Kukoroma usingizini: Fahamu chanzo na tiba yake

Du mie nilienda ugenini kuna binti alikuwa akikoroma yaani ni bora utangulie weye kusinzia lakini akitangulia yeye wewe ndo utahesabu mabati mpaka morning

lakini wewe ama siku hizi umenenepa na kupata kitambi ..kama zamani ulikuwa hukoromi iweje sasa ??
 
1stlady1 best nimenenepa mno yaani mpaka jamaa hatuongozani tena njiani:(
 
Nina Maradhi ya Kukoroma wakati wa kulala na naona nimerithi kutoka kwa Marehemu Baba yangu yeye ndie aliyekuwa anakoroma sana wakati wa kulala je kama kuna mtu anayejuwa Dawa ya kutibu hayo Maradhi ya Kukoroma anisaidie jamani nikiwa na mke wangu huwa ananilalamikia sana wakati wa usiku kuwa nakoroma sana naombeni Dawa jamani ili matatizo yangu yaishe Asanteni.
 
Kukoroma sio maradhi, ni hulka tuu, wakoromaji huwa wanalala kifudifudi na mdomo kufunguka usingizini, lla kiubavu ubavu au lala tumbo.

Kukoroma ambako ni maradhi ni pale mtu anapokuwa na sinus puani, hivyo akilala zinaziba njia ya hewa inabidi mdomo ufungunge, dawa yake ni oparation ndogo kuziondoa hizo growth kwenye njia ya hewa, kukoroma kwisha.
 
kukoroma sio maradhi, ni hulka tuu, wakoromaji huwa wanalala kifudifudi na mdomo kufunguka usingizini, lla kiubavu ubavu au lala tumbo

This is totally misleading, kitu kama hujui kaa kimya mzee! Kuna watu wanakoroma hata kiwa amejiegesha kwenye kiti na kupitiwa na usingizi.

Kukoroma ambako ni maradhi ni pale mtu anapokuwa na sinus puani, hivyo akilala zinaziba njia ya hewa inabidi mdomo ufungunge, dawa yake ni oparation ndogo kuziondoa hizo growth kwenye njia ya hewa, kukoroma kwisha

This nonsensical again!

Ufumbuzi wa hili tatizo ni kujua nini chanzo cha kukoroma!Watu wengi wanene hukoroma huku husababishwa na mafuta ya ziada yaliyo kwenye shingo.

Uvutaji wa sigara kupita kiasi huchangia tatizo la kukoroma, Ulevi kupindukia, kuchoka kupita kiasi,

Kuna watu wenye matatizo na ufunguaji wa vinywa hii husababisha wapate shida na kupumua na kupelekea kukoroma.

Matatizo kwenye ulimi (toungue base) hasa kwenye koo na ulimi hawa hukoroma kupita kiasi

Watu wenye umri mkubwa hukoroma pia.

Hizo nisababu za kusababisha kukoroma, kupunguza hili tatizo kuna njia nyingi, moja wapo ni hiyo aliyoitaja MziziMkavu, kufanya mazoezi ya ulimi.

Njia nyepesi ni kufanya mazoezi kupunguza unene na excess fat kwenye ulimi, kuacha sigara na ulevi kupindukia. ingawa sababu zingine zinataka operation kwenye shingo na mfumo wa njia za hewa. Pia

  • Sleep on your side - changing sleeping posture
  • Elevate the head of your bed
  • Limit alcohol and medications
  • Clear your nasal passages - SURGICAL OPERATION ama kuna gargets za kuvaa puani kulingana na tatizo chanzo chake
  • Lose weight - Mazoezi kuondoa floopy tissues around the neck
Kuna wengine tatizo hili halina suluhisho hasa kama nilakurithi, ama magonjwa kama Allergies, asthma, a cold, or chronic sinus infections

Masa
 
Wakuu habari ya siku nyingi!!

Wakuu nina mdogo wangu yaani ana hilo tatizo hapo juu mpaka natamani kutengeneza bit za mziki kwani akiweka kichwa tu kitandani hapohapo anaanza na base yaani hata ukimshitua anatulia mara anarudia tena.

Wakuu naomba kama kuna mtu yeyote anayejua dawa la hii tatizo anijuze nimsaidie ndugu yangu asije kimbiwa na mchuchu wake kwa makelele hayo.
 
Watanzania nimeletewa dada wa kukaa na familia
akiwa kama mmoja wa wanafamilia na anaemkea mtoto wangu na mi pia
nimeona vyema nikapambana nae kumsaidia hili swala la kokroma usiku ni shida tupu kama jiran wangeuwa karibu sidhan ambae angelala
dawa yake ni nini...ahsanten kw a ushauri mtakaoutoa...
 
1.Ana miaka mingapi huyo dada,?
2.Unamuonaje kiafya?Hana kikohozi au mafua ya mara kwa mara
3.Je anayo tabia ya kupenga au kuvuta makamasi kwa ndani mara kwa mara?
Alishawahi kupata medical attension before,kama ndio waligundua nini na alitibiwaje?
MWANGALIE VIZURI HALAFU LETA HABARI,UTAKUWA UMENIPATIA CLUE THAT WILL POINT US TORWARDS A SOLUTION.
 
SABABU KWA UJUMLA

1.Physiologica; inaweza kuwa kawaida kama hakuambatani na maradhi au pindi hamna malalamiko toka kwa wenzi unao ishi nao,kama wenzio wana malalamiko ambayo yatageuka kuwa kero kwako binafsi,basi tayari huo ni ugonjwa na una matibabu yake.
2. Pathological process; mara nyingi ni matokeo ya ugonjwa/magonjwa ambayo hupelekea tendo la kukoroma,nayo hutofautiana kufuatana na umri.Hata watu wazima kuna wengine utakuta walikuwa hawana historia ya kukoroma,lakini GHAFLA ukubwani wanakumbwa na ugonjwa huo.[mfano ni baadhi ya wagonjwa wa ukimwi,ingawa sio wote,na sio lazima kuwa kila mwenye hali hiyo basi awe ni mgonjwa wa ukimwi lakini huonekana kwa (some HIV and someof the CANCER PATIENTS)]

3.Congenital; Huanza kuonekana pale tu baada ya kuzaliwa,kisababisho kinaweza kuwa ni URITHI[ hereditary]kutoka kwa waliomtangulia au kama sio urithi basi ni tokeo la hitilafu za kimuundo
zilizotokea kipindi cha uumbaji wa mtoto, wakati akiwa bado yupo tumboni mwa mama yake [fetal development]

4 Drug induced; Husababishwa na matumizi ya baadhi ya dawa,ambazo mbali na kutibu ugonjwa hutowa matokeo ambayo hayakutarajiwa medically known as adverse drug reactions [An unwanted effect caused by the administration of a drug] Hali hii huweza kutokea ghafla au taratibu.

5 Traumatic or corrosive injury; Ikitokea kwenye larynx au trachea huweza pia kusababisha.Unywaji wa sumu pindi watu wanapotaka kujiua ,sumu wavutayo wafanyakazi kwenye baadhi ya viwanda n.k. ambayo ina uwezo wa kusababisha kusinyaa kwa larynx au trachea[capable of causing their stenosis or narrowing]

6.Post thyroidectomy; Hutokea baada ya kufanyiwa opration ya kuondoaTezi THYROID.Sababu moja wapo ni kuumizwa,au kukatwa kwa recurrent laryngeal nerve wakati wa kuiodoa hiyo tezi[thyroid]


SABABU ZIPO NYINGI MNO NA NDIO MAANA NIKAANZIA NA SUALA LA UMRI KWANZA,..ILI TUWEZE KUTOA USHAURI WA WAPI PA KUANZIA..KAMA NITAZUNGUMZIA YOYE HAYO juu ,NA KUTOA USHAURI WA TIBA NADHANI NITAKUA SIJAJIBU SWALI,NA WALA SITAELEWEKA.
 
FOREIGN BODY;PIA nilitaka kusahau.,,.jamaa alikuwa ameoa,na waliishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili.Mama alilijua tatizo za mumewe na alilivumilia. kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo mama uvumilivu ilipozidi kumshinda,kwani aligundua kuwa mkoromo wa mumewe ni sawa na mtu anayepuliza filimbi sauti ambayo sio kawaida ukilinganisha na ya mikoromo mingine.
Hivyo akaamua kumrekodi bila kumpa taarifa.Baadaye wakiwa kwenye hali ya utulivu ndipo akampa taarifa na kumuwekea ile sauti.

jamaa kusikia hali ilivyo akakosa raha kabisa,.na kuamua kutafuta tiba ya tatizo.Alipokuja kwetu,tukaoda X-ray kwanza.Picha ya kifua mapaka usawa wa koo .Picha ilipotoka ilionekana kuwa na kimvuli cha duara juu ya shingo. Nilipoenda kuitoa ilikuwa ni shilingi yenye mwengei likuwa imegeuka rangi na kuwa ya kijani.

Jamaa alipoamka na kupatiwa hiyo shilingi yake ,ndipo kumbukumbu zikamjia kuwa alipokuwa mtoto aliweka shilingi mdomonina aliimeza bahati mbaya.

aliporipoti tukio kwa wazazi wake,wakamwambia kuwa itatoka kwa njia ya haja kubwa hivyo asiwe na wasi wasi. tangu siku aliyoumeza huo mwenge mpaka siku aliyoripoti tukio,hakuwahi kuwa na matatizo ya ziada,si kwenye kifua wala kupumua.
Shilingi ilitolewa miaka 25 baada ya kuimeza,na tangu ilipotolewa ndio ikawa mwisho wake wa kukoroma.
 
MBONA MKALI HIVYO,NADHANI NIMEJARIBU KUTENGEZA INITIAL CLUE TORWADS A SOLUTION,KUFUATANA NA JINSI SWALI LILIVYOULIZWA.WEWE UMESOMA BWANA,..NADHANI SIKU ZOTE HUWA UNAJIBU ULICHOULIZWA.

SABABU KWA UJUMLA

1.Physiologica;inaweza kuwa kawaida kama hakuambatani na maradhi au pindi hamna malalamiko toka kwa wenzi unao ishi nao,kama wenzio wana malalamiko ambayo yatageuka kuwa kero kwako binafsi,basi tayari huo ni ugonjwa na una matibabu yake.
2. Pathological process; mara nyingi ni matokeo ya ugonjwa/magonjwa ambayo hupelekea tendo la kukoroma,nayo hutofautiana kufuatana na umri.Hata watu wazima kuna wengine utakuta walikuwa hawana historia ya kukoroma,lakini GHAFLA ukubwani wanakumbwa na ugonjwa huo.[mfano ni baadhi ya wagonjwa wa ukimwi,ingawa sio wote,na sio lazima kuwa kila mwenye hali hiyo basi awe ni mgonjwa wa ukimwi lakini huonekana kwa (some HIV and someof the CANCER PATIENTS)]

3.Congenital;Huanza kuonekana pale tu baada ya kuzaliwa,kisababisho kinaweza kuwa ni URITHI[ hereditary]kutoka kwa waliomtangulia au kama sio urithi basi ni tokeo la hitilafu za kimuundo
zilizotokea kipindi cha uumbaji wa mtoto, wakati akiwa bado yupo tumboni mwa mama yake [fetal development]

4 Drug induced;Husababishwa na matumizi ya baadhi ya dawa,ambazo mbali na kutibu ugonjwa hutowa matokeo ambayo hayakutarajiwa medically known as adverse drug reactions [An unwanted effect caused by the administration of a drug] Hali hii huweza kutokea ghafla au taratibu.

5 Traumatic or corrosive injury;Ikitokea kwenye larynx au trachea huweza pia kusababisha.Unywaji wa sumu pindi watu wanapotaka kujiua ,sumu wavutayo wafanyakazi kwenye baadhi ya viwanda n.k. ambayo ina uwezo wa kusababisha kusinyaa kwa larynx au trachea[capable of causing their stenosis or narrowing]

6. Post thyroidectomy ;Hutokea baada ya kufanyiwa opration ya kuondoaTezi THYROID.Sababu moja wapo ni kuumizwa,au kukatwa kwa recurrent laryngeal nerve wakati wa kuiodoa hiyo tezi[thyroid]


SABABU ZIPO NYINGI MNO NA NDIO MAANA NIKAANZIA NA SUALA LA UMRI KWANZA,..ILI TUWEZE KUTOA USHAURI WA WAPI PA KUANZIA..KAMA NITAZUNGUMZIA YOYE HAYO juu ,NA KUTOA USHAURI WA TIBA NADHANI NITAKUA SIJAJIBU SWALI,NA WALA SITAELEWEKA.
Ahahhhhhhaaah sio ukali mkuu, si unaelewa mgonjwa au mtu anaeuguza anavyokuwa mkali pale anapocheleweshewa tiba mbele ya daktari!
By the way nashukuru sana kwa maelezo yako nimepata somo!
 
Wana JF
Naombeni msaada wenu ili nijue sababu inayomfanya mtu akorome na kama kuna dawa please nisaidieni maana sielewi sababu, nilienda katika ofisi moja, huwezi kuamini kuna mtu anakoroma vibaya mno hata kama amekaa! yaani akisinzia tu ni kosa, popote pale anakoroma mno. Baba yangu pia anakoroma sana hadi watu wanasikia nje!

Hivi ni nini kinasababisha mtu akorome?
Na, je, kuna dawa ya kuacha kukoroma?

Naombeni msaada wenu tafadhali niwasaidie na wengine
 
Kinacho sababisha ni kupumua, kama unaweza kuwa ziba njia ya hewa fanya hivyo wataacha kukoroma.
 
Kinacho sababisha ni kupumua, kama unaweza kuwa ziba njia ya hewa fanya hivyo wataacha kukoroma.


Kama hujui hivi ni lazima uchangie?, mimi niko serious, we unaleta utani, siyo sehemu ya jokes hii, naomba uwe serious please, au na wewe unakoroma? Subiri watu watusaidie!
 
kuna sababu 3 za haraka haraka
1 kulala vibaya, kwa maana ya kuzuia hewa kupita smoothly kwenye koo. mito (pillows) zinaweza kusababisha hii kama haziko laini kiasi cha kuruhusu shingo ikae mkao ulio comofrtable.
2 kuwa na nyama ambazo zinazuia koromeo kuwa wazi kiasi cha kutosha (mfano goita, mafindofindo/tonsills) ama nyama ambazo zinakuwa kwenye pua
3 uzito mkubwa wa mwili, ambapo moyo unakuwa na kazi ya ziada ku-support system nzima (sijafuatilia physiology yake hii)
kama kunakuwa na mkoromo wa kukera, nadhani ni vizuri kuonana na daktari kujihakikishia kuwa hakuna tatizo la kiafya
 
  • Thanks
Reactions: LAT

Similar Discussions

Back
Top Bottom