Kuku wa kienyeji baada ya kutaga uchukua muda gani kuanza kuyalalia mayai

Miguel Alvarez

JF-Expert Member
May 28, 2019
2,144
3,795
Habari za majukumu wakuu,

Naomba kuuliza hivi Kuku wa kienyeji baada ya kutaga uchukua muda gani kuanza kuyalalia mayai.
 
Maana nachangamoto ya kuku wangu ametaga mayai Kama 15 lakin ni siku kadhaa sioni kuanza kulalia je hi iko sawa
 
Mhh sidhani je kwa kawaida huwa anaanza kulalia kwa muda gani baada ya kutaga
 
Maana nachangamoto ya kuku wangu ametaga mayai Kama 15 lakin ni siku kadhaa sioni kuanza kulalia je hi iko sawa
Inategemea na aina ya kuku, wapo wanaotaga hadi mayai 22 ila wengi ni mayai 13. Kawaida akimaliza kutaga analalia moja kwa moja tena anaweza kulalia then yai la mwisho akalitaga akiwa ameshaanza kulalia.

Inawezekana huyo kuku sehemu aliyokua anatagia ina utitiri wanamsumbua ndio maana hataki kulalia au umehamisha mayai yake na kuyaweka sehemu nyingine. Pia kuna baadhi ya kuku wa kienyeji hawalalii au wanalalia lakini hawamalizi siku 21.
 
Inategemea na aina ya kuku, wapo wanaotaga hadi mayai 22 ila wengi ni mayai 13. Kawaida akimaliza kutaga analalia moja kwa moja tena anaweza kulalia then yai la mwisho akalitaga akiwa ameshaanza kulalia...
Mkuu kuku wangu Kuna mahali alitagia mazingira hayakuwa mazuri nikayaamisha lkn baada ya siku moja akataga mahali nilipomwamishia je hi inaweza kuwa sababu ya kutokulalia na je nifanyeje ili aweze kulalia
 
Sahihi kabisa kuku chotara huwa hawalalii mayai na ikitokea akiatamia baada ya muda flan atatoka kabla ya kutotoa


Niliwahi fuga kuku alikua anataga sana akimaliza atapumzka baadae ataanza tena.

But. Baadae ya muda flan akaanza kuatamia baada ya kuatamia hakumaliza siku 21 ......akaanza kutaga . tena .....so hawa viumbe hawanaga habari na kutaga.....option tafta kuku wa kienyeji wawe special kwaajili ya kuatamia.
 
Maana nachangamoto ya kuku wangu ametaga mayai Kama 15 lakin ni siku kadhaa sioni kuanza kulalia je hi iko sawa
Huyo atakuwa chotara, hao huwa hawalalii mayai

inabidi uyapeleke kwenye mashine ya kutotoleshea.hao huwa wanataga tu.
 
Asante mkuu na je wanaweza kulea watoto ukiwatotoloshea
Hao kuku wanpenda ubosi sana mkuu,ni sawa na mabinti wa masaki.Hawana time ya kulea ,wao ni kutaga tuu full stop.ukiyatotolesha vifaranga inabidi uvilee mwenyewe.Ila wanataga sana.mimi niliwahi kubadilisha.

Niliyatoa matetea yote ya chotara nikatafuta matetea yale kienyeji pure na kutumia yale majogoo chotara,nilipata vifaranga vyenye nguvu sana ya kuhimili magonjwa.

Hao chotara pure ni pasua kichwa sana
 
Hao kuku wanpenda ubosi sana mkuu,ni sawa na mabinti wa masaki.Hawana time ya kulea ,wao ni kutaga tuu full stop.ukiyatotolesha vifaranga inabidi uvilee mwenyewe.Ila wanataga sana.mimi niliwahi kubadilisha....
Mkuu unawezaje kumtambua kuku chotara na sifa zake ni zip?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom