Mr pianoman
JF-Expert Member
- May 22, 2019
- 2,549
- 6,102
Mimi kama kijana nisiye na ajira pia nimekosa mtaji wa kuanzisha biashara ili kuendana na ile kauli ya vijana tujiari inayo tolewa na wanasiasa au viongozi wa serikali ambao na wenyewe wameajiriwa serikalini.
Napenda kuishauri serikali yangu ifikirie kuweka kipengele cha ajira za miaka kumi yaani kuwe na ajira za kudumu kama ilivyo hivi sasa na kuwe na ajira za mkataba wa miaka kumi.
Hapa namaanisha kuwe kuna ajira zinazo tangazwa special kwa mkataba wa miaka kumi tu hapa serikali inaweza kuajiri kada zote ila baada ya miaka kumi mtu anastaafu na kupisha wengine.
Lengo hapa ni kupunguza ukosefu wa ajira na kuwapatia vijana mtaji wa kwenda kuendeleza ile sera ya vijana tujiari. Serikali kwa kufanya hivi itakuwa imesaidia vijana wengi na wengi wao wataitumia nafasi hii kuhakikisha hawastaafu kizembe.
Kupitia vijana hawa hawa watakao staafu baada ya miaka kumi na kwenda kuanzisha biashara zao mtaani kuna vijana wengine pia watapata fursa kupitia kwa hawa vijana.
Note: hizo ajira zitatoka kwa ajili ya mkataba wa miaka kumi tu hivyo ni vijana wenyewe kuangalia kama itampendeza kuomba au aendelee kukaa mtaani akisubiri ajira za kudumu za serikali.
Ni ushauri wangu tu huu kwa serikali mimi kijana wa kidato cha nne. Asanteni