Kukosoa au kutofautiana ni DHAMBI kubwa kwenye vyama vya siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukosoa au kutofautiana ni DHAMBI kubwa kwenye vyama vya siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Landson Tz, Jan 5, 2012.

 1. L

  Landson Tz Senior Member

  #1
  Jan 5, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 113
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Kutokana na mtindo uliyoibuka wa viongozi wa umma kufukuzwa uanachama na hatimaye kupoteza sifa ya kuwa viongozi ni tatizo kubwa na mtihani katika kupima demokrasia ya nchi hii. Waanzilishi katika vyama vya upinzani CHADEMA walianza kwa kuwafukuza madiwani watano, Arusha. Dhambi hii ikasambaa hadi NCCR wkawafukuza uanachama akina Rungwe na Kafulili, sasa na CUF zamu yao imewafikia kutenda dhambi hiyo, Hamad Rashid na wenzie tayari wamefukuzwa chama.

  Tukimbilie wapi? maana tulidhani walioweka kifungu dhalimu kwenye katiba, kinachowanyima wasio wanachama kunusa hata harufu ya uongozi nchi hii wakati katiba inasema kila raia ana haki ya kuchagua au/na kuchaguliwa ni CCM, kumbe ni kitamu kwa vyama vyote. SASA NANI ATAPINGA UDHALIMU HUU KAMA ILIDHANIWA NI DHAMBI YA CCM, SASA VYAMA VYOTE VIMEIONJA.

  Hakuna heshima kwa mpiga/mwnanchi kama anachagua mwakilishi wake alafu wanajiita viongozi wa kitaifa huko juu wanamfukuza bila hata kuomba radhi kwa wananchi waliomchagua!
  DAWA NI KUWA NA MGOMBEA BINAFSI, TULIPIGIE DEBE KWENYE KATIBA MPYA.
   
 2. Silly

  Silly JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  I support, we need some kind of democracy within our parties, we cannot afford to hold silly elections because of petty party issues..
   
 3. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Safari yetu kisiasa ni ngumu sana, wale wote wanaojaribu kutofautiana au kuwakosoa viongozi wao kwenye vyama vyao, wamekutwa na yaliyowakuta. Labda ni kwa sababu karibu viongozi wote wa vyama vya siasa wanatokana na CCM kwa hiyo ama wako pale kwa maslahi ya CCM, au ni mfumo waliourithi kutoka CCM.

  Nawahurumia wote waliochini ya viongozi wa aina hiyo, maana ni kama wameshika mipini, ukijifanya mjanja kama Kafulila, au kama Zitto, au kama Hamad, kaa mkao wa kuadabishwa maana hutaki kudumisha fikra za Mwenyekiti wako au mkuu wako.
  Ni pale tu, vyama hivi vitakapopata viongozi na si madikteta kama tuliyonayo sasa, hii dhambi ya kukosoa na kutofautiana itakwisha.

  Hata humu ndani tumerithi tabia hiyo hiyo, ole wako uonekane unavikosoa vyama vyao pendwa au viongozi wao wapendwa humu, utatukanwa hadi ufananishwe na Malaria Sugu, labda ukosoaji huo utoke kwa watu wa aina ya Mwanakijiji and the likes, utaonekana wa maana.
   
 4. T

  The third Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwasababu kila alie juu ataki kushuka chini japo kuwa mambo wanayo
  yasema ni yakweli mfano seif shalf hamad baada ya kupewa kuwa makamu
  wa kwanza wa rais ukatibu mkuu wa chama kausaau kabisa kabisa kuzunguka katika mikoa
  ya Tanzania na wilaya zake kuamasisha chama ajafanya toka ashike nyazifa iyo.
   
 5. k

  kabuga Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na je kuwafukuza wana Chuo ambao wamepishana mitazamo na uongozi wa chuo ndosuluhisho ya matatizo vyuoni?
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  kufukuzana koote si kuzuri iwe chuo au kwenye vyama, haka kanchi ni ketu sote na vyama ni vyetu sote tusifukuzane kwa kutofautiana mitazamo. Tukae na tuyamalize kwa amani sisi soote ni ndugu! hii nchi iwe ya furaha ka kila mtu!
   
Loading...