Kukosekna kwa Mwandishi bora katika uandishi wa mitandao(online journalism) ni Pengo kwa MCT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukosekna kwa Mwandishi bora katika uandishi wa mitandao(online journalism) ni Pengo kwa MCT

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by qq.com, Mar 31, 2012.

 1. qq.com

  qq.com JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2012
  Joined: Jan 9, 2012
  Messages: 370
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wanabod
  Kwanza naomba sana Mod msiunganishe hii thred na nyingine inajitegemea.

  Kwakweli nimetazama namna utoaji tuzo kwa waandishi nchini tz ulivyoendeshwa jana usiku,lakini nimeshangaa kuona wanasahau mchango wa uandishi katika mitandao ya kijamii.

  mfano JF ni mtandao pekee wa kijamii nchini tanzania ulioweza kuripoti LIVE tukio hilo kupitia thread hii ya mdau Byabato(sijui aliwezeshwa na JF,alifanya mwenyewe au ilikuwaje) lakini inatosha kusema kuwa JF ilitoa taarifa za papo kwa papo kuhusu lile tukio.

  Aidha mitandao iliyofuatia kama blogs mbalimbali na FB zimetoa taarifa hizo leo jumamosi wakifuatiwa na baadhi ya redio nchini.

  AJABU ni kuwa TV za tanzania zitaanza kurusha tukio hilo kuanzia leo mchana na usiku wakati magazeti yatatanagza kesho jumapili.

  ukitazama mlolongo huu,utakubalina nami kwamba mitandao ya kijamii nchini(online journalism) ni njia ya kisasa kabisa na ya haraka katika kuhabarisha jamii.hivyo ni lazima waandaaji wa tuzo kama hizi kutuelekeza huko badala ya kugangania waandishi wa magazeti ambao wanatupatia habari tulizokwisha jua tena kwa live.(mfano kesho umapili,gazeti la mwananchi watachapisha katika uk wa 1 juu ya mwandishi wao Nevile meena kuibuka mshindi wa jumla,hivi nani atanunua hgazeti kwa kutaka kujua hilo).

  MCT,wadau wa sekta hii na waandishi wa habari wenyewe muda umefika kutambua kuwa uandishi wa kwenye mtandao kwa sasa ndiyo kimbilio.ikiwezekana kwenye tuzo za 2012 (tazama aljazeera.CBS News,Fox nk wao kwa sasa wana-broadcast live kupitia internet na watazamaji kibao.)


  Nawasilisha

  QQ.COM
   
 2. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160

  kwa hapa JF ingepata tuzo hii bila chenga
  wao MCT sijui kama wanalijua hili
   
 3. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  nimeptia BLOG ya michuzi muda mfupi ambayo hujinadi kuwa inaongoza kwa klupost matukio ya kibongo lakini hakuna lolote kuhusu tukio la jana
   
Loading...