Kukiri Waziri Mkuu wa UK kwamba yeye ni Zayuni "la kutupwa"

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,990
17,869
Kukiri Waziri Mkuu wa UK kwamba yeye ni Zayuni "la kutupwa"

Oct 07, 2022 02:36 UTC

[https://media]

Liz Truss ambaye ni karibu mwezi mmoja tu nyuma ameanza kazi ya uwaziri mkuu wa Uingereza, amejitokeza hadharani na kutangaza kuwa yeye ni Zayuni "la kutupwa" yaani Mzayuni mkubwa sana na amesema atahakikisha uhusiano wa London na Wazayuni utaimarika mno wakati wa uongozi wake.

Waziri mkuu huyo wa Uingereza ametangaza uungaji wake mkono kwa Wazayuni kiasi chote hicho wakati ambapo hakuna chochote kipya kwa nchi za Magharibi kwani kwa miaka mingi nchi hizo hasa Uingereza na Marekani ni waungaji mkubwa mno wa jinai za utawala wa Kizayuni tena kwa kila upande.

Kwa makumi ya miaka sasa utawala wa Kizayuni unawafanyia dhulma na jinai kubwa Wapalestina, unawaua kikatili na unaendelea kuwapora ardhi zao na sehemu yake kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huku jamii ya kimataifa ikiendelea kukaa kimya bila ya kuchukua hatua za kuilazimisha Israel ikomeshe jinai zake hizo. Si hayo tu, lakini pia madola ya kibeberu kama Marekani na Uingereza yanazuia hata kuwafikia Wapalestinna misaada ya madawa na matibabu, yote ikiwa ni kwa shabaha ya kuusaidia utawala wa Kizayuni uendeleze ukatili wake dhidi ya Wapalestina. Siasa hizo zinawakasirisha watu wengi duniani na sasa kila mwenye mtazamo huru anakubali kuwa Wapalestina wanadhulumiwa. Lakini kama tulivyosema, viongozi wa nchi za Magharibi hasa Uingereza na Marekani wanatangaza waziwazi kuunga mkono jinai hizo za Israel na hivi sasa tunamuona waziri mkuu wa Uingereza akisema mbele ya kadamnasi ya watu kuwa yeye ni Mzayuni mkubwa sana na atahakikisha uhusiano wa nchi yake na Wazayuni unakuwa mkubwa zaidi wakati wa uongozi wake. Mtu unajiuliza, Liz Truss anataka kuongeza nini kipya katika uhusiano huo wakati hakuna sehemu iliyobakia tupu? Au ameamua kujikomba tu kwa Wazayuni wenzake?

[https://media]Sami Abu Zuhri

Sami Abu Zuhri, mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS anasema: Matamshi ya Liz Truss ya kuunga mkono utawala wa Kizayuni maana yake ni kutangaza kuwa yuko pamoja na jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina. Ni watu wa namna hii ndio wanaochochea kuendelea kuuliwa watoto wadogo wasio na hatia na wanasimama imara kuficha jinai hizo.

Katika upande mwingine, kitendo cha nchi za Magharibi cha kuipa Israel kiwango kikubwa cha silaha za kufanyia jinai na ukatili, ni miongoni mwa mambo yanayolalamikiwa mno na makundi ya kutetea haki za Wapalestina. Hivi karribuni kundi moja la watetezi wa Palestina lilikusanyika mbele ya benki ya Berkley mjini Manchester huko Uingereza na kuitaka nchi hiyo iache kutumia fedha za wananchi kuupa silaha utawala wa Kizayuni. Taasisi hiyo ya kupiga vita umaskini imesema, uongozi wa benki ya Berkley ndio unaogharamia fedha za silaha za utawala wa Kizayuni na kuchochea jinai na mauaji ya Wazayuni dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Palestina.

[https://media]Liz Truss, waziri mkuu wa Uingereza aliyejigamba kuwa yeye ni "Zayuni la kutupwa"

Abdel-Latif al-Qanou ni msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS. Yeye anasema, uamuzi wa Liz Truss wa kuhamishia Quds ubalozi wa Uingereza kutoka Tel-Aviv na kutangaza waziwazi uungaji mkono wake kwa utawala wa Kizayuni, ni kutangaza rasmi uadui wa Uingereza kwa taifa la Palestina. Ameongeza kuwa, mji wa Baytul Muqaddas ni ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Mji huu ni mali ya taifa letu. Kuhamishia Quds ubalozi wowote ule hakuwezi kubadilisha uhakika huo wa kihistoria.

Ukweli ni kuwa Wapalestinna hawana matumaini hata chembe ya kuungwa mkono na madola ya Magharibi. Matumaini yao wameyaelekeza kwenye uungaji mkono wa mamilioni ya watu wenye fikra huru katika pembe mbalimbali za dunia ambao mara kwa mara wamekuwa wakichukua hatua za kuonesha uungaji mkono wao kwa malengo matukufu ya ukombozi wa Palestina. Aidha inaonekana wazi kabisa kwamba Wapalestina hawakushangazwa na hatua ya waziri mkuu wa Uingereza, Lizz Truss ya kutoka hadharani na kuutangazia ulimwengu kuwa yeye ni Mzayuni mkubwa.

View attachment 2380159
4c0y179d39307325jup_800C450.jpg

Sent from my TECNO KD6 using JamiiForums mobile app
 
Ukiona nchi yoyote inashinda vita, ujue ina siraha za hali ya juu zilizotengenezwa Kwa mkono wa wazayuni (Israel) na ilipia hiyo gharama ya utengenezaji wa siraha hizo za technology ya hali ya juu zaidi,

Na zile zinazoshindwa vita ujue hawataki hizo siraha Kutoka Kwa usiowapenda!
 
Mungu akikubariki hakuna wa kukulaani, mnahangaika bure tu na hawa Wayahudi, wamependwa hawa.
 
Mtu unajiuliza, Liz Truss anataka kuongeza nini kipya katika uhusiano huo wakati hakuna sehemu iliyobakia tupu? Au ameamua kujikomba tu kwa Wazayuni wenzake?
Hakuna Muyahudi mweupe wewe!! hao unao waona leo, hao ndani ya Israel ya leo ni mabaki ya waingereza, waturuki, greeks, Waarabu hao ile nchi ya Isarel walipewa maksudi na hao hao! Babu zao! lkn ni walewale!

USA,UK, CANADA nk! ni wale wale tu!! fungua akili hiyo uelewe!! tabaka tawala lilitawala enzi na enzi hawazuliani hata kidogo! hakuna kujikomba wanaendeleza fkra za baba/babu zao! usijidanganye!

Wayahudi original walipotea mpaka leo hawajulikani walipo Duniani, wale wazungu/waarabu wa leo ni walee vitukuu vya Majemadari wa Alexander de Great! na tawala nyingine kubwa kubwa zilizo kuwepo hapo Duniani!

Israel ya leo ina siri kubwa sana juu ya uwepo wao hapo mashariki ya kati, fikiria tu hawatikisiki hata chembe wamezungukwa na maadui kila kona! kwa taarifa yako wata tawala mpakaa Nile na viunga vyake!

Ndo maana ya alama zile mbili za Blue, pamoja na Nyota, tunao ijua Siri hii Africa hatufiki hata KUMI!......usiniulize kwa nini!.....ila jua hao! km wao!! hkn cha kujikomba ndo walivo!

ni Agenda zao fiche tangu miaka 6000 iliyo pita tena, tegemea Mengi zaidi ya hayo kutoka UK/Israel!!
 
Wayahudi original ni weusi? Nani alikupa habari hii? Unaweza toa ushahidi kuthibitisha hili?
 
Sasa kuna mtu mwenye akili timamu atasimama na watu wajinga km wapalestina?

Wapalestina wajinga kwa sababu wanachokipigania hawajui ndio maana hata waarabu wengi waneachana na hao wapuuzi

Tena bora huyu mwanamama yule muhindi aliyekosa uwaziri mkuu hataki kabisa kusikia kitu palestine
Brainwashed & mental slavery
 
Hakuna Muyahudi mweupe wewe!! hao unao waona leo, hao ndani ya Israel ya leo ni mabaki ya waingereza, waturuki, greeks, Waarabu hao ile nchi ya Isarel walipewa maksudi na hao hao! Babu zao! lkn ni walewale!

USA,UK, CANADA nk! ni wale wale tu!! fungua akili hiyo uelewe!! tabaka tawala lilitawala enzi na enzi hawazuliani hata kidogo! hakuna kujikomba wanaendeleza fkra za baba/babu zao! usijidanganye!

Wayahudi original walipotea mpaka leo hawajulikani walipo Duniani, wale wazungu/waarabu wa leo ni walee vitukuu vya Majemadari wa Alexander de Great! na tawala nyingine kubwa kubwa zilizo kuwepo hapo Duniani!

Israel ya leo ina siri kubwa sana juu ya uwepo wao hapo mashariki ya kati, fikiria tu hawatikisiki hata chembe wamezungukwa na maadui kila kona! kwa taarifa yako wata tawala mpakaa Nile na viunga vyake!

Ndo maana ya alama zile mbili za Blue, pamoja na Nyota, tunao ijua Siri hii Africa hatufiki hata KUMI!......usiniulize kwa nini!.....ila jua hao! km wao!! hkn cha kujikomba ndo walivo!

ni Agenda zao fiche tangu miaka 6000 iliyo pita tena, tegemea Mengi zaidi ya hayo kutoka UK/Israel!!
Waisrael oG walipotea haijukikani walipo.
Halafu unasema tena mnaojua siri mko 10 tu.
Aisee .
Ujinga nacho ni kipaji
 
Sasa kuna mtu mwenye akili timamu atasimama na watu wajinga km wapalestina?

Wapalestina wajinga kwa sababu wanachokipigania hawajui ndio maana hata waarabu wengi waneachana na hao wapuuzi

Tena bora huyu mwanamama yule muhindi aliyekosa uwaziri mkuu hataki kabisa kusikia kitu palestine
Wanapigania taifa lao waliloporwa, kipindi wayahudi wanachinjwa kma kuku na Hitler mliona ni haramu ila wapalestina kuuawa Kila siku mnaona ni haki. Siku meza ikigeuka kma kipindi Cha Hitler msirudi hpa kulialia
 
Mungu akikubariki hakuna wa kukulaani, mnahangaika bure tu na hawa Wayahudi, wamependwa hawa.
Wamependwa na nani? Unaweza niambia makabila 10 Yako wapi au unadhani makabila 12 yote yapo Hadi Leo? Acheni kupotosha maandiko, wayahudi na sawa na Mimi na wewe tu hawana special treatment yoyote Ile in fact hata hawamuamini Yesu mnayemuabudu na wanatuona manyani tu.
 
Wazayuni wamebarikiwa kuanzia baba zao Abraham , Isaac na Jacob .
Jacob alibadilishwa jina na kuitwa Israel maanake “ ni mshindi “
 
Mimi mwenyewe mzayuni wa kutupwa kama huyo Waziri mkuu wa Uingereza

Wazayuni tuko kila nchi duniani
 
Back
Top Bottom