Kukosea hakumaanishi kutokufaa, kukubali hujenga nguvu mara mbili

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,429
1574087874331.png
Moja ya mambo yanayofikirisha ni pamoja na utaratibu wa wadau za siasa nchini kutokukubali kwamba wamekosea hata pale wanapofanya makosa ya wazi sana. Sikumbuki kama kuna chama au kiongozi wa chama ambaye ashawahi kujitokeza hadharani hata siku moja akakiri kukubali kukosea kwenye jambo lolote lile na kukubali kurekebisha kitu.

Inavyoonekana ni kwamba, kuna imani kwamba mtu akikubali kukosea; maana yake hafai, ndio maana hata kama kuna makosa ambayo ni ya wazi kabisa, kwa kawaida hakuna anayekubali.Hata hivyo haifahamiki vyema chanzo cha Imani hiyo ni nini hasa.

Jambo ambalo pengine hatulifahamu ni kuwa, unapokosea na makosa yakawa yako wazi sana, kisha ukakubali na ukaonesha nia ya kubadilika, unajenga imani kubwa sana kwa umma na hivyo kupata nguvu mara mbili lakini unapofanya makosa ya wazi halafu ukawa unakataa, jamii inapoteza imani na wewe kiasi kwamba hata ukifanya kwa usahihi sasa ni vigumu kuaminika.Moja ya vitu vyenye nguvu sana katika siasa ni Imani, pengine ndio nguvu muhimu kuliko zote.

Tunaweza kushauri kuwa ni vyema tukajenga utamaduni kwamba pale ambapo inatokea mmoja wetu kufanya makosa ambayo yako wazi sana; basi ni vyema kukubali na pengine hata kuomba radhi na kisha kurekebisha. Watanzania wako 'fair' sana wala hakuna mtu mwenye shida na mtu eti tu kisa kakubali kosa ambalo kimsingi kalifanya. Kukubali kukosea na kujisahihisha hakumaanishi kwamba mkoseaji hafai na wala si jambo la aibu bali ni sehemu ya kawaida ya maisha na faida yake ni kubwa kuliko kinyume chake kwa sababu hujenga kuaminiana.
 
Kuwa specific,nani amekosea nini. Ujumbe huu kuwekwa humu means unataka ujumbe uwafikie wahusika na sisi wengine tujifunze. Ukiandika hivyo tutachukulia unaongea pekeyako
 
Mbowe alikosea sana kumfukuza kama mbwa Dr..Slaa na kumkaribisha Lowasa, lakini mpaka leo hajakiri kosa
 
"He who has never failed has learned nothing and has no tale to tell"....kosea tu mkuu wee kosea hasa!! ndo kujifunza huko ila siasa siyo halisi.
 
Back
Top Bottom