Kukua Na Kuanguka Kwa Utawala (Rise & Fall Of Governments/Empire States)

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,582
Habari wana JF,

Leo, nimevutiwa kuandika makala hii, inaohusiana na maswala ya kukua na kuanguka kwa mataifa kwa madhumuni ya elimu kwa wasiojua (kwa wanaojua iwe ukumbusho).

NB: Ntatumia mifano ya mataifa ya zamani, yaliowahi kutokea na kupitia hatua hizi husika za kukua na kuanguka ki-dola, ili kuepusha hoja zisizo na tija.

Nirejee kwenye makala husika,

MTAZAMO WA TAIFA (Government/Empire):

Neno "taifa" linajumuisha mambo mengi, miongoni ya hayo ni kua na SERIKALI KUU (Central State) ambayo ina endesha/ina linda eneo fulani (territory) sambamba na idadi ya watu mbali mbali humo ndani ya hilo eneo.

Taifa hukua na kushuka pale ambapo linatanuka kwa ushawishi kwa raia na kupata nguvu zaidi. Na mara ingine huanguka pindi linapokosa mwelekeo au kushindwa kudhibiti mambo fulani.

Wana historia huchambua maswala haya na hatua za mataifa "kukua na kuanguka" kwa kutumia falsafa ya "kuainisha/kufananisha/kulinganisha" baina ya mataifa, ambayo yaliowahi kupitia huko.

Kwa kulinganisha/kufananisha/kuainisha baina ya mataifa mbali mbali, wana historia huweza kutabiri mwelekeo wa taifa husika. Na kutoa maoni yao dhidi ya muelekeo huo. Miongoni mwa matamko waliowahi kutamka ni; ""Hatua za ukuaji wa mataifa mbali mbali duniani, huwa na mafanano na tofauti baina yao, ila mafanano ni mengi zaidi kuliko tofauti zao"".

Mataifa hukua kwa sababu tofauti, mfano;

Taifa hili la uajemi (Persian Empire), lilikua kwa kutumia njia za MABAVU, NGUVU na MAPINDUZI YA KIJESHI.

Taifa la Maurya (Maurya Empire) lilikua kwa kutumia combination za njia ya HUJUMA ZA KISIASA, KUBADILI KWA DINI, na MAPINDUZI YA KIJESHI ili kupanua dola yao.

Taifa la Roma (Roman Empire) japokua lilikua taifa la kijeshi, ila kiujumla halikua na madhumuni ya kukuza dola yao, japokua waliingia katika vita nyingi. Baada ya kushinda vita zao, walitoa uraia kwa mateka ili iwe kinga ya uaminifu. Hii ilisababisha kukua kwa taifa la Roma.

Point yenyewe (main point) ni kutambua ukuaji wa serikali kuu kitaifa, ni kwa kutanua udhibiti wa kisiasa kwa wananchi wa hilo taifa husika. Hii inawezakua kwa njia ya Kinguvu (Jeshi/Vita), Uchumi, au Utamaduni (Muda mwingine vyote huambatana kwa pamoja).

MTAZAMO WA KUKUA KWA WATAWALA,

1) ALEXANDER THE GREAT (Ukuaji wa kasi wa utawala wake).

Huyu anatambulika kama mtawala aliekuza utawala wake kwa kasi ya juu (Great Empire Builders In History). Je, kuna uwiano gani wa kukua kwa utawala wake kwa dhidi ya "tabia na uwezo binafsi" aliokua nao????.

Japokua anakumbukwa kama BABA MZAZI wa Alexander The Great, Mfalme PHILIP II wa Macedon (alie tawala mnamo mwaka 359 BCE - 336 BCE). Alikua mtwala na amiri jeshi mkuu aliepata mafanikio makubwa sana bila shaka. Alitengeneza ngazo ya ushindi wa Alexander katika vita na Waajemi. PHILIP II alitumia RUSHWA, VITA, na VITISHO kulinda utawala wake. Na kwa mtazamo wake wa kina na kujituma, historia isingemshuhudia Alexander.

Baada ya kifo cha baba yake Alexander mwaka 336 BCE, Philip II, alienda katika kutimiza mipango iliokua imeandaliwa na baba yake (kwa njia za rushwa na vitisho) ya kuangusha taifa la Uajemi.

Ushindi wa Alexander uliwashawishi raia wengi wa hali ya chini kuukubali utawala wake, bila tafakuru ya kina.

2) HANS CHINA (Mabadiliko ya ndani/Internal Reform)

Utawala wa QIN Dynasty ulidumu kwa muda mfupi sana, kutoka 221 BCE mpaka 206 BCE. Mtawala Qin, alitumia njia ya ARDHI JUMUIFU, KODI, UKALI (HARSHNESS), sambamba na utawala wa kutumia sera ya HOFU na UKANDAMIZAJI (FEAR & OPPRESSION METHODS).

Alitokea kiongozi mwingine aitwae HAN GAOZU aliehamasisha kwa uwazi kabisa UKONFUSIO (CONFUCIANISM:- sera za kuhamasisha raia kutumia jitihada na uwima) pamoja na kupunguza kodi kubwa, hofu na ukandamizwaji. Kitu ambacho kilimsababishia kuangusha nusu ya utawala wa QIN.

Mbele zaidi, utawala wa HAN ulihamasisha sera za utamaduni baina ya raia, utoaji wa elimu, uhuru, na HALI YA UTAMBULISHO WA PAMOJA (Shared Sense Of Identity). Umoja wao ulikua zaidi ya utawala wa serikali ya kati, siasa, na mahusiano ya kiuchumi baina ya raia:- It was part of a cultural Identity.

SWALI LA KUJIULIZA;- Ni vipi Utawala wa HAN uliweza kutawala kwa kutumia sera za Utambulisho Wa Pamoja, Utamaduni, Mahusiano ya kiuchumi baina ya raia, na Ukonfusio kwa KULINGANISHA/KUZINGATIA/KUFANANISHA na mikakati aliotumia Alexander The Great????

MTAZAMO WA KUANGUKA KWA WATAWALA,

Baadhi ya mambo ambayo wana historia hutumia kuelezea sababu za mataifa/watawala kuanguka ni;

1) Maswala Ya Uchumi (Economic Issues).

2) Maswala Ya Kijamii na Utamaduni. (Social & Cultural Issues).

3) Maswala Ya Mazingira (Environmental Issues).

4) Maswala Ya Kisiasa (Political Issues).

UTAWALA WA UAJEMI (PERSIAN EMPIRE):- RAPID COLLAPSE.

Maswala yaliyo changia kuanguka kwa dola ya uajemi ni Rushwa, Siasa, Jeshi. Mgawanyiko wa wanasiasa ndani ya utawala ulisababisha kudhoofika kwa umoja baina yao, kudhoofika kwa ulinzi wa jeshi na kusababisha wakuu wa majeshi kugombania/kugawana uongozi baada ya Alexander kufa, mnamo 323 BCE (The Generals divided the empire amongst themselves within a very short period of time).

SWALI FIKIRISHI;- Sababu ipi iliosababisha kudondoka kwa utawala wa uajemi,

a) Kufa kwa Alexander, ndio kulisababisha wakuu wa majeshi kugombania/kugawana uongozi?

b) Kulikua na mgawanyiko wa kisiasa ndani ya utawala wa uajemi, kwasababu ya rushwa, uasi na tamaa kabla hata Alexander hajaingia kuichukua dola?

UTAWALA WA GUPTAS (THE GUPTAS EMPIRE):- SLOW DEATH.

Utawala wa GUPTA ulikamata sehem kubwa ya India, kutoka Mwaka 320 CE mpaka 550 CE. Utawala huu ulishika kasi mnamo miaka ya 450 CE, na kuanzia hapa utawala huu ulianza kupokea mashambulizi ya ki UCHUMI na ULINZI kutoka kwa WA-HEPHTHALITIES (muda mwingine huitwa HUNS WEUPE). Mashambulizi haya yaliwaua taratibu kiuchumi, kisiasa na kiulinzi (Kijeshi) mpaka kusababishia dola yao kudhoofika, kupata umasikini, kuanguka na kutoweka kabisa.

Jambo kui lililo angusha utawala wa GUPTAS, ni kumomonyoka kwa uchumi ulilolipata, likichochewa na mitihani ya kijeshi lililokua likipata mara kwa mara. Hii iligeukia katika kudhoofika kwa SIASA baada ya serikali kudhoofika.

SWALI FIKIRISHI:- Ni vipi utawala wa GUPTAS ulidondoka kwa KULINGANISHA/KUZINGATIA/KUFANANISHA na kuanguka kwa utawala wa UAJEMI?

Cha kuchukua hapa;

- Utawala huanguka na kukua kwa sababu nyingi.

- Wana Histori huainisha sababu kuu za utawala kuanguka ni kwa msukumo wa; KISIASA, UCHUMI, JAMII, TAMADUNI au MAZINGIRA.

- Kufananisha/Kuainisha/Kulinganisha baina ya utawala fulani na utawala mwingine unatusaidia kutambua ni jinsi gani utawala unaweza kukua/kuanguka.

Ahsanteni,
Alexander The Great
 
kwa utawala wetu wa miaka mitano mitano sioni hayo yakitokea. naona watu wanahesabu bado miaka saba tule bata tena
Inawezekana na isiwezekane mkuu, hao waliokua huko nyuma kwenye hayo mataifa ni binaadam, na hawa waliopo tanzania/kenya/uganda ni binaadam pia.

Binaadam hawatabiriki, kisayansi njia pekee unaweza kuwatawala binaadam ni wakiwa hawana shida ya chakula (hawana njaa), ila wakiwa na njaa hawa tawaliki hata kwa mtutu.

Tukichambua vita za wenyewe kwa wenyewe kama Somalia/Libya na kwengine mkuu, tutazunguka kwenye vichaka vya maswala ya dini/ukabila/tamaa ya madaraka ila mwisho wa jibu itakua NJAA kwa raia ndio inasitisha mapigano. (Japo uchochezi baina ya maraifa haukosekani na ndio chanzo).

Libya walidanganywa wakaingia vitani, sasa wanajuta ila kinachowafanya vita isiishe ni DHIKI/NJAA, na ndio kinawafanya waendelee na vita.

#Human beings are CUNNING creatures. To say; Fast, Smart, Very Intelligent, Wise, Friendly/Revengeous.
 
Habari wana JF,

Leo, nimevutiwa kuandika makala hii, inaohusiana na maswala ya kukua na kuanguka kwa mataifa kwa madhumuni ya elimu kwa wasiojua (kwa wanaojua iwe ukumbusho).

NB: Ntatumia mifano ya mataifa ya zamani, yaliowahi kutokea na kupitia hatua hizi husika za kukua na kuanguka ki-dola, ili kuepusha hoja zisizo na tija.

Nirejee kwenye makala husika,

Mtazamo wa Taifa (Government/Empire):

Neno "taifa" linajumuisha mambo mengi, miongoni ya hayo ni kua na SERIKALI KUU (Central State) ambayo ina endesha/ina linda eneo fulani (territory) sambamba na idadi ya watu mbali mbali humo ndani ya hilo eneo.

Taifa hukua na kushuka pale ambapo linatanuka kwa ushawishi kwa raia na kupata nguvu zaidi. Na mara ingine huanguka pindi linapokosa mwelekeo au kushindwa kudhibiti mambo fulani.

Wana historia huchambua maswala haya na hatua za mataifa "kukua na kuanguka" kwa kutumia falsafa ya "kuainisha/kufananisha/kulinganisha" baina ya mataifa, ambayo yaliowahi kupitia huko.

Kwa kulinganisha/kufananisha/kuainisha baina ya mataifa mbali mbali, wana historia huweza kutabiri mwelekeo wa taifa husika. Na kutoa maoni yao dhidi ya muelekeo huo. Miongoni mwa matamko waliowahi kutamka ni; ""Hatua za ukuaji wa mataifa mbali mbali duniani, huwa na mafanano na tofauti baina yao, ila mafanano ni mengi zaidi kuliko tofauti zao"".

Mataifa hukua kwa sababu tofauti, mfano;

Taifa hili la uajemi (Persian Empire), lilikua kwa kutumia njia za MABAVU, NGUVU na MAPINDUZI YA KIJESHI.

Taifa la Maurya (Maurya Empire) lilikua kwa kutumia combination za njia ya HUJUMA ZA KISIASA, KUBADILI KWA DINI, na MAPINDUZI YA KIJESHI ili kupanua dola yao.

Taifa la Roma (Roman Empire) japokua lilikua taifa la kijeshi, ila kiujumla halikua na madhumuni ya kukuza dola yao, japokua waliingia katika vita nyingi. Baada ya kushinda vita zao, walitoa uraia kwa mateka ili iwe kinga ya uaminifu. Hii ilisababisha kukua kwa taifa la Roma.

Point yenyewe (main point) ni kutambua ukuaji wa serikali kuu kitaifa, ni kwa kutanua udhibiti wa kisiasa kwa wananchi wa hilo taifa husika. Hii inawezakua kwa njia ya Kinguvu (Jeshi/Vita), Uchumi, au Utamaduni (Muda mwingine vyote huambatana kwa pamoja).

MTAZAMO WA KUKUA KWA WATAWALA,

1) ALEXANDER THE GREAT (Ukuaji wa kasi wa utawala wake).

Huyu anatambulika kama mtawala aliekuza utawala wake kwa kasi ya juu (Great Empire Builders In History). Je, kuna uwiano gani wa kukua kwa utawala wake kwa dhidi ya "tabia na uwezo binafsi" aliokua nao????.

Japokua anakumbukwa kama BABA mzazi wa Alexander The Great, Mfalme PHILIP II wa Macedon (alie tawala mnamo mwaka 359 BCE - 336 BCE). Alikua mtwala na amiri jeshi mkuu aliepata mafanikio makubwa sana bila shaka. Alitengeneza ngazo ya ushindi wa Alexander katika vita na Waajemi. PHILI II alitumia RUSHWA, VITA, na VITISHO kulinda utawala wake. Na kwa mtazamo wake wa kina na kujituma, historia isingemshuhudia Alexander.

Baada ya kifo cha baba yake Alexander mwaka 336 BCE, Philip II, alienda katika kutimiza mipango iliokua imeandaliwa na baba yake (kwa njia za rushwa na vitisho) ya kuangusha taifa la Uajemi.

Ushindi wa Alexander uliwashawishi raia wengi wa hali ya chini kuukubali utawala wake, bila tafakuru ya kina.

2) HANS CHINA (Mabadiliko ya ndani/Internal Reform)

Utawala wa QIN Dynasty ulidumu kwa muda mfupi sana, kutoka 221 BCE mpaka 206 BCE. Mtawala Qin, alitumia njia ya ARDHI JUMUIFU, KODI, UKALI (HARSHNESS), sambamba na utawala wa kutumia sera ya HOFU na UKANDAMIZAJI (FEAR & OPPRESSION METHODS).

Alitokea kiongozi mwingine aitwae HAN GAOZU aliehamasisha kwa uwazi kabisa UKONFUSIO (CONFUCIANISM:- sera za kuhamasisha raia kutumia jitihada na uwima) pamoja na kupunguza kodi kubwa, hofu na ukandamizwaji. Kitu ambacho kilimsababishia kuangusha nusu ya utawala wa QIN.

Mbele zaidi, utawala wa HAN ulihamasisha sera za utamaduni baina ya raia, utoaji wa elimu, uhuru, na HALI YA UTAMBULISHO WA PAMOJA (Shared Sense Of Identity). Umoja wao ulikua zaidi ya utawala wa serikali ya kati, siasa, na mahusiano ya kiuchumi baina ya raia:- It was part of a cultural Identity.

SWALI LA KUJIULIZA;- Ni vipi Utawala wa HAN uliweza kutawala kwa kutumia sera za Utambulisho Wa Pamoja, Utamaduni, Mahusiano ya kiuchumi baina ya raia, na Ukonfusio kwa KULINGANISHA/KUZINGATIA/KUFANANISHA na mikakati aliotumia Alexander The Great????

MTAZAMO WA KUANGUKA KWA WATAWALA,

Baadhi ya mambo ambayo wana historia hutumia kuelezea sababu za mataifa/watawala kuanguka ni;

1) Maswala Ya Uchumi (Economic Issues).

2) Maswala Ya Kijamii na Utamaduni. (Social & Cultural Issues).

3) Maswala Ya Mazingira (Environmental Issues).

4) Maswala Ya Kisiasa (Political Issues).

UTAWALA WA UAJEMI (PERSIAN EMPIRE):- RAPID COLLAPSE.

Maswala yaliyo changia kuanguka kwa dola ya uajemi ni Rushwa, Siasa, Jeshi. Mgawanyiko wa wanasiasa ndani ya utawala ulisababisha kudhoofika kwa umoja baina yao, kudhoofika kwa ulinzi wa jeshi na kusababisha wakuu wa majeshi kugombania/kugawana uongozi baada ya Alexander kufa, mnamo 323 BCE (The Generals divided the empire amongst themselves within a very short period of time).

SWALI LA KUJIULIZA;- Sababu ipi iliosababisha kudondoka kwa utawala wa uajemi,

a) Kufa kwa Alexander, ndio kulisababisha wakuu wa majeshi kugombania/kugawana uongozi?

b) Kulikua na mgawanyiko wa kisiasa ndani ya utawala wa uajemi, kwasababu ya rushwa, uasi na tamaa kabla hata Alexander hajaingia kuichukua dola?

UTAWALA WA GUPTAS (THE GUPTAS EMPIRE):- SLOW DEATH.

Utawala wa GUPTA ulikamata sehem kubwa ya India, kutoka Mwaka 320 CE mpaka 550 CE. Utawala huu ulishika kasi mnamo miaka ya 450 CE, na kuanzia hapa utawala huu ulianza kupokea mashambulizi ya ki UCHUMI na ULINZI kutoka kwa WA-HEPHTHALITIES (muda mwingine huitwa HUNS WEUPE). Mashambulizi haya yaliwaua taratibu kiuchumi, kisiasa na kiulinzi (Kijeshi) mpaka kusababishia dola yao kudhoofika, kupata umasikini, kuanguka na kutoweka kabisa.

Jambo kui lililo angusha utawala wa GUPTAS, ni kumomonyoka kwa uchumi ulilolipata, likichochewa na mitihani ya kijeshi lililokua likipata mara kwa mara. Hii iligeukia katika kudhoofika kwa SIASA baada ya serikali kudhoofika.

SWALI LA KUJIULIZA:- Ni vipi utawala wa GUPTAS ulidondoka kwa KULINGANISHA/KUZINGATIA/KUFANANISHA na kuanguka kwa utawala wa UAJEMI?

Cha kuchukua hapa;

- Utawala huanguka na kukua kwa sababu nyingi.

- Wana Histori huainisha sababu kuu za utawala kuanguka ni kwa msukumo wa; KISIASA, UCHUMI, JAMII, TAMADUNI au MAZINGIRA.

- Kufananisha/Kuainisha/Kulinganisha baina ya utawala fulani na utawala mwingine unatusaidia kutambua ni jinsi gani utawala unaweza kukua/kuanguka.

Ahsanteni,
Alexander The Great
Hongera sana Alexander kwa hiyo kwa ufafanuzi huu tuseme na EMPIRE ya jiwe ieanguka? Maana naona hapa kama historia inatimia.
 
Historia ni jambo la kutufumbua macho/kutukumbusha, either tujifunze au tusijifunze, na kufuata ama kutokufuata, ina tusaidia kuangalia njia ipi tuchukue mkuu,

Na jua sijakupatia jibu lililosahihi, ila hawa mabwana wanaweza wakatusaidia kwa ufafanuzi wa kina, kwwenye hilo swali lako mkuu.
Zitto Pascal Mayalla Salary Slip GENTAMYCINE erythromycine na General Mangi
 
Hebu%20jaribu%20kueleza%20ujumbe%20una%C3%B2jitokeza%20kwenye%20mchoro%20huu%20wa%20katuni%20...jpeg
 
Inawezekana na isiwezekane mkuu, hao waliokua huko nyuma kwenye hayo mataifa ni binaadam, na hawa waliopo tanzania/kenya/uganda ni binaadam pia.

Binaadam hawatabiriki, kisayansi njia pekee unaweza kuwatawala binaadam ni wakiwa hawana shida ya chakula (hawana njaa), ila wakiwa na njaa hawa tawaliki hata kwa mtutu.

Tukichambua vita za wenyewe kwa wenyewe kama Somalia/Libya na kwengine mkuu, tutazunguka kwenye vichaka vya maswala ya dini/ukabila/tamaa ya madaraka ila mwisho wa jibu itakua NJAA kwa raia ndio inasitisha mapigano. (Japo uchochezi baina ya maraifa haukosekani na ndio chanzo).

Libya walidanganywa wakaingia vitani, sasa wanajuta ila kinachowafanya vita isiishe ni DHIKI/NJAA, na ndio kinawafanya waendelee na vita.

#Human beings are CUNNING creatures. To say; Fast, Smart, Very Intelligent, Wise, Friendly/Revengeous.

Nakubaliana na wewe.....

Na tusisahau kitu kimoja muhimu sana tunapojadili haya mambo....

Kwamba, kwa kawaida Mungu ndiye mtawala na kiongozi wa watu wote....

Kinachofanyika ni kuwa hawezi kushuka yeye mwenyewe moja kwa moja kutawala isipokuwa anatumia binadamu hawa hawa kutawala kwa niaba yake....

Kwa hiyo sisi ni mawakili wa kazi ya uumbaji wake kwa njia mbalimbali......

Na ktk kutawala huko ameweka "principles" ama sheria za kuzingatia ktk kutawala.....

Ni moja tu: Lazima utawala uzingatie HAKI kwa sababu yeye Mungu sifa yake kuu ni MUNGU wa UPENDO na HAKI....

Kwenda kinyume na kanuni hii muhimu bila kujali ulipata vipi nafasi hiyo ya utawala, atakukataa tu.....

Na kukataliwa hakuji vuu bin vuu.....

Bali hutanguliwa na "series of warnings" ikitarajiwa kuwa mtawala huyu atakuwa mwerevu wa kugundua makosa yake na kujirekebisha.....

Na kwa kuwa Mungu yeye ni wa HAKI na UPENDO husamehe na kukupa nafasi tena ya kuendelea mbele....

Kuliweka hili vizuri hebu kwa wakristo tuingie kwenye Biblia katika kitabu cha Kutoka na tuungalie utawala wa FARAO wa Misri ya kale dhidi ya Waisrael.....

Huyu bwana alikuwa ni miongoni wa watawala makatili na wenye roho ngumu na ya korosho ambao ulimwengu uliwahi kushuhudia.....

Pamoja na mlolongo wa mapigo mabaya (series of warnings) toka kwa Mungu ili asiendelee kuwafanya wana wa Israel kuwa watumwa wake, na kuwaachia kwenda ktk nchi yao, hakuwahi kusikia wala kumtii Mungu.....

Ninachotaka kusema hapa ni kuwa, kwa watawala wa dunia ya leo hayupo mwenye roho ngumu za hao uliowataja ktk andiko lako na hakuna mwenye roho ngumu kama Farao wa Misri ile ya kale BC....

Hawa wa leo, kama ulivyosema njaa tu inatosha kabisa kuwashikisha adabu na ikawa anguko lao....

Nahisi Tanzania tunaweza kuwa ndiyo uelekeo wetu huo.

Biblia inasema;

, "........ajidhaniaye kuwa amesimama, na aangalie asije anguka....."
 
Nakubaliana sana na wewe mkuu, na umefafanua jambo ambalo hatujaligusia, hapo kwenye "Kiongozi ni mungu anaekuchagua, na kutokusahau tumeupata vipi na kuacha mambo ambayo mungu anaya penda na kuyatilia mkazo (katika vitabu vya dini) ambayo naweza nikaya weka katika ""upendo, haki na heshima"".

Mfano kwingine ni ADOLF HITLER,

Huyu unyama aliofanya sidhani kama kuna binaadam katika zama hizi (tulipo) na zijazo (mbele) atakuja kutokea hata nusu yake.

Pindi alipokua na nguvu kuzidi kiongozi yoyote duniani katika zama zake (vita ya pili ya dunia). Na ndipo mungu alii staajabisha dunia kwa jinsi alivyoanguka na kuadhirika kwa muda mfupi sana.
 
WaTz lazima tukubali:- Kama watu watasema utawala fulani ni MBAYA basi wao wenyewe ndio WAMEURUHUSU. Kwa unafiki na KUJIPENDEKEZA vilivyopo kwa sasa hapa Tz sioni mwanga huko mbele. Akija mbaya sana bado kuna watakaomsifia kwa kujipendekeza kwao, na akiwepo mzuri sana vivyo hivyo. Unafiki huu usipoondoka kukawa na umoja na watu wote wakawa tayari kusema nguo hii ni nyeupe na hii ni nyeusi, kila leo hata kwa miaka mia ijayo vitakuwepo vilio tu.
 
Back
Top Bottom