Kukosekana kwa uwiano kati ya Elimu itolewayo Vijijini na Mjini.

Kagondo

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
296
79
Habari za muda huu mwana Jf.
Kwa muda mrufu imekuwepo lawama mbalimbali kuhusu huduma za kijamii hususani Elimu, imeonekana kuwa shule za mjini zinapewa kipaumbele kupata elimu bora zaidi ya zile za vijijini.

pia, hii uwenda inachangiwa na hali ya miundo mbinu na huduma shirikishi za kijamii zinazopatikana sehemu zote mbili, vijijini na mijini.

waalimu hawapendi kuishi au kufundisha shule za vijijini kwa sababu hakina huduma za kijamii rafiki.

Tatu ni kwamba, mipango mikakati ya ufikishaji wa huduma hizi vijijini, hukomea mijini kutokana na uimara wa miundo mbinu.

Ombi langu kwa vyombo husika, tafadhali tunaomba msaada, ili na sisi huku vijijini tuweze kupata huduma za elimu zinazowiana na wazipatazo wa mjini, kwani mtihani ukitungwa unakuwa mmoja kwa wanafunzi waote.
 
Back
Top Bottom