KUKU WA KIENYEJI vs KUKU WA KISASA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KUKU WA KIENYEJI vs KUKU WA KISASA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Power G, Aug 14, 2011.

 1. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Wapenzi wa JF, kwa muda mrefu wakati nikiwa nyumbani Tz nimekuwa nikisikia na kuona watu wengi wakipendelea kula nyama ya kuku wa kienyeji. Hata katika maeneo yale tunayokamata moja baridi moja moto, bei ya kuku wa kienyeji huwa kubwa kuliko ya kuku wa kisasa. Nilishawahi kusikia watu wakisema wanaogopa kula kuku wa kisasa kwani wanaume wanahofia kuota matiti na akina mama wanahofia kuota ndevu. Ukweli wa jambo hili siujui ingawa nimekuwa nikichukua tahadhari ya kutotumia nyama ya hao kuku wa kisasa.

  Tatizo linalonikabili kwa sasa ni kwamba niko ughaibuni. Huku wale kuku wanaotafuta mende, funza na panzi mitaani hawapo kabisaaa. Na wala ukisema kuku wa kienyeji ni msamiati ambao ni mgumu kwa wenyeji wa hapa kuufahamu. Kuku wote waliopo ni wale wa kisasa. Nyama ya kuku ndiyo kitoweo kinachopatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu. Jamani mwenye uhakika wa madhara ya hawa kuku wa kisasa aniambie maana naogopa kurudi Tz nikiwa nimeota matiti!! Wakati huo huo ndiyo kitoweo ambacho gharama yake ni ndogo na kinaweza kunisaidia ku-save vi-dola kidogo kwa ajili ya matumizi ya ndugu na jamaa huko Tz.
   
 2. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  kuku wa ulaya hawawezi kukuuotesha matiti,we tafuna tu ukiota matiti washtaki utalipwa uongezee kwenye vidola unasave
   
 3. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  ulaya ipi unakaa?mbona kuku wa kienyeji wanapatikana..?ingia maduka ya wahindi/wapakistan ulizia 'hard chicken' utapewa?
   
 4. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Uko wapi kwani? Kama UK naweza kukuletea kuku wa kienyeji nyumbani kwako.
   
 5. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Niko Trondheim Norway. Unaweza ukaniletea hao kuku wa kinyeji mpaka huku???
   
 6. P

  Pazi JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 2,918
  Likes Received: 623
  Trophy Points: 280
  Tehteh leo umenifurahisha unaposema wa kisasa unakosea mkuu. Hata wa kienyeji anaweza kuwa wa kisasa(wasikuhizi) mie naita kuku wa kienyeji na wale kwetu tumezoea kuita kuku wa kizungu na waita, kuku "matahira" wapowapo tu hawakimbii imenenepeana wazungu wao ndio kabisa wanawachoma sindano.
   
 7. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Au nenda maduka pia ya afro Caribbean au ya west african zile nadhani jina ni pluvera (kama nimekosea sipo mbali hata ukilitamka hivi) ndio watamu zaidi kampuni hiyo ni namba 1, zinapatikana kuku mzima kwa weight imepakiwa na kunyolewa kabisa. Na pia vipaketi vya vibawa au miguu. Enjoy uliza utaelekezwa na hata hao wenyeji.
   
 8. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #8
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,403
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Mkuu kuku wa kisasa anaefugwa ulaya hana shida kwani hawachakachui kama wanaofungwa huku kwetu...wafugaji wanawalisha madawa ili wakue haraka lakini mwisho wa siku zile kemikali zina madhara kwa binadamu.
  wenzetu wapo makini sana linapokuja suala la afya.
   
 9. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2011
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 670
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  Mkuu hebu jaribu kununua h√łne kylling uone tofauti yake na hao wengine. Lakini pia kwenye English speaking countries nimekutana wako kuku wanaoitwa "Free range chicken" au "Organic chicken" hawa wanaaminika ni sawa na wa kienyeji! Maana wanajiokotea wenyewe chakula na hawafanyiwi de-beaking!!
   
Loading...