Kuku aina ya SASSO wakiwa na siku 52

Mie sitaki kabisa kuwasikia hao Sasso. Nilinunua vifaranga 200 kutoka kwa Nzowa Enterprises pale Kibaoni-Tegeta. Jamaa walinichanganyia umri tofauti tofauti kinyume na makubaliano. Kilichofuatia ikawa vigumu kujua yupi amepata chanjo ipi; na ipi au yupi hajapata. Waliopoanza kuugua, nilirudi Nzowa kuwaeleza tatizo la vifaranga walivyoniuzia lakini hawakunipa ushirikiano wala msaada wowote. Vifaranga walipukutika mpaka nikachanganyikiwa. Waliofikia umri wa mauzo ni 83 tu!
pole sana hawa watu waliwahi kunifanyia hivyo, nilinunua kuku 100 nikawambia waniwekee majogoo kumi tu, walikuwa na umri mwezi mmoja, yaani nusu yote waliweka majogoo
 
Wadau kuku wazuri wa mayai ni aina gani ukiwatoa hawa Sasso ambao wamekuja ndivyo sivyo?
 
Fuata kanuni zote za ufugaji bora utawapenda hawa kuku usisahau wape chakula cha silver land
Mkuu chakula cha silverlands ni mkasi sana huku mwanza ni 80,000 kipakage cha kilo hamsini. Na nitawapa chakula hiki mpaka wafikie muda gani au mpaka wakati wa mauzo?
 
niliwalisha stater mwezi mmoja sasa nawalisha grower mwezi na mwezi wa tatu nawalisha finisher ...
kuku wako vizuri sana napingana na hao wanaosema hawafai tena nawafungulia nje kwa sasa na ninawapa chakula mara tatu kwa siku
kuku unatakiwa ujali usafi na uwe karibu nao

kwangu nafuga aina tatu za kuku
1.malawi
2.kienyeji pure croos na israel
3.sasso

katika wote nimewakubali sana sasso na hao israel malawi nimewachukia kwasababu wanakufa kwa kunya chokaa na wanakula kupitiliza japo bado ninao
Mkuu umewahi kufuga Kuroiler pia? Wakoje? Kwa Tanzania wanapatikana wapi?
 
Sasso Ni Kuku Wazuri, Tena Kutoka Nzua enterprises Tegeta, Mimi Nimenunua Hapo Ingawa Nilipata Shida Za Vifo Lakini Ni Wazuri Na Ukufuga Kwa Lengo Utafanikiwa
 
Back
Top Bottom