Kukomesha nunua nunua tufanye hivi

kipara anahonga kodi zetu..
tupaze sauti risasi kaundiwa binaadamu..
Bila aibu yule fisadi mwenzake, Mnyeti anatangaza wazi eti bado wanazo kodi za kutosha kwa ajili ya kuhongea..
halafu fisadi kama hilo eti unalipandisha wadhifa..
 
Ukifanya hivyo basi itakuwa ndio umehalalisha "ununuzi" na "manunuzi".

Nasisitiza tusitafute short-cuts kwenye matatizo haya, Vyama vya Upinzani vijtathmini na kujijenga upya kuanzia CHINI kwenda juu, vijenge vijana na kuandaa viongozi ili kuondoa nunuliwa-nunuliwa na makando kando kama hayo.

Kwa sababu historia inayonyesha kuwa hata miongoni mwa Wabunge walioko Upinzani sasa hivi na wanaodhaniwa ni dam-dam kuna waliowahi kununuliwa na/au wengine kushiriki michezo michafu huko nyuma.

CCM ni chama na taasisi yenye mfumo na uwezo wa kutumia kila mbinu na silaha iwe safi au ovu kwa kiwango ambacho Upinzani hawawezi kukabiliana nao mpaka pale tu watakapokuwa na watu (viongozi, wanachama) thabiti, walioandaliwa na walio committed. Kwa sasa hakuna njia maana Upinzani uko kwenye tanuru la aidha kufa au kupona.
 
Mimi nana shauri kuliko kupoteza fedha nyingi kurudia uchaguzi kwa hawa wanaojiuzulu au kwasababu yeyote mnaonaje tuanzishe Campaign ya mabadiliko ya katiba kuwa jimbo au kata iliyowazi ,hakuna uchaguzi isipokuwa mshindi wake wa pili ndio aijaze nafasi hiyo.

Mnaonaje ndugu?

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
Imekaa vizuri.Na ikitokea kifo,chama chenye mbunge kiteue mrithi ambaye alikuwa mshindi wa pili kwenye kura za maoni za chama chao.
 
Fanyeni haraki tuzione sio kudai mkiwa chumbani boss
Mbona unaongelea chumbani, ndio nini? Au jf imekuwa chumba, maana sikuekewi kabisa. Wewe fanya yako, haya tuachie sisi ambao tunajua kufa ni sehemu ya maisha.
 
Mimi nana shauri kuliko kupoteza fedha nyingi kurudia uchaguzi kwa hawa wanaojiuzulu au kwasababu yeyote mnaonaje tuanzishe Campaign ya mabadiliko ya katiba kuwa jimbo au kata iliyowazi ,hakuna uchaguzi isipokuwa mshindi wake wa pili ndio aijaze nafasi hiyo.

Mnaonaje ndugu?

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app

Wazo langu iwapo mbunge/diwani anajiuzulu basi nafasi hiyo ijazwe na chama chake kwa kufanya uchaguzi wa ndani.
 
Labda kama mnadai chumbani otherwise mtakufa kifo cha ajabu
Kwa vyovyote vile utakuja kufa hata kama waogopa kifo. Pili hakuna ajuae aina ya kifo alichopangiwa. Chaweza kuwa cha ajabu huna uwezo wa kujipangia.
 
Mimi nana shauri kuliko kupoteza fedha nyingi kurudia uchaguzi kwa hawa wanaojiuzulu au kwasababu yeyote mnaonaje tuanzishe Campaign ya mabadiliko ya katiba kuwa jimbo au kata iliyowazi ,hakuna uchaguzi isipokuwa mshindi wake wa pili ndio aijaze nafasi hiyo.

Mnaonaje ndugu?

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
Umesahau jambo kndugu. Ikiwa hivyo itakuwa ni hatari sana kwa wale wabunge waliochaguliwa. Ni rahisi kufanyiwa figisufigisu na mshindi wa pili, ikiwezekana hata kumpoteza ili nafasi ibaki wazi na yeye achukue. Hebu ifikirie vizuri hii hoja yako ndugu
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom