Kukithiri udhalilishaji wa viongozi nchini ipo haja ya kuendesha mafunzo ya uzalendo nchi nzima

Binti Msichana

Senior Member
Oct 9, 2016
109
247
Kwa uhalisia kila kukicha baadhi ya Watanzania wanazidi kuwakosea heshima viongozi wetu wakitaifa kwa kuwadhalilisha kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Tena wengine ni watu maarufu na wenye nyadhifa katika jamii.

Kibaya zaidi watu hawa wanatumia vibaya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa kuwadhihaki na kuwakebehi viongozi wetu waliojitolea kwa hali na mali kututumikia sisi wananchi.Wanatumia vyombo hivyo kuidhihaki serikali na kupotosha wananchi.Hawaoni mazuri ya serikali na viongozi wake.

Tabia hii imezidi kuwa sugu bila kuogopa sheria za nchi kama ile ya makosa ya mitandaoni.

Kinachoonekana hapa ni kukosekana kwa uzalendo kwa watu hawa wenye kuwakosea heshima viongozi na Taifa kwa ujumla.

Hivyo kupunguza hali hii kuwe na mafunzo ya uzalendo kwa kila mtu nchi nzima ili kupunguza tabia hii inayozidi kuligawa Taifa.

Elimu ya uzalendo inayogusa makundi yote ya kijamii ni muhimu sana hasa wakati huu ili kwenda sambamba na juhudi za rais wetu John P.Magufuli za kubadilisha maisha ya Watanzania kwa uongozi wake bora na uliotukuka kwa maslahi ya Taifa.
 
wazalilishaji ndio hao wanatakiwa watoe mafunzo hapo unafikiri utajenga au utabomoa?
 
Hata Rais anatakiwa kuwa mwangalifu na matamshi yake.Ukiwa huna matamshi ya heshima kama Baba tegemea watoto nao watakuwa hivyo hivyo.
 
Udikteta uchwara kwenye nchi yetu unatakiwa kupingwa kwa nguvu kwa kila mtanzania mwenye akili timamu. Mkitaka kuwaabudu viongozi wenu huko vyama vyenu. Msitupangie kila mtu atavuna alichopanda kwa muda wake.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa uhalisia kila kukicha baadhi ya Watanzania wanazidi kuwakosea heshima viongozi wetu wakitaifa kwa kuwadhalilisha kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Tena wengine ni watu maarufu na wenye nyadhifa katika jamii.

Kibaya zaidi watu hawa wanatumia vibaya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa kuwadhihaki na kuwakebehi viongozi wetu waliojitolea kwa hali na mali kututumikia sisi wananchi.Wanatumia vyombo hivyo kuidhihaki serikali na kupotosha wananchi.Hawaoni mazuri ya serikali na viongozi wake.

Tabia hii imezidi kuwa sugu bila kuogopa sheria za nchi kama ile ya makosa ya mitandaoni.

Kinachoonekana hapa ni kukosekana kwa uzalendo kwa watu hawa wenye kuwakosea heshima viongozi na Taifa kwa ujumla.

Hivyo kupunguza hali hii kuwe na mafunzo ya uzalendo kwa kila mtu nchi nzima ili kupunguza tabia hii inayozidi kuligawa Taifa.

Elimu ya uzalendo inayogusa makundi yote ya kijamii ni muhimu sana hasa wakati huu ili kwenda sambamba na juhudi za rais wetu John P.Magufuli za kubadilisha maisha ya Watanzania kwa uongozi wake bora na uliotukuka kwa maslahi ya Taifa.
Kwa mujibu wa kamusi ya majuha wa Lumumba, maana ya uzalendo itakuwa ni kushangilia kila jambo hata lisilokuwa la maana bora tu limetamkwa na mmoja wa mafisiem.
 
Back
Top Bottom