Kukojoa kwenye chupa yenye mfuniko, halafu kila saa inafungwa mfuniko, kuna athari yoyote?

kufanakupona

JF-Expert Member
Jun 18, 2015
522
417
Nyakati za usiku, wengine ni uvivu kuinuka kwenda chooni kujisaidia haja ndogo, baadala yake wanatumia kopo, ndoo au chupa kujisaidia haja ndogo.
Swali langu lipo kwenye hawa wanaotumia chupa yenye mfuniko, yaani akishamaliza kukojoa, anaifunga kwa mfuniko.
Maswali:
(1) Lile joto kali linalokuwa kwenye chupa linalosababishwa na kufunga chupa kwa mfuniko kwa muda mrefu halina athari kwenye uume?
(2) Ukitumia chupa au kopo kwa muda mrefu, kwenye kopo au chupa kunabaki vitu kama magadi, yale magadi ni nini?
Asanteni.
 
Kuhusu swali la kwanza...

Huwa wanaingiza kabisa uume kwenye chupa? Nilidhani wanalenga shabaha tu.

Mkojo una salts nyingi. Hayo magadi itakuwa residual ya hizo salts baada ya kukauka kwa solvent.
 
Kuhusu swali la kwanza...

Huwa wanaingiza kabisa uume kwenye chupa? Nilidhani wanalenga shabaha tu.

Mkojo una salts nyingi. Hayo magadi itakuwa residual ya hizo salts baada ya kukauka kwa solvent.
Ukilenga shabaha unalowanisha godoro Mkuu, mwishowe sehemu ya kulala inakuwa kero kwa unyevunyevu, wanaingiza kabisa Mkuu.
 
Kama mnashare sio vizuri kama kuna contact unaweza kupata Urine Transmitted Infections kwasababu normaly mkojo uko 'sertile' unapotoka kwenye kibofu lakini baada ya kuwa exposed una attracts microbes na hivyo unakua na bacteria waoweza kusababisha magonjwa.

Ni vizuri ukatumia choo safi ili kulinda afya yako
 
Wanaume wa Dar wakipeana trick za kupata haja pasi'nakushuka vitandani mwao....wazee mnaniangusha sana,hivi mwanaume unashindwa nini kuachia kitanda na kutoka nje kwenda kujisaidia hadi ukojoe kwenye makopo?tena bila hata kusimama kushusha miguu chini?ikiwa mwanaume utakojoa kwenye chupa tena ndani ya neti mkeo atafanyaje,si atajikojolea kitandani kabisa?

Ila nahisi huu ni utani!
 
Kama mnashare sio vizuri kama kuna contact unaweza kupata Urine Transmitted Infections kwasababu normaly mkojo uko 'sertile' unapotoka kwenye kibofu lakini baada ya kuwa exposed una attracts microbes na hivyo unakua na bacteria waoweza kusababisha magonjwa.

Ni vizuri ukatumia choo safi ili kulinda afya yako
sertile = sterile
 
Duh wanaume wa dar uwe unaomba watu wakusindikize si vzr kiafya tena unatumbukiza kwenye chupa yenye hewa nzito
 
Mwanaume unakuwa na kopo la kukojolea ndani ina maana unaogopa nini kutoka usiku!?.
Siyo woga, ni uvivu unaosababishwa na usingizi wa uchovu wa pilikapilika za kazi ngumu za mchana kutwa.
 
Wanaume wa Dar wakipeana trick za kupata haja pasi'nakushuka vitandani mwao....wazee mnaniangusha sana,hivi mwanaume unashindwa nini kuachia kitanda na kutoka nje kwenda kujisaidia hadi ukojoe kwenye makopo?tena bila hata kusimama kushusha miguu chini?ikiwa mwanaume utakojoa kwenye chupa tena ndani ya neti mkeo atafanyaje,si atajikojolea kitandani kabisa?ila nahisi huu ni utani!
Wanaoogopa kutoka wengi ni wale wa Dar, madhara kwenye mfumo wa mkojo ni lazima mkuu
Mimi ni wa mkoani wakuu, sina hata chembe ya woga. Ninavyokojoa kwenye chupa siyo woga, ni uvivu unaosababishwa na shughuli nyingi za mchana kutwa.
Halafu mwanaume kukojolea kwenye kopo siyo ajabu, hiyo desturi ipo tangu enzi na enzi.
Kwa hiyo msiotumia makopo kujisaidia msione kitu cha kigoigoi.
 
Duh wanaume wa dar uwe unaomba watu wakusindikize si vzr kiafya tena unatumbukiza kwenye chupa yenye hewa nzito
Acha kebehi Mkuu, kukojoa kwenye chupa ni jambo la kawaida, siyo kwa mwanamke wala kwa mwanaume. Inavyoelekea akili yako muda wote inawaza kihasihasi tu.
Hayo madhara kiafya ni yapi na yapi?
 
Marehemu Mama yangu alituzoesha hivyo kuna maeneo hatari sana huwezi kutoka usiku
Ni bora utaratibu huu
Wenzetu wenye Masterbedroon In sha Allah msituseme sie makapuku
 
Mimi ni wa mkoani wakuu, sina hata chembe ya woga. Ninavyokojoa kwenye chupa siyo woga, ni uvivu unaosababishwa na shughuli nyingi za mchana kutwa.
Halafu mwanaume kukojolea kwenye kopo siyo ajabu, hiyo desturi ipo tangu enzi na enzi.
Kwa hiyo msiotumia makopo kujisaidia msione kitu cha kigoigoi.
Ni ajabu kukojolea kwenye makopo mwanaume!..Ni kama dalili ya Uoga hivi, choo hata kama kipo nje ya nyumba sitaki amini kipo mita 100 toka unapoishi labda kama ni kijijini.
Halafu kuna baadhi ya desturi zilifanyika miaka hiyo kutokana na mazingira sasa mtu msomi wa JF unalojoa kwenye kopo ukisema kawaida!!..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom