Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Bwana Mchanga alipata nafasi ya kwenda masomoni nchi za Scandinavia, alibahatika kupata mke wa Kizungu na baraka ya mabinti watatu. Baada ya masomo Mrs Mchanga alikataa kurudi Tanzania. Waliachana kwa amani na bwana Mchanga kurejea nyumbani.
Alipata ajira serikalini kama afisa mwandamizi. Alikutana na Ruth na wakafunga ndoa. Ruth alipata mtoto wa kike, Mchanga alikua mvumilivu, wapili akaja binti mrembo. Hapa Bwana Mchanga uvumilivu ulimwishia. Alikwenda kijijini kwao na kuoa kabinti kigori kabisa. Kwakua uwezo wa fedha alikua nao alimjengea nyumba nzuri pale kijijini.
Huku kwa Ruth alimuacha akiwa mja mzito na alijaliwa kupata mtoto wa kiume. Ruth hakua na habari kuwa mume wake ana mke kijijini. Kila weekend Mchanga alikwenda kijijini akidai anajiandaa kugombea Ubunge. Ruth slipata habari mume wake ana mke mwingine yeye akiwa na mtoto wa pili wa kiume.
Huyu mke wa kijijini alianzisha leagu na Ruth, Ruth akiwa career woman hakuwa na muda huo, aliachana na Mchanga na kugaiwa mali zake. Maisha yanaendelea na watoto wakakua.
Mchanga alianza familia mpya kijijini. Umri nao unasogea. Sasa Mchanga anastaafu akiwa na watoto wanasoma shule ya msingi. Wale mabinti wa Scandinavia wameolewa na wameanza familia.
Katika jitihada za kutafuta mtoto wa kiume sasa Mchanga anatumia mafao ya kustaafu kulea watoto.