Kuku wa kukaanga kwa mtindo wa Kijapani

Ila hiyo sosi ya soya ndio sijaelewa ni kitu gani.
Mkuu ni kiungo hutiwa kwenye nyama na michuzi kutokana na soya zipo sosi nyingi, ukitaka kuifahamu vizuri nenda duka la viungo ulizia mara nyingi hupatikana Zanzibar na huku bara basi maduka yale makubwa ya viungo.
 
Wao wanaita "karage".
Mahitaji (Kutumiwa na watu wa 4)
View attachment 1499403

・Mapaja 2 ya kuku (gramu 500)
・1/2 kijiko kidogo cha chumvi (gramu 2.5)
・Pilipili manga kwa ajili ya kutia ladha
・Vijiko vikubwa 2 vya sosi ya soya (mililita 30)
・Vijiko vidogo 2 vya maji maji ya tangawizi (mililita 10) juice ya tangawizi kamua.
・Unga wa ngano kwa ajili ya kupaka kwenye kuku
・Mafuta ya mbogomboga kwa ajili ya kukaangia.
Jinsi ya kupika
  1. Changanya majimaji ya tangawizi na sosi ya soya. Kipande cha sentimita 3 cha tangawizi kikisagwa au kutwangwa kinaweza kutoa kiasi cha vijiko vidogo 2 vya majimaji ya tangawizi.
  2. Kata nyama ya kuku vipande vya ukubwa wa sentimita 3, na uvipake chumvi na pilipili manga.
    howto_110701_3.jpg

    3.Weka nyama ya kuku kwenye sosi ya soya na maji maji ya tangawizi, uviache kwa dakika 10.
    4.Kausha vipande vya kuku kwenye chujio na uvipake unga wa ngano.
    5.Pasha mafuta hadi kuwa na nyuzi joto 170, kaanga kuku kwa kiasi cha muda wa dakika 4. Kwa nyama yenye mifupa, kaanga kwa dakika 7 hadi 8.
    6.Ipua tayari kuliwa usisahu kunikaribisha......
 
Kuna video moja niliona ya mbongo anapika hao kuku aisee nilihisi kuchefuka, jinsi anavyochovya chovya wale kuku kwenye yale mauji, too dirty yaani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom