Kuku kienyeji wanakunywa sana mayai

kitokololoo

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
704
813
Wakuu habari poleni na majukum ya kitaifa!!!
Ase naombeni msaada nina kuku wa kienyeji matetei 30 na majogoo 4 tatizo hawa kuku nahisi kama kuna mtu ananichezea kwenye kuku wangu yani kuku wanakula chakula cha kutosha pia nawafungulia njee wanaokata wadudu na wanakula majani kifupi wanakula na kushiba vzr tu chaajabu hawa kuku hawatagi vzr kabisa na wakitaga majogoo pamoja na matetei wanakunywa mayai nina miezi sita sijawahi kupata ata kifaranga kupitia kuku hawa

Eneo nawafugia ni zuri sana chumba kikubwa kina hewa ya kutosha pia napuliza dawa naposafisha banda lakini cha ajabu hawatagi vzr kabisa.
Kuku wenyewe ni wakienyeji
Wajumvi wa ufugaji naomba mnisaidie nifanye nn hawa kuku waache kunywa mayai na watage vzr na kutotoa mayai?
 
Huchezewi na mtu bali unachezewa na kuku wako mwenyewe. Tatizo umesema wanakunywa mayai tena unataka elimu ya watu wazima kugundua tatizo siyo mtu bali ni kuku wako.

Ondoa mayai baada ya kuku kutaga na uchague kuku waaminifu watano uwape jukumu la kuatamia hayo mayai. Pia kata midomo yao ili wasiwe na ncha kali ya kuweza kutoboa yai.
 
Asante kaka viatu vya samaki ngoja nijaribu ushauri wako maana naona kama nafanya kazi ya kuosha makalio ya mbwa.
 
Fika kwenye duka la dawa za mifugo au wataalamu wa ufugaji watakuelekeza. Kuku wako wanakosa madini ya calcium ambayo yapo kwenye maganda ya mayai ila kuna chakula kina madini hayo ukiwapa watapa uwezo wa kutaga zaidi mayai bila kuyala.
 
Kuku Kula Mayai Husababishwa Na Sababu Kuu Nne(4 ) : -
1.Upungufu Wa Kalishiamu (Ca).

2.Upungufu Wa Madini Ya Potashiamu (Ka).

3.Kulisha Chakula Kichache (Underfeeding).

4.Tabia Mbaya (Vices)

Tiba:-
1.Kalishiamu.Tumia Chumvi, Dcp,chokaa Au Mifupa Kama Wanakula Mayai Na Kudonoana Manyoya.

2.Potashiamu.Wapatie Majani Yakutosha Pamoja Na Mifupa Kama Wanakula Mayai Na Manyoya Yao Kuwa Rafu.

4.Tabia Mbaya.Wakate Midomo Na Kuwapunguza Kwenye Banda Kama Wamebanana Na Wanakula Mayai.

3.Kulisha Chakula Kichache.Ongeza Kipimo Cha Chakula Kama Wanakula Mayai Na Wamepungua Uzito.

Credited to Christophambinda blogspot
 
Asante kaka
Fika kwenye duka la dawa za mifugo au wataalamu wa ufugaji watakuelekeza. Kuku wako wanakosa madini ya calcium ambayo yapo kwenye maganda ya mayai ila kuna chakula kina madini hayo ukiwapa watapa uwezo wa kutaga zaidi mayai bila kuyala.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom