Kukomesha malaria, dengue ni kuzuia mbu kuzaana

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,025
2,000
pampu.JPG

Katika kupambanana maradhi ya malaria, hapo miaka ya nyuma, msisitizo ulikuwa zaidi katika kuzuia maradhi kuliko kuponya. Hivyo basi kulikuwa na jitihada kubwa ya kuangamiza mbu pamoja na mazalia yake. Tuliona wakati ule, watumishi wa jiji, manispaa au miji wakipita mitaani na pampu zao migongoni wakinynyuzia dawa sehemu zile ambazo zilikuwa ni vyanzo vya mbu.

Majumbani pia, wakati wa jioni au usiku, familia nyingi zilikuwa zinapuliza dawa ya kuulia mbu kwa kutumia pampu za mikono. Vitendo hivi vilikwenda sambamba na elimu ambayo ilikuwa inatolewa katika jamii, hususani mashuleni, redioni na kwenye mabango, jinsi ya kuweka mazingira katika hali ambayo mbu hawakuweza kuzaliana. Naweza kusema kwamba, kampeni zote hizi ambazo zilikuwa zinafanywa na serikali ya wakati ule, zilikuwa na mafanikio makubwa, kwani hapakuwa na milipuko mikubwa ya maradhi ya malaria n.k.

Kwa bahati mbaya sana, mpaka sasa sijaona juhudi zozote ambazo serikali hii inafanya katika kuzuia milipuko ya maradhi ya hatari kama malaria, na hivi sasa huu mlipuko wa dengue.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom