Kukosekana kwa huduma bora za dharura na wa wataalam wa magonjwa ya dharura afrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukosekana kwa huduma bora za dharura na wa wataalam wa magonjwa ya dharura afrika

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Karata, Apr 9, 2012.

 1. K

  Karata JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2012
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Kifo cha Rais wa Malawi, Bwana Bingu wa Mutharika na Msanii wa filamu wa Tanzania Bawa Kanumba (The great) vinaonyesha jinsi gani Afrika tunavyokabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Huduma za Magonjwa ya Dharura. Mifano hiyo miwili inaonyesha jinsi gani, tatizo hili lilivyokuwa kubwa Afrika, kwa mfano baada ya Rais Bingu wa Mutharika kupatwa na tatizo la moyo wake kusisimama (Cardiac Arrest) alikimbizwa hospitali ya Lilongwe na gari ya kawaida, si Ambulance kisha alionekana akiingizwa hospitalini kwa kutumia baiskeli ya matairi mawili (Wheelchair), mgonjwa wa ''Cardiac Arrest'' anakimbizwa hospitali na Gari ya kawaida kisha anaingizwa hospitali na ''Wheelchair'''??.

  Aidha, kifo cha msaanii wa filamu Tanzania, Bwana Kanumba kilichotokea jana saa 9 usiku nacho kimetokea katika mazingira hayo hayo, alianguka nyumbani kwake, hakuna huduma yeyote ya dharura aliyopewa wakati alipokuwa anakimbizwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili na kufia njia, hakukuwa na ''Ambulance'' iliyomkimbiza Muhimbili??. Hii ni mifano tu ya vifo vilivyotokea Afrika vilivyosababishwa na magonjwa ya dharura, kwa mawazo yangu ni vifo vilivyoweza kuzuilika kama kungekuwa na huduma bora za magonjwa ya dharura katika nchi hizo. Viongozi wengi wa nchini za Kiafrika, Tanzania ikiwemo hazitilii mkazo kabisa, kuimarisha huduma za magonjwa ya dharura katika nchi zao, na pindi wanapopatwa na magonjwa ya dharura watu wao, huwa na mawazo ya kuwakimbiza nchi za nje kama South Africa, Israel au India, lakini wanasahau kuwa magonjwa ya dharura yanapotokea kunakuwa hakunaga muda wa kupoteza (time is critical), ukishazipoteza dakika za mwanzo, hakuna utakachoweza kufanya kumuokoa mgonjwa hata kama mgonjwa atakimbizwa kwenye hospitali iliyobora kiasi gani.

  Huduma za magonjwa ya dharura zinaanza mara moja katika eneo la tukio, Wataalam wa magonjwa ya dharura (Emergency Medicine Specialists) wanaitwa eneo la tukio maramoja na kufika kwenye eneo la tukio na gari ya kubeba wagonjwa (Ambulance) haraka huku wakiwa na vifaa tiba vya huduma ya kwanza tayari kuokoa maisha ya wagonjwa. Katika nchi zilizoendelea huduma za magonjwa ya dharura ni za hali ya juu, huduma hizo zinafaamika kwa wananchi wote, elimu ya magonjwa ya dharura zinatolewa kwa wanchi wote na wanafahamishwa nini cha kufanya pindi inapotokea dharura, kuna namba maaluum ambazo unapiga na watoa huduma hufika katika eneo la tukio haraka, lakini katika nchi za Afika ni kinyume chake. Hali ni mbaya, kinachosikitisha ni watawala wa nchi za Kiafrika kutotilia mkazo huduma hii, ikiwa wao ni watu ambao wapo kwenye hatari na kupatwa na magonjwa ya mstuko kutokana na mazingira ya kazi zao za siasa ambazo zina ''stress'' kubwa na kama wataendelea na dharau zao za kutoimarisha huduma hii wataendelea kuangamia maana watakapopatwa na magonjwa ya dharura majukwaani hakutakuwa na mtu wa kuwasaidia ''and their life will at stake''

  USHAURI

  Viongozi wa Afrika haraka imarisheni huduma za magonjwa ya dharura kwa kuwajengea uwezo wataalam wao wa ndani kwa

  1. Kusomesha wataalam wengi wa magonjwa ya dharura (Emergency Medicine Specialists), kuanzia ngazi ya vyeti (Certificate), stashahada (Diploma), Astashahada (Advanced Diploma), Shahada (Degree) na Udhamili (Master), wakiwemo paramedics.

  2. Kununua vifaa tiba vya kisasa vya magonjwa ya dharura na kuviweka katika hospitali za Wilaya, Mkoa na ngazi ya Taifa, pamoja na kuweka na vifaa vya msingi katika Zahanati zote na Vituo vya Afya.

  3. Kununua magari ya wagonjwa (Ambulance) yenye vifaa tiba ndani yake na kufanya gari hilo kutoa tiba ya dharura kuanzia kwenye eneo la tukio na katika safari nzima kuelekea hospitali au kituo cha Afya. Magari haya ya wagonjwa yasambazwe katika hospitali na vituo vya afya vyote.

  4. Maslahi ya watoa huduma za dharura yaboreshwe ili wapende kufanya kazi yao muhimu ya kuokoa maisha ya watu

  5. Kutoa elimu ya umma endelevu kuhusu huduma za magonjwa ya dharura ikiwemo huduma ya kwanza na jinsi gani ya kutoa huduma hiyo kwa watu walipatwa na magonjwa ya dharura majumbani, maofisini, kwenye viwanja na kumbi za starehe n.k.. Elimu hiyo ianzie mashuleni.

  6. Mawasiliano ya kati ya wataka huduma na watoa huduma yaboreshwe, kwa mfano kuwe na namba maalum ambayo itatumika kuombea huduma za dharura kama ''Ambulance'' ambazo wananchi watapiga bure (free call) kwa mfano 911. Wanachi wote waelimishwe uwepo wa namba hizo za dharura na jinsi ya kuzipiga.

  7. Kuwe na Sera ya Afya ya huduma ya magonjwa ya dharura.

  Kama yote hayo hapo juu yatakelezwa na Viongozi wa Kiafrika, maisha ya watu wasio na hatia yataokolewa wakiwemo wanasiasa wenyewe. Vifo vya kina Kanumba na Bingu wa Mutharika vingeepukika. Kwa mfano Kanumba kaanguka nyumbani kwake saa 6 usiku na kapelekwa hospitali ya Muhimbili saa kumi na moja alfajiri, imechukua zaidi ya masaa 5 kumfikisha Muhimbili huku akiwa amekosa kabisa huduma ya dharura ya msingi kuanzia nyumbani kwake.

  Tutafakari Waafrika kisha tuchukue hatua.
   
Loading...