Kukimbiza kuku wa kienyeji?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Hili swali limekuwa likinitatiza sana.. kwanini kuna raha ya aina fulani kufukuza kuku wa kienyeji kabla ya kumfanya kitoweo?
 
Haahaaa umeniacha mbavu sina asubuhi asubuhi....haya maswali yako ya siku hizi, mhhh.
Nafikiri enjoyment yake ni kutoa jasho na kutanua mbavu ili kupata nafasi ya kushushia hicho kitoweo.Lol
 
Kwanza wakati akimbiapo,unamuona kwa nyuma anavyochezesha mkia wake,alafu chenga atakazo kuwa anakupiga zitafanya ufurahi maana wakati mwingine chenga hizo ni ndogo sana kiasi kwamba ungeweza kumksmata,lkn ukishamkamata si unajua hana tena nguvu ya kukimbia?nadhani unajua kitakacho fuata kitoweo tu then baada ya kula unalala chali kwa uchovu wa kushiba!
 
hahahaha! swafi sana! hasa unapofukuzia sanaaaaaaaa kisha anakuletea mapozi we unaachana naye. Baada ya muda akiona umuhimu wako akirudi basi ukitafuna anakuwa hana ujanja kabisa! Tena wakati unachinja unamkumbusha alivyokusumbua, utamsikia akisema 'na wewe naeeeee anmhhhh'
 
Hili swali limekuwa likinitatiza sana.. kwanini kuna raha ya aina fulani kufukuza kuku wa kienyeji kabla ya kumfanya kitoweo?

huu mtego sasa; ngoja nijaribu...
kuku wa kienyeji hushinda nje siku nzima hivyo kama unataka kuchinja lazma umtaim ndio umpate na mara nyingi ni wajanja hivyo inabidi wakimbie --- hasa wakisikia sauti ya kisu kinanolewa, na ndio maana ni watoto mara nyingi ndio wakimbizao kuku wa kienyeji.... ila sasa ukimtaim asubuhi saaaana au jioni wakiwa mabandani, unampata kirahisi sana

vilecile kwa kalcha na maisha yetu, kula kuku ni ishara ya neema nyumbani kwahiyo siku hiyo kuku atakimbizwa hadi kila jirani ajue leo kwa mwafulani wanakula kitoweo :eek::D
 
Mzee siku hizi una mafumbo kweli!

Uzuri wa kuku wa kienyeji wala hakimbii kwenda mbali na nyumbani. Atakuzungusha hapo hapo nyumbani tu! Akiona unataka kukata tamaa, anaingia mwenyewe bandani tayari kwa kufanywa kitoweo..Lol
 
Kwanza wakati akimbiapo,unamuona kwa nyuma anavyochezesha mkia wake,alafu chenga atakazo kuwa anakupiga zitafanya ufurahi maana wakati mwingine chenga hizo ni ndogo sana kiasi kwamba ungeweza kumksmata,lkn ukishamkamata si unajua hana tena nguvu ya kukimbia?nadhani unajua kitakacho fuata kitoweo tu then baada ya kula unalala chali kwa uchovu wa kushiba!
sasa wajameni mnamzungumzia kuku ninaemfahamu mimi au?...!
 
Hahaha Mzee Mwanakijiji wewe ni kiboko, raha yake nyingine ni ku draw attention kwa majirani kwamba leo mnakula kuku si maharage tena hahaha.
 
sasa wajameni mnamzungumzia kuku ninaemfahamu mimi au?...!

hahahaha kaka bwana bado tu!?

hawa kuku wetu hawa yaani hawa kuku wetu hawa kuna raha yake hasa huy wa kienyeji wakati unamkimbiza, wakati mwingine anarukia mibani unsita kidogo baadaye unamuona anakuja usawa wako mwenyewe anajaribu kuruka juu pembeni aktua tu unae, analia pale baada ya mda ananyamaza unamweka kwapani hadi home, unaanda kisu na mahali pa kumchinjia,
ukimshika shingon na kuwmachia unaona macho yanalegea, na wazuri sana ni wale ambao hawajataga.
 
Hahaha Mzee Mwanakijiji wewe ni kiboko, raha yake nyingine ni ku draw attention kwa majirani kwamba leo mnakula kuku si maharage tena hahaha.
Haahaa mkuu hii nimeipenda...mpaka jirani naye anajua leo kuna kuku anakimbizwa ili aje awe kitoweo!Lol
 
wakuu,
sasa huyu kuku anaingiaje kwenye hili jukwaa maridhawa la MMU?....
 
Kuna raha yake kumkimbiza kuku wa kienyeji bwana ..kwanza kijasho chembamba kikutoke mala usimame ufikilia chenga zipi za kumpata ndio uendelee na zoezi la kukimbiza tena ,mpaka kumchinja na kumfanya kitoweo aaah wewe mwenyewe unafurahi na kujisemea vijineno vya hapa na pale ....
aaah huyu kuku wa kienyeji mtamu sana,thupu yake ndo usiseme lakini kanisumbua huyu kanipiga chenga mpaka nimechomwa miiba ,nimeanguka mie mtu mzima ..Nk nk .
Lakini mwisho wa yote umepata kitoweo !
 
Mzee siku hizi una mafumbo kweli!

Uzuri wa kuku wa kienyeji wala hakimbii kwenda mbali na nyumbani. Atakuzungusha hapo hapo nyumbani tu! Akiona unataka kukata tamaa, anaingia mwenyewe bandani tayari kwa kufanywa kitoweo..Lol

Kuku wa kienyeji anakimbizwa ikiwa suala la kumla limetokea ghafula!(mgeni au mtu muhimu kaja ghafula). Lakini kuku wa kienyeji ambaye ameishapigiwa mahesabu ya kuliwa anashikwa mapema (jioni anapoingia kibandani au asubuhi kabla hajatoka kibandani)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom