Kuku aina ya SASSO wakiwa na siku 52

Ni kweli ni wazuri mimi niliwapata kutoka silverlands. Ila wanashida moja inayonikera! Wanadonoana sana japokuwa nawapa Chakula muda wote na vitamins zote zinazotakiwa. Mpaka sasa wameshakufa watano kwa kutoboana matumbo, na wanawiki tano sasa.
 
Ni kweli ni wazuri mimi niliwapata kutoka silverlands. Ila wanashida moja inayonikera! Wanadonoana sana japokuwa nawapa Chakula muda wote na vitamins zote zinazotakiwa. Mpaka sasa wameshakufa watano kwa kutoboana matumbo, na wanawiki tano sasa.
Punguza midomo yao pia wawekee majani yakutosha huwa inasababishwa na upungufu wa madini ya chuma pia inawezekana ni tabia ya hao kuku
 
Majani kwa maana ya mboga mboga? Kama mchicha, ndicho unachomaanisha mkuu
Ndio pia kuna majani yakawaida kama makengera , majani ya magimbi na mengineyo kama huna unaweza kuyapanda yakamea ktk bustani kwa ajili ya kuku
 
Mimi nami nilisikia sifa zake nikawanunua january 21 wakiwa wa day one, vifaranga vilikuwa vikubwa mpaka raha...nikawapa chanjo zote kwa kufuata taratibu zinazoshauriwa. Lakini mwezi wa 6 walipukutika kama maji kwa ugonjwa wa mafua...hawakusilia dawa wala nn..ikinifanya nikate tamaa.

wale waliobaki hawajataga mpaka leo.


kwa uchunguzi wangu si wavumilivu kwa magonjwa wala njaa!!


sitaki kabisa kuwasikia hawa kuku..wa malawi wako vizuri sana.
Nitaendelea kuwafuga wa malawi
Yaani umeongea pointi, hawa Kuku wapo kwa ajili ya kuserve the same purpose kama boiler jaribu kufuatilia vipeperushi vyao. Hawatagi hata wakitaga ni kidogo, wadhaifu kwa magonjwa na nyama yake haikomai. Utakuta kuku umbo kubwa lkn ukimchinja nyama take teke sana.
 
Wakuu sijaacha kufuga kuku ,kwa sasa nafuga kuroiler na aina zingine .kwa ajili ya kutaga na wanataga kweli kweli ukiwajulia.na pia nauza majogoo tu Mbegu nzuri kwa bei 20,000@
 
Back
Top Bottom