuliza, ni nini tena kimewafika viongozi wakuu wa CHADEMA mpaka suala la ufisadi wameamua kuliweka kando na kuungana na list of shame?

Nikakumbuka maneno ya Mmarekani aitwaye Jim Henson ambaye aliwahi kusema, If you can't beat them. Join them.

Kwa maana nyingine, CHADEMA kama chama wameshindwa kupambana na ufisadi na sasa wanaungana na mafisadi ndiyo maana hata msingi wa Ilani yao ya Uchaguzi na mgombea wao wa mwaka 2010, Dk. Slaa wameamua kumuweka kando na kumteua fisadi, Edward Lowassa kama mgombea Urais wa Tanzania.

Nikakumbuka pia maneno ya wanasaikologia wanayosema, ‘’Mara nyingi fikra za viongozi wetu zinaakisi fikra zetu’’, lakini vile vile nikakumbuka kuwa, Money talks hasa kwenye jamii yenye ufinyu wa uelewa!

Vyombo vingi vya habari kwa sasa hivi vinawashambulia sana wapinga rushwa/ufisadi nchini kiasi kwamba hata jamii imeanza kununua hoja za vyombo vya habari kwa kuwaona wapinga rushwa/ufisadi kama ni debe tupu.

Lowassa ana kundi kubwa la vyombo vya habari, viongozi na wananchi ambao ni kama waumini walioweka imani yao kwake katika raha na shida.

Imenibidi niende kwenye maktaba za Jamiiforums kutafuta kumbukumbu kuhusiana na kile kilikuwa kikisemwa na wanaJF kabla ya Lowassa kuhamia CHADEMA ili nijidhirishe kama kweli fikra za viongozi wetu zinaakisi fikra zetu. Nilichokipata na kukisoma kimenishitua na kunishangaza sana. Nimefikia hitimisho na kusema, kweli Tanzania siyo kama tuijuavyo.

Hizi hapa chini ni baadhi ya thread ambazo viongozi wetu na wanaJF walisema kuhusu Lowassa wakati akiwa mwana CCM.

Gonga ili usome comments za Wananchi mbali mbali.

Yanayoendelea ndani ya Tanzania yananipa maswali mengi ambayo yanaangukia kwenye msingi wa maswali matatu, Je, kubalika kwa Lowassa pamoja na ufisadi wake kunabebwa na sababu kubwa ipi? Pesa, Ujinga, Upumbavu au kuichukia CCM?

Wapinga rushwa/ufisadi waliobaki nchini are about to learn a stern lesson about the vigour of mafisadi nchini!.
Mkuu inayokubalika ni Chadema kutokana na msingi aliouweka Dr Slaa,Lowassa angekuwa anakubalika asiengeenda Chadema,angeenda vyama vidogo ndio tungeona nguvu zake ,pia angekuwa anakubalika angekuwa na plan B ya kuanzisha chama chake kwani ni siri iliyowazi kuwa alijua asingepitishwa CCM na ndio maana alianza kujipanga kuonekana kama anapendwa,tusubiri October 25 ndio tutaona hizo nguvu.
 
Tumeshayajua madhara ya kuchagua Rais anayeingia Ikulu akiwa na kundi la marafiki nyuma yake. Haturudii kosa hilo. Lowassa na marafiki zake watusamehe, nasema haturudi huko urais wa "marafiki" haufai. Tutamchagua magufuli ni kwa kule kukosa kwake "marafiki".
Mkuu,
Makundi yaliyomwingiza Rais Kikwete Ikulu kwa makubaliano ya kuachiana nafasi ya Urais ndiyo hayo leo anapambana nayo baada ya kukiuka makubaliano yao.

Kwa sasa wanamtandao waliomwingiza Rais Kikwete Ikulu wanajikusanya CHADEMA kwa mashambulizi zaidi.

Ninasubiri kampeni zianze ili nizifahamu mbivu na mbichi za hatima ya Rais Kikwete na kundi lililomwingiza Rais Kikwete Ikulu.
 
samahani kama nimekukwaza mkuu ila hoja yangu ilikua kuonesha hatari ya ile mentality ya watu wa aina yako ya "waondoke kwanza kwa njia yoyote ile halafu baadae ndo tuchambue pumba na mchele" na nilitolea mfano wa libya kwakua nao walikua na mentality hiyo hiyo ingawa walitumia mbinu tofauti kumuondoa marehem gaddafi madarakan bila kujali kama anaem replace ana uwezo ama hana matokeo yake sasa libya is as good as a failed state,, nilitoa tu angalizo...
Sijui tena nasema sijui elimu yako, tena sijui uvivu wako wa kusoma, tena sijui uzembe wako, tena sijui uelewa wako. Hivi katika karne hii can you fool us all the time kweli!!!! kwanini hukutumia mifano ya Zambia, Malawi, South Africa, Nigeria and Ghana. Au unataka kutuaminisha hapa kuwa wewe ni mvivu wa kusoma vitabu na majarida mbalimbali kama akina fulani!!!!! ambao matendo yao yanaonesha sio wasomaji wa vitabu na kama ni wasomaji basi ni poor assimilators of the knowledge. Hukunikwaza ila umejikwaza mwenyewe kwa kuweka vitu ambavyo sivyo.

Hivi unajua Kanali Gadaffi kuondolewa kwake madarakani, ni msala aliojitakia. Unafahamu alichowafanyia majemedari wenyeji wa kule Bengazi, ujinga wa kwanza huo, ujinga wa pili, akaanza kumwandaa mwanawe awe Mkuu wa nchi baada ya yeye kukaa madarakani for more than 35 years, kumbuka alipindua ufalme hivyo akaanza kujenga ufalme wa familia yake kama tunavyoona viongozi wetu hapa Tanzania, ujinga wa tatu ni pale alipowaita wananchi walimwinukia, kupinga ufalme wake aliokuwa anaujenga, kuwa ni panya, sawasawa kabisa na viongozi wa sasa wa CCM wanaowaita Watanzania wenzao ambao wanakihama CCM kuwa eti ni makapi bila kujua madhara yake katika mioyo ya watu hao, matokeo chama kimeanza kuchukiwa, naye alianza kuchukiwa na wananchi wake, tena na wakubwa huku duniani ambao wengine tayari alishajenga uhasama nao, wakawa wanatafuta opportunity tu ya kumla nyama, sasa ikiwa imepatikana wakamla nyama, Yaliyosalia ni historia.

Kumbuka kuitana majina mabaya hubomoa taifa, fuatilia mauaji ya kimbali sehemu zote duniani huambatana na uitanaji wa Majina mabaya. TAFAKARI
 
basi mkuu naona tu elimu yangu kumbe ndo haijatosha,,
 
Hii ni hali ya kukichoka chama tawala iliyondani ya watanzania wengi(yaani wanaichukia ccm) , lakini ukweli ni kwamba mtu akibadilika kwanza ndo nchi pia itabadilika(hivyo jambo la ujinga linaingia hapo), hivyo ni vema watu tukafahamu hilo ili upinzani usije ukawaOVERESTIMATED alafu wananchi wasione utofauti, kwani wanaohama ni wengi kuingia upinzani hivyo michango yao ya kisera na kiutendaje itaingia na upinzani ambayo ni ileile iliyopo sasa!
 
Sijui tena nasema sijui elimu yako, tena sijui uvivu wako wa kusoma, tena sijui uzembe wako, tena sijui uelewa wako. Hivi katika karne hii can you fool us all the time kweli!!!! kwanini hukutumia mifano ya Zambia, Malawi, South Africa, Nigeria and Ghana. Au unataka kutuaminisha hapa kuwa wewe ni mvivu wa kusoma vitabu na majarida mbalimbali kama akina fulani!!!!! ambao matendo yao yanaonesha sio wasomaji wa vitabu na kama ni wasomaji basi ni poor assimilators of the knowledge. Hukunikwaza ila umejikwaza mwenyewe kwa kuweka vitu ambavyo sivyo.

Hivi unajua Kanali Gadaffi kuondolewa kwake madarakani, ni msala aliojitakia. Unafahamu alichowafanyia majemedari wenyeji wa kule Bengazi, ujinga wa kwanza huo, ujinga wa pili, akaanza kumwandaa mwanawe awe Mkuu wa nchi baada ya yeye kukaa madarakani for more than 35 years, kumbuka alipindua ufalme hivyo akaanza kujenga ufalme wa familia yake kama tunavyoona viongozi wetu hapa Tanzania, ujinga wa tatu ni pale alipowaita wananchi walimwinukia, kupinga ufalme wake aliokuwa anaujenga, kuwa ni panya, sawasawa kabisa na viongozi wa sasa wa CCM wanaowaita Watanzania wenzao ambao wanakihama CCM kuwa eti ni makapi bila kujua madhara yake katika mioyo ya watu hao, matokeo chama kimeanza kuchukiwa, naye alianza kuchukiwa na wananchi wake, tena na wakubwa huku duniani ambao wengine tayari alishajenga uhasama nao, wakawa wanatafuta opportunity tu ya kumla nyama, sasa ikiwa imepatikana wakamla nyama, Yaliyosalia ni historia.

Kumbuka kuitana majina mabaya hubomoa taifa, fuatilia mauaji ya kimbali sehemu zote duniani huambatana na uitanaji wa Majina mabaya. TAFAKARI

well said kamanda kwa sasa tuna watu wachache sana humu wenye uelewa
mdogo alafu wanatusumbua na ninadhani uelewa wao ni mdogo sana ndio maana hawajui wanachokitetea hakuna pesa za kugawa watu hovyohovyo,watu wameamua rasmi kabisa kuachana na ccm,kinachochekesha ni jinsi viongoz wa ccm wanavyojitutumua wakati tayari walishazikwa zamani,nyuso za maccm ukiwatazama vzr wanaonesha wana masikitiko makubwa.Nawashauri ccm wakubaliane name gharika hili ili wapumzike kwa amani.
 
Sio pesa, si ujinga wala si upumbavu ni kuichukia ccm
Ukiongelea kufisadi wameshika namba,wizi wa kura ,mikataba mibovu ya maliasili, wabunge wavivu , kuruhusu ajira hadi za vibarua kwa wageni (mchina analeta mamia ya wachina kufanya kazi za vibarua kiwandani ) , kudharau wananchi elimu afya maji umeme tabu tupu, tembo wameisha,mateja kila kona viongozi wamo kwenye biashara hii nk nk yote haya ccm tu halafu watu wasi ichukie kwa nini?
 
Back
Top Bottom