Kukosa Uhalisia kwa Taarifa ya Clouds ni Sababu ya Kupuuzwa Kwake.

Msororo69

JF-Expert Member
Feb 27, 2016
2,726
985
Naanza kwa swali. Je clouds ilivamiwa na mkuu wa mkoa? Kwangu nasema hapana. Kwa mujibu cctv inayorushwa hakioneshi kitendo chochote cha uvamizi wakati wa kuingia waala wakati wa kutoka. Maana si lazima mara zote uvamizi hufanyika wakati wa kuingia tu. Kwanini hawaakutuonesha cctv wakati Makonda na askari wakitoka? Huenda clip hiyo inaonesha namna wahusika wakiagana kwa bashasha na uelewano mkubwa kwa kusindikizana hivyo kuvunja dhana yao ya uvamizi.
Kosa ambalo ni halisi kwa muonekano ni la kuingia kwa jinai ambalo ni rahisi kwa Makonda kujitetea kwa mujibu wa maelezo ya Ruge. Ushauri wangu ni kuwa wakweli kwa kusema kitu halisi.
Nategemea kamati ya Mh Nape itakuja na jawabu la nani mwanzilishi wa hiyo stori. Je ni Makonda ndiye aliyemleta huyo dada kwa waatumishi wa clouds? Au watumishi hao baada ya kuiona stori ilivyo inaweza kumfurahisha Mh Makonda wakaamua kumtia tamaa ya kuhakikisha inarushwa? Kwa kauli ya Ruge mpaka saa tano usiku Mh Makonda hakuwa na hiyo clip ya shilawadu. Huu ni uthibitisho tosha kuwa Makonda hausiki kumtafuta huyo dada.
Kitendo cha kuchukuwa video hiyo kwenye flash ni kiini cha kutokuelewana. Je ilichukuliwa kwa nguvu? Kama ndio. Mh Makonda alijuaje imehifadhiwa kwenye foda gani na koompyuta ipi? Kushindwa kupewa hali halisi ya kilichoendelea wakati akiingia studio, kinafanya umma unaofikiria sawasawa kuamini kuwa waendesha kipindi waalimpa Mh Makonda kwa maelewano yao ya kirafiki au kibiashara.
 
IMG_20170321_210249.jpg
 
Yaani kuna kuna watu ni mabogaz kama hili hapa kichwa cha habari na post haviendani

Post unaeleza ushuzi tu
 
Yaani unaona umedadavuaaaaa!!!!!! Pole!!! Hakuna haja ya mjadala! Tumeambiwa mhusika alikuwa "anachapa kazi"!!!
 
Yaani kuna kuna watu ni mabogaz kama hili hapa kichwa cha habari na post haviendani

Post unaeleza ushuzi tu
Huyo ndo Masogange sasa, kama ulikuwa hujamstukia. Lazima amtetee bwanaake...
 
we umenunua simu leo?hukuona wanatoka na min dv acha kukurupuka
 
Kuvamia sehemu si lazima uwe na mtutu wa bunduki ndio umevamia Bali inawezekena ukawa umeingia mahali bila taarifa na kuvuruga shughuli au utaratibu wa shughuli zilizokuwa zikiendelea.
 
Umesema kweli tupu kwa picha za cctv, hakuna jinai hapo, hivi walitaka makonda atembee usiku bila ulinzi? Watafute single ingine ya kutokea.
 
Back
Top Bottom