Kukiwa pia na ajira serikalini za mkaba wa miaka kumi kisha mtu anastaafu kupisha wengine itapendeza zaidi.

Mr pianoman

JF-Expert Member
May 22, 2019
2,123
2,000
Mimi kama kijana nisiye na ajira pia nimekosa mtaji wa kuanzisha biashara ili kuendana na ile kauli ya vijana tujiari inayo tolewa na wanasiasa au viongozi wa serikali ambao na wenyewe wameajiriwa serikalini.

Napenda kuishauri serikali yangu ifikirie kuweka kipengele cha ajira za miaka kumi yaani kuwe na ajira za kudumu kama ilivyo hivi sasa na kuwe na ajira za mkataba wa miaka kumi.

Hapa namaanisha kuwe kuna ajira zinazo tangazwa special kwa mkataba wa miaka kumi tu hapa serikali inaweza kuajiri kada zote ila baada ya miaka kumi mtu anastaafu na kupisha wengine.

Lengo hapa ni kupunguza ukosefu wa ajira na kuwapatia vijana mtaji wa kwenda kuendeleza ile sera ya vijana tujiari. Serikali kwa kufanya hivi itakuwa imesaidia vijana wengi na wengi wao wataitumia nafasi hii kuhakikisha hawastaafu kizembe.

Kupitia vijana hawa hawa watakao staafu baada ya miaka kumi na kwenda kuanzisha biashara zao mtaani kuna vijana wengine pia watapata fursa kupitia kwa hawa vijana.

Note: hizo ajira zitatoka kwa ajili ya mkataba wa miaka kumi tu hivyo ni vijana wenyewe kuangalia kama itampendeza kuomba au aendelee kukaa mtaani akisubiri ajira za kudumu za serikali.

Ni ushauri wangu tu huu kwa serikali mimi kijana wa kidato cha nne. Asanteni
 
R.K

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
203
250

Umewaza vema sana.
 
ruaharuaha

JF-Expert Member
Feb 14, 2018
1,923
2,000
Watakuwa wapigaji sana. Wakijua wana muda mchache sana.

Muhimu masomo ya finance, commerce, businesss, jinsi kutumia pesa, kuzalisha, kukuza biashara compound interest, math, vyuo vya veta kuimarishwa.
 
Congressman

JF-Expert Member
Jun 2, 2020
442
1,000
Umewaza vyema ila umewaza ki-layman zaidi, hopeful wataalamu wa mambo ya Human Resource watanielewa.

Ukimuajiri mtumishi kwa miaka 10 tayari anakuwa ni asset kama zilivyo nyingine kwenye taasisi. Sababu ndani ya miaka 10 huyu mtu unakuwa umempika na ameiva kiutendaji, kiufupi anageuka kuwa lulu. Sasa kwa akili ya kitaalamu huwezi kuvunja mkataba na mtu wa hivi alaf uajiri kijana kiduku mwingine uanzie upya kumtrain, hapo lazima utaleta demage katika ufanisi wa kazi na taasisi kwa ujumla.

Taasisi nyingi zinajivunia watumishi wa muda mrefu shirikani sababu wanakuwa wameiva na kuingia kwenye system na kuepelekea utendaji wa kazi kuwa wenye tija ndomana Makampuni mengi yakitoa ajira huwa yanafocus mtu wenye experience.

Hivyo endapo serkali itatendea kazi ushauri wako hiyo itakuwa ni mistake kubwa na misuse of human resources.
 
Ajira za kudumu zinakuwepo kama kawaida mkuu ili kuendeleza wazoefu kazini.
 
tarvian

Senior Member
Feb 6, 2014
139
225
Watakuwa wapigaji sana. Wakijua wana muda mchache sana.

Muhimu masomo ya finance, commerce, businesss, jinsi kutumia pesa, kuzalisha, kukuza biashara compound interest, math, vyuo vya veta kuimarishwa.
Mkuu unadhani hayo masomo sasa hivi hayapo? Yapo Ila hayawezi kufanya chochote au kumsaidia kijana kama hana MTAJI wa biashara. Masomo yatafundishwa, veta inaimarishwa kila siku Ila kama hauna njia ya kupata MTAJI ni kazi bure na wanao piga debe ujiajiri wenyewe wameajiriwa.
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
3,283
2,000
Mimi kama kijana nisiye na ajira pia nimekosa mtaji wa kuanzisha biashara ili kuendana na ile kauli ya vijana tujiari inayo tolewa na wanasiasa au viongozi wa serikali ambao na wenyewe wameajiriwa serikalini.

Napenda kuishauri serikali yangu ifikirie kuweka kipengele cha ajira za miaka kumi yaani kuwe na ajira za kudumu kama ilivyo hivi sasa na kuwe na ajira za mkataba wa miaka kumi.

Hapa namaanisha kuwe kuna ajira zinazo tangazwa special kwa mkataba wa miaka kumi tu hapa serikali inaweza kuajiri kada zote ila baada ya miaka kumi mtu anastaafu na kupisha wengine.

Lengo hapa ni kupunguza ukosefu wa ajira na kuwapatia vijana mtaji wa kwenda kuendeleza ile sera ya vijana tujiari. Serikali kwa kufanya hivi itakuwa imesaidia vijana wengi na wengi wao wataitumia nafasi hii kuhakikisha hawastaafu kizembe.

Kupitia vijana hawa hawa watakao staafu baada ya miaka kumi na kwenda kuanzisha biashara zao mtaani kuna vijana wengine pia watapata fursa kupitia kwa hawa vijana.

Note: hizo ajira zitatoka kwa ajili ya mkataba wa miaka kumi tu hivyo ni vijana wenyewe kuangalia kama itampendeza kuomba au aendelee kukaa mtaani akisubiri ajira za kudumu za serikali.

Ni ushauri wangu tu huu kwa serikali mimi kijana wa kidato cha nne. Asanteni
Mtu akikaa kazini miaka 10,anakuwa na uzoefu mkubwa,kazi anakuwa ameijua vzr,sasa kumuachisha kazi harafu uajiri mwingine asiye na uzoefu ni matumizi mabaya ya rasilimali,itakuwa ni kichekesho ufukuze wahandisi na madakitari wote waliotimiza miaka 10 kazini,eti uajiri wengine wapya harafu uanze ku wapa uzoefu kwa gharama kubwa,
Kwahiyo kwa miaka 10,vijana wakae tu nyumbani wakisubili kuajiriwa?
Hii haisaidii chochote,hata ukifukuza watumishi wote wa umma kuanzia Katibu kata,Mwalimu mpaka Raisi,ukaweka wengine,huwezi kutatua tatizo la ajira,kila mwaka sokoni wanaingia vijana 800000,kwa miaka 10,ni vijana millioni 8!watumishi wa umma hawafiki millioni 1!
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
3,283
2,000
Serikali haina masikio,Mimi Mara zote ntapendekeza umri wa kustaafu uwe miaka 45 ili kila kijana apate nafasi ya kulitumikia taifa lake.
Bakheresa,Mo,Didmond,Van boy,Freddy vunja bei,hawa wote wanalitumikia Taifa,na wewe unaweza ukalitumikia Taifa kwa Kulima,kufuga,kupamba kucha za wadada,kusuka nywele,bodaboda,mie mwenzenu nimeamua kuwa beachboy huku Zenj,nimeona nigonge vibibi vya kizungu,nipate pesa,mavyeti nimetupa mbali.
Kila kijana anataka aajiriwe,ajira zenyewe chache,na hata ajira za hadhi ya hawa ma graduate,kuzipata mbinde,
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
10,474
2,000
Sasa kwa akili ya kitaalamu huwezi kuvunja mkataba na mtu wa hivi alaf uajiri kijana
Kijana mwenyewe hana anachojua zaidi ya kuboost makalio na manyonyo ama kwa wavulana ni kunyoa kiduku na kuvaa milegezo.

Simu zao zimejaa video za ngono plus soga za umbeya..

Nitarudi ngoja nikale msosi ushaiva saa hizi
 
legend Babushka

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
515
1,000
Hakuna kampuni itakubali kufanya hili jambo. Mojawapo ya sifa za kuweza kutulia kwenye soko ni utulivu wa wafanyakazi. Uzoefu wa miaka mingi huleta commitment kwenye kazi ambayo muajiri anaweza kuweka long term goals ambazo zitawekeza high capital.

Mabadiliko ya kila mara hata hayana tija kwa waajiriwa sababu unakosa kujiamini ukijua hutaweza kufikia malengo yako kwa fixed term employment.
 
rr3

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,863
2,000
Well said....

Au Serikali itumie flat rate method ambapo 1 mil itoshe kulipa wafanyakazi wasiopungua watatu no matter cheo chake.

Hii itasaidia kuajiri wengi zaidi.

Lakini pia viwanda vipewe kipaumbele ili export iwe kubwa kuliko import na matumizi yawe Bei nafuu.
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
6,310
2,000
Serikali haiwezi kufanya hiki kitu mkuu, labda huko sekta binafsi......serikali inakuajiriri ukiwa bado kijana mdogo, unapanda ngazi kiuweledi na kiuzoefu kuwa afisa mwandamizi na kupewa madaraka zaidi ya kiutendaji na kimaamuzi. Namaanisha utumishi wa umma unajengwa kwa ku- recruit na ku-retain watu ndo maana wameweka na umri wa kustaafu kisheria. Mfano chukulia serikali imeajiri mtu akiwa na miaka 25, akistaafu na miaka 35 itaweza kumlipa pesheni za kila mwezi hadi atakapofariki?
 
ruaharuaha

JF-Expert Member
Feb 14, 2018
1,923
2,000
Mkuu unadhani hayo masomo sasa hivi hayapo? Yapo Ila hayawezi kufanya chochote au kumsaidia kijana kama hana MTAJI wa biashara. Masomo yatafundishwa, veta inaimarishwa kila siku Ila kama hauna njia ya kupata MTAJI ni kazi bure na wanao piga debe ujiajiri wenyewe wameajiriwa.

Labda kuwe na Bank maalum kuwapa vijana grants, na mikopo hasa kwa vikundi.

Kila mwaka labda zitengwe pesa kadhaa kusaidia biashara kwa vijana.

Kilimo kinaweza kuwakomboa vijana. Population inaongezeka kila siku. Kwa hiyo mahitaji na huduma za chakula, makazi, Afya, private, quality, education zitaongezeka pia.

Serikali inaweza kuweka mikakati kutumia hizi fursa kuwawezesha vijana.

Kwenye kilimo Serikali inaweza kuwapa vijana ardhi wakalipa kiasi kadhaa kama down payment 10% (kama mortgage kwenye nyumba), watailipia taratibu asilimia fulani wakiuza mazao yao kwa miaka kadhaa.

Labda heka kumi kwa vijana watano. Halafu wakishirikiana na wataalamu wa SUA kulima na kufuga kisasa.
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
11,708
2,000
Hata umri wa kustaafu ukifanywa miaka 30 vijana wote wasio na ajira hawawezi kuajiriwa serikalini. Hata Robo hawawezi kuajiriwa serikalini. Sekta binafsi ndio injini ya uchumi na ajira katika nchi.
Serikali haina masikio,Mimi Mara zote ntapendekeza umri wa kustaafu uwe miaka 45 ili kila kijana apate nafasi ya kulitumikia taifa lake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom