Kukubali ushauri si ujinga. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukubali ushauri si ujinga.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Alhandro, Jun 16, 2011.

 1. A

  Alhandro Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  Salama wana jamii?
  Kwanza napenda kuchukua fulsa hii kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kunijalia kuiadhimisha siku hii ya kuzaliwa tena furaha iliyoje inakuwa siku ya kipekee kwa wanaafrika wote kwa kuitambua kama siku ya mtoto wa kiafrika.
  Nimechagua topiki hii nikitaka kuelezea hisia zangu kwa upande wa ujenzi wa taifa letu.Jana tumeisikia na kuielewa bajeti mbadala ya kambi ya upinzani kwa msimu wa mwaka 2011/2012.Kwa mtazamo nilionao mimi nimeiona bajeti hii ikiwa imesheheni vipau mbele kadha wa kadha ambavyo vinaweza kuwa sehemu ya kujikwamua na mambo mbalimbali yanayolisibu taifa.Ninavyo jua mimi hii ni bajeti mbadala na wala si ya serikali.hivyo basi kwa kuwa lengo letu sote ni kuliona taifa letu likipiga hatua za kimaendeleo ningependa kuishauri serikali kutoiona bajeti hii ya kambi ya upinzani kama adui kwao bali ikubali kuuchua ushauri{mipango} utakayoonekana kuwa wa kimanufaa na kuiingiza ktk bajeti yao ili kuboresha ufanisi.Kwa kufanya hivi hakutaifanya serikali ionekane kwamba haina uwezo wa kiutendaji ama kifikra isipokua itakuwa ikiwakilisha mtizamo na msimamo wa serikali iliyo tayari kuwatumikia wananchi wake na wala si vinginevyo.
  Na kwa upande wake wabunge ambao watanzania tumewajili wanapaswa kutambua kuwa kile wanachokifanya wawapo kazini kwao na hasa wawapo bungeni ni kwa ajili ya watanzani ambao ndiyo waajili wao na kusahau habali za siasa ambazo wamekuwa wakiziendeleza ndani ya bunge.Watambue kuwa uamzi mbaya ndiyo utakao liteketeza taifa na ndiyo itakayo kuwa hukumu yao siku ya kurudi kwa walio waajili kwani hawata kuwa na jipya la kuwaeleza wakaafikiana nao.
  Kwa kufanya hivyo natumai ile sera ya uwajibikaji itakuwa ina chukua nafasi yake na matunda yake yatakuwa yanaonekana kwa kila mtu.
   
Loading...