Kukosekana kwa amani DRC Congo ni pigo kubwa sana kwa Tanzania

themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
965
3,277
DRC Congo ni nchi tajiri sana, inawezekana kwa Africa nzima hakuna nchi inayoipata kwa utajiri hasa kwenye sekta ya madini. Basi Congo hawakamatiki, ile Ardhi yao imejaa pesa lakini kwa bahati mbaya wazungu walikuja wakawamwagia silaha mwisho wa siku yakaibuka matabaka.

Zikaanza kuzuka vita za wenyewe kwa wenyewe na lengo kuu ni kuwafanya wapigane ile upatikane mwanya wa kuiba madini, ambayo wanayachota watakavyo huku wakitumia miamvuli ya vikundi vya waasi.

Hili jambo limewafanya asilimia kubwa ya wacongo kuwa maskini wa kutupa tofauti na namna ambavyo walitakiwa wawe. Yaani Congo ilitakiwa iwe kama Qatar vile, watu wa pale walitakiwa wawe na utajiri wa kutisha. Watu wa congo walitakiwa muda wawe na maisha mazuri kulingana na maliasili walizonazo. Unaambiwa vifaa vya electronics dunia nzima kama simu na laptop, madini yanayotumika kutengeneza asilimia kubwa yanatoka Congo.

Ukitaka kuijua Congo kuwa ni sehemu ya fursa kwa Tanzania basi nenda pale Kariakoo kawaulize wafanyabiashara wa pale namna Lubumbashi inavyowatajirisha baadhi yao. Ila kama Congo nzima ingekuwa na amani na wananchi wa pale wangekuwa na pesa na wana maisha mazuri basi asilimia kubwa ya bidhaa zao wangekuwa wanaagiza Tanzania, maana ndiyo sehemu kubwa au chimbo lao ka kuagiza chakula na bidhaa za umeme hadi mavazi. Asilimia kubwa chimbo lao ni Tanzania.

Sasa kitendo cha Wacongo kuwa masikini moja kwa moja kinatuathiri hadi sisi huku, yaani kama Congo ingekuwa na amani kama Qatar basi wale wangekuwa matajiri sana na huenda kuna vijana karibu milioni kadhaa wa Tanzania wangekuwa wamejichimbia huko kutafuta fursa na hapa Tanzania biashara ingechangamka kupindukia. Ila kitendo cha ile nchi kutawaliwa na vita, kumeifanya fursa nyingi sana kupotea, na yale madini wanayoiba wazungu huenda yangekuwa yananunuliwa kihalali basi ile pesa ingewanufaisha Wacongo na wao wangetunufaisha sisi.

Kwa kifupi wazungu huwa hawataki kabisa kuona sehemu yenye utajiri wa madini, gesi na mafuta kwa Africa panakuwa na amani. Angalia kule Libya, Nigeria, Msumbiji, Congo namna yalivyoibuka makundi ya ajabu ajabu.

Angalia Uganda baada ya uvumbuzi wa mafuta yao kitendo cha harakati za kuanza tu kupitisha bomba la mafuta, angalia nchi za Ulaya walivyochachamaa kupinga wakati kwao huko mabomba yamejaa. Utajua tu hawa hawapendi kabisa maendeleo yetu.
 
DRC Congo ni nchi Tajiri sana inawezekana kwa Africa nzima hakuna nchi inayoipata kwa utajiri hasa kwenye sekta ya madini basi Congo hawakamatiki, ile Ardhi yao imejaa pesa lakini kwa Bahati mbaya wazungu walikuja wakawamwagia silaha mwisho wa siku yakaibuka mtabaka zikaanza kuzuka vita za wenyewe kwa wenyewe na lengo kuu ni kuwafanya wapigane ile upatikane mwanya wa kuiba madini ambayo wanayachota watakavyo huku wakitumia miamvuli ya vikundi vya waasi

Hili jambo limewafanya asilimia kubwa ya wacongo kuwa maskini wa kutupa tofauti na namna ambavyo walitakiwa wawe, yaani Congo ilitakiwa iwe kama Qatar vile, watu wa pale walitakiwa iwe na utajiri wa kutisha , watu wa congo walishatakiwa mda wawe Na maisha mazuri kulingana na maliasili walizonazo, unaambiwa vifaa vya electronics dunia nzima kama simu na laptop madini yanayotumika kutengeneza aslimia kubwa yanatoka Congo

Ukitaka kuijua Congo kuwa ni sehemu ya Fursa kwa Tanzania basi nenda pale Kariakoo kawaulize wafanyabiashara wa pale namna Lubumbashi inavyowatajirisha baadhi yao , Ila kama Congo nzima ingekuwa na amani na wananchi wa pale wangekuwa na pesa na wana maisha mazuri basi asilimia kubwa ya bidhaa zao wangekuwa wanaagiza Tanzania maana ndio sehem kubwa au chimbo lao ka kuagiza Chakula na bidhaa za umeme hadi mavazi asilimia kubwa chimbo lao ni Tanzania

Sasa kitendo cha Wacongo kuwa maskini moja kwa moja kinatuathiri hadi sisi huku, yaani kama Congo ingekuwa na amani kama Qatar basi wale wangekuwa matajiri sana na huenda kuna vijana karibu milioni kadhaa wa Tz wangekuwa wamejichimbia huko kutafuta fursa na hapa Tza biashara ingechangamka kupindukia, ila kitendo cha ile Nchi kutawaliwa na vita , kumeifanya fursa nyingi sana kupotea na yale madini wanayoiba wazungu huenda yangekuwa yananunuliwa kihalali basi ile pesa ingewanufaisha Wacongo na wao wangetunufaisha sisi

Inshort wazungu huwa hawataki kabisa kuona sehem yenye utajiri wa madini,gesi na mafuta kwa Africa panakuwa na amani, Angalia kule Libya,Nigeria,Msumbiji,Congo namna yalivyoibuka makundi ya ajabu ajabu

Angalia Uganda baada ya uvumbuzi wa mafuta yao kitendo cha harakati za kuanza tu kupitisha bomba la mafuta angalia nchi za ulaya walivyochachamaa kupinga wakati kwao huko mabomba yamejaa, utajua tu hawa hawapendi kabisa maendeleo yetu
...Mbona Hujazungimzia Kisiwa chetu Cha Amani, pamoja na kuwa na Dhahabu, Almasi, Tanzanite, Gesi...Badu hatujashikiana Bunduki????
 
Mnaweza kuwa na amani ila mkawa wajinga kupitiliza.

Tanzania ni nchi ya amani ila ni wajinga kupitiliza, kila aina ya rasilimali ipo ila inanufaisha wazungu na watu wa nje. Gesi ipo wapi? Madini ya kila aina yapo wapi? Kilimo kimelala, ufugaji ni kama tunalazimisha. Watanzani ni vibaraka na wanaofanya kazi za hovyo.

Isitoshe, tanzania inamilikiwa na wazungu na wahindi, hizo fursa za Congo watazichangamkia wao. Watanzania watabaki na shughuli zao za kila siku kama bodaboda, mama ntilie n.k.
 
Back
Top Bottom