Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Singida pia kuwa makini unaweza kuagiza huku ukaambulia hasara kabisa wenyeji wa huku Mara nyingi huuza kuku akiwa na tatizo labda upate kwa mkulima unaye mwamini na sivinginevyo usije ukaenda kununua kuku wakufuga sokoni. Tuwa makini wakulima wenzangu, kuna hasara zinazoweza kuepukika .Pure kienyeji agizia dodoma au singida
Sawa mkuu Mimi niliwachukua 100 wa umri wa siku moja kuna baadhi ya changamoto nami nimezi pata kama wakulima wenzangu walivyo eleza hapa.Sasso wanaozalishwa na Silverland ndo hao wanaosambazwa na Nzowa Enterprises!
Mkuu vp kuhusu kuku KUROILER??Hawa Sasso nahisi huwezi kuwatenganisha na ugonjwa wa mafua. Tena huwa wanayapata wakiwa na umri wa miezi minne na kuendelea. Ni kuku wa kijinga sana. Hata bure siwataki.
"Kwa Ukali".hao nimenunua hapo hapo mkuu na hao walikuwa 200 waliokufa hadi sasa ni 10 hadi sasa wanaendelea vyema kama unavyoona .
hao jamaa wana branch pale ubungo na nilinunua wa malawi 250 ambao wana miezi minne sasa walinichanganyia walivyofika wakaanza kuza hovyo vifaranga 30 ndani ya week sikukubali niliwarudia kwa ukali wakamtuma daktari wao akaja kucheck mazingira nayofugia ila hakukuta kasoro ilibidi wanifidie vifaranga waliokufa......
Nzowa au NZUA?Sasso wanaozalishwa na Silverland ndo hao wanaosambazwa na Nzowa Enterprises!
afadhali wewe umenipa moyo kidogo,nilivyosoma comments za watu kuhusu sasso nikawa nachanganyikiwa!niliwalisha stater mwezi mmoja sasa nawalisha grower mwezi na mwezi wa tatu nawalisha finisher ...
kuku wako vizuri sana napingana na hao wanaosema hawafai tena nawafungulia nje kwa sasa na ninawapa chakula mara tatu kwa siku
kuku unatakiwa ujali usafi na uwe karibu nao
kwangu nafuga aina tatu za kuku
1.malawi
2.kienyeji pure croos na israel
3.sasso
katika wote nimewakubali sana sasso na hao israel malawi nimewachukia kwasababu wanakufa kwa kunya chokaa na wanakula kupitiliza japo bado ninao
Kweli kabisa, kulea vifaranga wa siku 1 kunahitaji utaalamu sana. Mbeya huwa tunanunua wa mwezi 1.hao hata asiye na utaalamu mkubwa anaweza watunza,unajua watu wanapenda kukurupuka kulea vifaranga kuna htaj tahadhali ya hali ya juu,andaa mazingira kwanza kabla ya kuanza fanya survey uone wenzio wanafanyaje jipe mda wa kujifunza den ndo uanze ukiandaa mazingira vzur utafurah na ukikurupuka utachukia kila breed tujipe muda wa kujifunza wajameni
Kweli kabisa, kulea vifaranga wa siku 1 kunahitaji utaalamu sana. Mbeya huwa tunanunua wa mwezi 1.hao hata asiye na utaalamu mkubwa anaweza watunza,