Kukodisha Airbus ni mkataba wa kipuuzi - Mwakyembe

Mkuu Bitabo,binafsi sifahamiani na Paul Chizi,lakini nadhani badala ya Mwakyembe kumfuta kazi angesimamia mchakato huru na haki kulifufua shirika letu la ndege. Kama kawaida ya Mwakyembe na wenzake ametumia taratibu kumwondoa mtu ambaye mimi naamini alikua anafanya kazi kizalendo na analipenda shirika! Walioua ATCL ni wanasiasa na watendaji serikalini. Inaumu sana kwetu sisi ambao tumetumia huduma za shirika ili toka tukiwa watoto wadogo!
Wakuu Mh. Mwakyembe hakupindisha maneno juu ya uovu wa Mr. Chizi na wenzie. sasa hizo uniform za staff za dola za obama 50,000 kwa wafanyakazi wangapi hapo ATCL? tena bila tendering process? Tumpe nafasi na kama ametupiga changa la macho soon tutajua tu maana hata huyo Chizi ameyasikia yaliyosemwa.

lakini Chizi alishastaafu kwa mujibu wa sheria na Mwakyembe anasema utaratibu wa kumuajiri mstaafu haukufatwa. hapo napo kuna ukabila?

Amesema mwenyekiti wa bodi mpya atatangazwa na JK soon, ngoj tuone hiyo bodi mpya na hao watakaoajiriwa kwenye menejiment mpya ndo tujue ukabila uko upande gani.

Issue hapa sio kupeleka ndege yenye picha ya twiga angani. Issue tunaipeleka kwa gharama gani na utaratibu upi?

Watu mnalalmikia picha ya twiga angani wakati watu wamepeleka twiga hai angani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Tanzania bwana utasikia ooh udini oooh ukabila huku watu wanaiba.
 
Huyu mzee wa Ukurutu nimekuwa simwamini tokea aseme kwenye ile ripoti yake ya Richimond kuna mambo ambayo ameficha ili serikali isianguke inamaana alitusaliti sisi wananchi. halafu turudi kwenye mada yeye ni mtaalamu wa mikataba ya kukodisha ndege?
Nawewe ni mnufaika wa ufisadi huu?
 
Huyu mzee wa Ukurutu nimekuwa simwamini tokea aseme kwenye ile ripoti yake ya Richimond kuna mambo ambayo ameficha ili serikali isianguke inamaana alitusaliti sisi wananchi. halafu turudi kwenye mada yeye ni mtaalamu wa mikataba ya kukodisha ndege?

Sasa nawe una ubongo wa aina gani sijui?
Duniani hapa kuna utaalamu wa mikataba ya kukodisha Ndege? Baadaye utasema;
Mikataba ya kukondisha treni
Mikataba ya kukondisha hoteli
Mikataba ya kukondisha kumbi za mikutano na ....

Wapi utafika? Soma upate elimu uitumie kila panapostahili.

Mwkyembe fanya kazi.
 
Nakubaliana na wewe,Mwakyembe ni mtu mnafiki na hatari ambaye kwa utaalamu mkubwa anajua kuchezea akili za watu wasiopenda kutumia ubongo kufikiria mara mbili. Lakini siku zote njia ya mwongo ni fupi. Alituingiza mkenge kuhusu kuvunja mkataba wa DOWANS,sasa ni kilio,na yeye na wenzie wako kimya. Kumbe uchungu wa kinafiki ilikua kumwondoa hasimu wao Lowassa!
Kitendo cha Mwakyembe kwenda redioni kuongelea mkataba wa kukodisha Airbus miaka mitano iliyopita ni unafiki uliopitiliza. Mi nilidhani ataongelea mapungufu ya sasa ya shirika na kueleza namna ya utatuzi wake. Nawashauri watanzania mlio wavivu wa kufuatilia mambo muwe makini sana na watu wa aina hii, wanacheza na public opinions kwa maslahi binafsi na cheap popularity. Kwanza akina Mataka si wana kesi mahakamani? Jamani shikeni maneno yangu huyu Mwakyembe ni msanii, makosa ya miaka mitano iliyopita hayahalalishi kumpa nafasi binamu yake kuongoza shirika
 
Kiukweli kwa jinsi Mzee Mwakyembe, Balozi Kagasheki na watendaji wanavyoanza kufunguka CDM waandae agenda nyingine haraka sana. Ama sivyo watajikuta wanaimba zilipendwa wakati wananchi wanageukia Zinapendwa!

Ingekuwa hivyo Marekani na Uingereza na nchi zingine ambazo zimepiga hatua kusingekuwa na Vyama Vya Upinzani!!
 
Nakubaliana na wewe,Mwakyembe ni mtu mnafiki na hatari ambaye kwa utaalamu mkubwa anajua kuchezea akili za watu wasiopenda kutumia ubongo kufikiria mara mbili. Lakini siku zote njia ya mwongo ni fupi. Alituingiza mkenge kuhusu kuvunja mkataba wa DOWANS,sasa ni kilio,na yeye na wenzie wako kimya. Kumbe uchungu wa kinafiki ilikua kumwondoa hasimu wao Lowassa!

Wakuu,mkuu Babito katia hoja pale..ni bora kuijibu ile hoja kuliko kuendelea kumpondonda mwakyembe kwa hoja ambazo hazina mashiko!!!hata kama ikiwa ni pesa kidogo ila kwa shirika la serikali kufanya manunuzi bila kufata sheria huo ni upuuzi!!!
 
Kwa uelewa wako hoja zangu hazina mashiko!
Wakuu,mkuu Babito katia hoja pale..ni bora kuijibu ile hoja kuliko kuendelea kumpondonda mwakyembe kwa hoja ambazo hazina mashiko!!!hata kama ikiwa ni pesa kidogo ila kwa shirika la serikali kufanya manunuzi bila kufata sheria huo ni upuuzi!!!
 
Huyu mzee wa Ukurutu nimekuwa simwamini tokea aseme kwenye ile ripoti yake ya Richimond kuna mambo ambayo ameficha ili serikali isianguke inamaana alitusaliti sisi wananchi. halafu turudi kwenye mada yeye ni mtaalamu wa mikataba ya kukodisha ndege?

Uwe na heshima ****** wewe
 
Huyu Chizi aliyewekwa pembeni anahusika vipi na mikataba ya Airbus?
 
Kiukweli kwa jinsi Mzee Mwakyembe, Balozi Kagasheki na watendaji wanavyoanza kufunguka CDM waandae agenda nyingine haraka sana. Ama sivyo watajikuta wanaimba zilipendwa wakati wananchi wanageukia Zinapendwa!
Nina wasiwasi sana na kiwango chako cha taaluma, ama kweli shule za kata ni balaa kubwa sana, kama wahitimu wake ndio wanaowaza kwa kiwango hiki!
 
Wasiwasi wangu ni speed anayoendeshea mwakyembe na ubovu wa bara bara zetu. Akipinduka hatoki mtu.
 
Nani? zomba? Au nani!!??
Hawa zomba type ni hovyo tu,
Kumlaumu Mwakembe hawawezi, kumsifia Chizi hawawezi, hovyo tu!!
Mkuu Bigirita, Zoba na kundi lake zaizi yao ni mihadhara ya uamsho ambako wanafikiri kwa mioyo na sio vichwa na ubongo.
 
Ni mkataba wa kipuuzi ambao haujawahi kutokea. alonga Mwakyembe .. Mpaka sasa hivi serikali inadaiwa 6.9 billion shillings..
ndege imekodiwa tumeanza kuilipia ikiwa angani hata kabla haijatua

Saint Ivuga
ktk nyekundu hapo hakumaanisha hivyo mkuu,alimaanisha HANGAR ikiwa na maana kuwa tulikuwa tukilipa pesa wakati ndege ikiwa ktk HANGAR kwa matengenezo
 
sasa kama chizi aliambiwa na mkuu wa magogoni huo mkataba yeye angefanyaje?kama mzee wa ukurutu anao huo ubavu basi amguse huyu kiongozi wa mafisadi a.k.a.mwanaasha kwa sababu ni lazima hapo kulikuwa na fungu lake

kuna harufu ya majungu hapa!!! mwache malafyale afanye kazi yake.
 
Hizi ndege naogopa hata kuzipanda coz hazikawii kuisha mafuta angani
 
Mkuu Bitabo,binafsi sifahamiani na Paul Chizi,lakini nadhani badala ya Mwakyembe kumfuta kazi angesimamia mchakato huru na haki kulifufua shirika letu la ndege. Kama kawaida ya Mwakyembe na wenzake ametumia taratibu kumwondoa mtu ambaye mimi naamini alikua anafanya kazi kizalendo na analipenda shirika! Walioua ATCL ni wanasiasa na watendaji serikalini. Inaumu sana kwetu sisi ambao tumetumia huduma za shirika ili toka tukiwa watoto wadogo!

Mkuu kwani ATCL imefungwa baada ya Chizi kufukuzwa?
Kwani huyu Chizi si aliwahi kuwa ATC kabla ya kustaafu? Mkuu namuunga mkono Mwakyembe kwa sasa until he proves me wrong.
 
Maswali ni mengi sana juu ya hili jambo, nafikiri tumpe muda Mh. Dr. Mwakyembe then tutajua mbivu na mbichi katika sakata hili!
 
Back
Top Bottom