Kukosekana kwa ukweli na uwazi, siasa safi na uongozi bora katika utawala wa Hayati Dkt. John Magufuli ndiyo chanzo cha ubadhirifu na ufisadi huu

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za serikali (CAG) mwaka 2019/2020 imesomwa na inaendelea kujadiliwa bungeni...

Hali ni mbaya sana. Karibu kila wizara na taasisi/mashirika ya umma ni upotevu wa mabilioni ya fedha yasiyoeleweka na kutokuwa na ushahidi zimetumika kufanyia nini.

Kubwa na la kushangaza zaidi kiasi cha kumwacha kila mtu mdomo wazi ni kauli ya Spika wa Bunge Ndg Job Ndugai kushauri na kupendekeza mradi wa ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo uliobuniwa na serikali ya awamu ya nne chini ya CCM ya Rais Jakaya Kikwete uendelee kwa maelezo kuwa wakati ule mwaka 2016 utekelezaji wake ulipostishwa eti ni kwasababu serikali ya awamu ya 5 chini ya CCM ya Rais hayati Magufuli ilishauriwa vibaya.

Kila mmoja wetu anaelewa kuwa moja ya jukumu kuu la Bunge ni KUISHAURI, KUILEKEZA NA KUIKOSOA SERIKALI ktk maamuzi na utendaji wake wa siku kwa siku.

Kumbukumbu ziko very clear kuwa, tangu mwaka 2015 mara baada ya uchaguzi mkuu ulioiweka madarakani serikali ya awamu ya 5 ya CCM ya Magufuli, spika wa Bunge la JMT alikuwa ni huyu huyu Ndugai.

Ingekuwa vyema akatueleza watanzania yeye na wabunge wenzake wanawajibika vipi kwa kumshauri Rais vibaya na kuisababishia nchi hasara kubwa ya mabilioni ya shilingi na tutawaamini vipi kuwa huyu aliyepo watamshauri vizuri.

Pamoja na hayo yote, sababu kuu ya kuwepo kwa ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha serikalini ni kukosekana kwa UWAZI na UKWELI ktk kipindi chote cha utawala wa Rais Magufuli (marehemu).

Hili pia lilichangiwa kwa kiasi kikubwa na Bunge la Job Ndugai kwa ungozi wake mbovu uliosababisha Bunge kushindwa kutimiza wajibu wake.

Ndilo Bunge lililopitisha sheria nyingi za kuminya au kunyamazisha sauti za wananchi, uhuru wa maoni, uhuru wa kujieleza, uhuru wa kupata habari nk na kila kitu kikawa kinafanyika gizani.

Jambo lolote linalofanyika gazani siku zote ndugu zangu haliwezi kuwa zuri bali huwa ni baya tu. Bunge ndilo lililopitisha utaratibu wa vikao vya bunge kutorushwa live na vyombo vyetu vya habari.

Bunge ndilo lililokuwa linamuunga mkono Rais Hayati John P. Magufuli kwa kila kitu alichokuwa anaamua kukifanya bila kujali utaratibu umefuatwa au la.

Sote tunafahamu kuwa maamuzi ya matumizi ya fedha za umma kwa ajili ya miradi mbalimbali yalikuwa yanafanyika Ofisi ya Ikulu ya Magufuli Magogoni au Chamwino au Chato na Bunge kuletewa baadae kinyume cha taratibu kuja kupitisha kwa kutia muhuri tu bila ya kujadili kwa kina kwa kupima faida au hasara kila propose ya serikali.

Mfano wa baadhi ya miradi hiyo iliyokosolewa na kulalamikiwa sana kwa kutofuata utaratibu ni ufufuaji wa shirika la ndege Tanzania - ATCL, ujenzi uwanja wa ndege Chato, Ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka DSM - Tabora - Mwanza kisha Tabora - Kigoma, mradi wa umeme - Nyerere Hydro Electric Dam nk nk

Sasa leo inashangaza Bunge letu hili hili kupitia Spika wake wanaposhangaa kuona uchafu wa maamuzi yao uko hadharani.

Ni kweli kabisa, Tanzania tunashindwa kuendelea kwa kasi kwa sababu ya ukosefu wa mambo mawili tu; SIASA SAFI na UONGOZI BORA. Hii hupelekea mambo yote kufanyika gizani na kukosa UWAZI na UKWELI wa kinachofanyika.

Rais Mama Samia Suluhu Hassani usipite ktk barabara hii. Na wewe utapotea hakika.
 
Back
Top Bottom