Kuku gani nifuge kibiashara?

Jay10

JF-Expert Member
Jul 9, 2018
707
530
Habari ya wakati huu wana Jf....!??...

Niende moja kwa moja katika mada hii husika na kichwa habari hapo juu...

Nipo katika mpango wa kufuga kuku kibiashara, hivyo naomba ushauri juu ya ni aina gani ya Kuku (chotara, kisasa au kienyeji)... Mana nimewaza wa kisasa lakini wale kuku nduguuu..... Duuh yaaan wamezubaaa kamaa....!??! Japo kibiashara wamoo...

... Anyways naomba ushaur seriously.... Nataman sasa kupata uzoefu kwa wazoefu ktk sekta hii.....nipo Moshi- Kilimanjaro.....

Nawasilisha....
 
Kama una soko la uhakika fuga kuku wa nyama broiler.
Kama hauna uhakika wa soko la kuku wa nyama fuga kuku wa mayai layers.
Usithubutu wala kujaribu kufuga kibiashara kuku wa pure kienyeji.
Ila kama upo makini kiufugaji na unataka mafanikio na mtaji wa kutosha unao,eneo zuri la kufuga unalo basi fuga kuku wa mayai my friend,angalau wasipungue kuku wa mayai kuanzia 1000 hivi utakula mema ya nchi mpaka utakinai.
 
Asante kwa ushauri ndugu,.... Je kuku chotara vp?!
 
Walojib wa mayai i think ni sawa..wa kienyeji uwe huna haraka ya hela...mie napambana na wakienyeji...nataka nifikishe walau 200 !
Kuna mentor ndo namfatisha😝
Au afuge chotara...it pays..ajiandae na msos tu maana hawalali wanakesha wanakula🙌

..vifaranga ulinunua au ulitotolesha mwenyewe?

..umepitia changamoto gani? Na ulikabiliana nazo vipi.

..tupe elimu kidogo kuhusu banda lako lilivyojengwa.

..Unadhani aina hiyo ya ujenzi ina faida, na changamoto gani.

..tueleze kuhusu CHANJO unazowapatia kuku wako.

..Una ushauri gani kuhusu changamoto ya chanjo / madawa feki.

..mwisho, tunaomba muongozo kuhusu unavyowalisha kuku wako.

NB:

..kwanini unafuga kienyeji? Je, uliwahi kufuga hao wengine ukapata hasara? Je, kwa knowledge uliyonayo sasa hivi nini ungebadilisha ktk project yako ya kwanza?
 
Nadhan ufugaj ni asili tu..toka naanza maisha nilianza kufuga ila sikua nafuga wa kuuza..kwahiyo nilikua nafuga ilimrad nipate kuku wa kula...so hata chanjo sikua nawapa..kwahiyo kuku wemgi wakawa wanarest in peace .sikua najali as nikitaka kuku napata wa kuchinja..
Last yr nikakutana na mama anafuga kuku wengi balaa..tena ana eneo dogo tu huko kahama...nikajiona mie mjinga.maana nna eneo kubwa kila sk najaza maua tu..so jan nikaanza okota mayai siwawekei kuku walalie naenda kautotoresha napata vifaranga vingi zaidi
Nawapa chanjo zote..7 dys,14 dys,21dys na wakifikisha 3mths!
Nafuga kienyeji kwasababu its a SIDE HUSTLE....sio biashara nayotegemea kwamba iniweke mjini ..
Niliwah fuga broiler miaka hiyo wakafa wote nilianza kipindi kibaya nilikua 🤰 kwahyo usimamizi ukawa F,
Changamoto nnayopata kipinfi hiki cha mvua kuku zimekufa aisee ...lakini naambiwa ni kwasababu ya hali ya hewa,
Ulishaji nawapa chakula special wanadai ukiwapa pumba tu wanadumaa..kwahuo wakiwa wadogo had mwez 1 nawapa kile chao special starter wakimaliza hicho nawabadilishia..
Changamoto nnayokumbana nayo nimeambiwa banda ni dogo coz kila wk napokea kuku...kwahyo wanabanana...ndo nikaambiwa pia sababu ya kufariki ..kwahyo nimewakatia vizimba nikaweka singboad kutenganisha ukiwamix wakubwa na wadogi wanaonewa sana wanang'atwa sana .na wanamaliziwa msos na wakubwa .yaan usiwamix waliofikisha 2wks na wapya wa siku 1 ..ni headache kwakweli...so this wk ninastop kupeleka mayai nikomae nao hawa kwanza,
La mwisho nilinunua pia hawa machotara kama kuku 40🙌🙌🙌 chotara anakula usk mzima..kwahyo changamoto ni hiyo wanakula mno mno mno afu wanavurugu balaa ....hawa niliamua kumix ili nipate mbegu fulan maana nna kuchi pia...kwakweki wanakula sijapata kuona na kilo 1 nanunua 1300! Kuku kirnyrji 10 wadogo wanakula kilo 1 kwa siku 2 ..chotara masaa3 hakuna msosi!
 
Ufugaji ni noma sana nataka niamie huko rasmi kwa kwelii… nifuge kuku wa mayai inabdi niende mahali nikapate shule nzito Sanaa kuhusu ufugaji huu alafu niwe serious sasaa..!!!
Jiran yangu hajamaliza nyumba yake nikimanisja hajaweka tiles..so sebule yake ameopt kufugia...yaan analala.na kuku....yaan siku anavyowapeleka msamv unabak kushangaa...yaan anapeleka had kuku 200 at per...! Namanisha pure kienyej..anauza.12000 awe jike au jogoo
 
Je, una mtaji wa kutosha?!

Kama una mtaji wa kutosha basi fuga kuku wa mayai! Mbegu za siku hizi ni bora sana kiasi kwamba, ukifuata kanuni bora za ufugaji basi kila siku utaokota mayai hadi 90% ya idadi ya kuku wako!

Hii maana yake ni kwamba, ukiwa na kuku 1000, basi kwa siku unaweza kupata mayai 900 ambazo ni trey 30.

Ninaposema kanuni bora za ufugaji ni pamoja na banda ya kisasa lenye ventilation ya kutosha na hivyo kuwawezesha kuku kupata hewa ya kutosha, and in turn, kutokuwa wavivu wa kula! Kuku akila vizuri ina-guarantee utagaji mzuri!!

Ninaposema kanuni bora za ufugaji pia tunaangalia utolewaji wa chanjo at the right time!! Ukishajenga tu banda, kabla hujaweka kuku, onana na mtaalamu wa mifugo akushauri!!!

Ninaposema kanuni bora za ufugaji ni pamoja na kutowabania chakula! Kuku anayepunjwa chakula hawezi kutaga vizuri lakini kwa bahati mbaya sana, chakula cha kununua ni very expensive, ndo sababu ya watu kuwabania kuku chakula bila kujua utakuwa unawabania kutaga vile vile!!

Kwavile chakula ni very expensive, unashauriwa kutengeneza mwenyewe kwa kutumia formular maalumu, na sio kuchanganya changanya tu hovyo hovyo!!!

NInaposema kanuni bora za ufugaji ni pamoja na kuhakikisha banda linakuwa safi and free from majimaji! Banda chafu na lenye maji maji ni chanzo cha magonjwa kwa kuku!!

Ninaposema kanuni bora za ufugaji, ni pamoja na kuweka kitu cha kupangusia miguu kwenye mlango wa banda ili kuhakikisha hutoi vijidudu huko nje na kuingia navyo bandani! Hakikisha hiki kifutio kinakuwa disinfected regularly!

REMEMBER, kuku anaweza kutaga kwa miaka 2 (miezi 24) however, wakishafikisha miezi 18 rate ya mayai itakuwa ina-drop! Best economic practice ni kufikiria kuwasimamisha ikishafika miezi 18 hata kama bado wanataga UNLESS ujiridhishe idadi ya mayai wanayotaga inakupa pesa ya kutosha kuweza ku-cover costs zote, na wewe kubaki na faida!

REMEMBER, bei kubwa ya vifaranga utakuja ku-compansate kwa kuuza hawa kuku unaowaachisha kutaga!!

Katika hali ya kawaida, kila siku utakuwa unaingiza almost 50% ya total variable costs, na kama chakula unatengeneza mwenyewe, basi utakuwa unaingiza over 50%!

REMEMBER, kuku wa mayai unawahudumia angalau miezi 5 bila kuingiza hata senti 5... yaani ni kukuchomoa tu!

That being said, make sure una mtaji wa kutosha, and to be safe, weka kiasi pembeni ambacho hicho kitakuwa kwa ajili ya kuhudumia kuku tu... especially chakula!!!

Usipofuata ushauri huo hapo juu, kuna hatari itafika siku au hata wiki huna pesa na kuku wanahitaji kula! Matokeo yake, utaanza kuwabania msosi!!!

Kwa maana nyingine, kama huna mtaji wa kutosha basi anza na kuku wa nyama lakini pia hakikisha unafuata kanuni hizo hapo juu kwa sababu na washikaji na wenyewe wanakula balaa!!!

HOWEVER, make sure unapata uhakika wa soko kwamba na usipofanya hivyo, utalazimika kuendelea kuwalisha wakati walitakiwa tayari wawe sokoni, na hivyo kukuongezea gharama zisizo na msingi, and in turn loss or faida kiduchu!

Kuku wa Kienyeji sikushauri unless kama unataka kufanya Free Range; ufugaji ambao sio mzuri kibiashara!!!
 
mkuu mimi pia kienyeji nataka niwe natotolesha na mashine inawezekana??? Maana ninao wachache na pia nataka mwezi wa saba nitafute hata 1.5MIl niitumbukize kwa kuku wa mayai itabidi nitafute mtu wa kunipa shule ya kiwango cha chakula na chanjo maana eneo ninalo.
 
mkuu umeongea point mpaka daah…!! ofcoz hapo kwenye kukadiria chakula cha kuku ndo changamoto kubwa maana ukienda vibaya unapata loss mimi nimenunua watano wale ambao tayari washapata chanjo zote na washaanza kutaga yani mkuu chakula cha layers mash ukiwa bila kuwabania wanweza maliza roba kwa week tu limeishaa...so sometimes nachanganya na pumba kidogo
 
Inawezekana..na mm natotoleshea huko...1.5m.kwa hao.kuku unajidanganya ndogo itaishia kununua vifarqnga
 
mkuu umeongea point mpaka daah…!! ofcoz hapo kwenye kukadiria chakula cha kuku ndo changamoto kubwa maana ukienda vibaya unapata loss mimi nimenunua watano wale ambao tayari washapata chanjo zote na washaanza kutaga yani mkuu chakula cha layers mash ukiwa bila kuwabania wanweza maliza roba kwa week tu limeishaa...so sometimes nachanganya na pumba kidogo
Yaani mapato ya kuku, yanaishia kwenye chakula, ndo maana kama unafuga kibiashara ni vizuri sana mtu ukawa unatengeneza chakula mwenyewe!
 
kweli kabisa mkuu… sasa hapo kwenye kutengeneza mwenyewe lazima ujue vyakula gani unanunua na unamix kwa ratio gani ili usikosee maana hawa kuku ni balaaaa wanakula viwavi wakasome.
 
Ukitaka kuwa precise, basi unatakiwa kuonana na watu wa Animal Science kama wale wa SUA! Utaeleweshwa kwa saa chache tu, na utaelewa!!
 
Back
Top Bottom