Kukemea uovu sio udini-Pengo

Shaycas

JF-Expert Member
Feb 13, 2009
906
110
RSS
Home
BOOKMARK THIS PAGE
Kukemea uovu si udini -Pengo
Send to a friend
Monday, 06 December 2010 08:39
0
digg
Kardinali Pengo
Boniface Meena
WAKATI serikali ikionyesha hofu ya
udini kuingizwa kwenye siasa, Kanisa
Katoliki limesema kuwa halitaacha
kukemea uovu hata kama uovu na
uozo huo unafanywa na watu walio
madarakani kwa kuwa kufanya hivyo si
udini.
Mara kadhaa wakati wa kampeni na
baada ya kuapishwa Rais Kikwete
alikuwa akizungumzia hofu yake ya
udini kuingizwa kwenye siasa na
akaweka bayana suala hilo wakati wa
hotuba yake kwenye Bunge jipya,
ingawa hakufafanua jinsi udini
ulivyopenyezwa.
Lakini jana, askofu mkuu wa Jimbo la
Dar es Salaam, Polycap Kadinali Pengo
alieleza kuwa hata kama walio
kwenye mamlaka watawatishia, kanisa
halitakuwa tayari kukaa kimya likiona
kuna uovu.
Kardinali Pengo alitoa msimamo huo
wa kanisa hilo kubwa nchini wakati
akitoa mahubiri yaliyorushwa na kituo
cha redio ya kanisa hilo cha Tumaini
katika ibada iliyofanyika kwenye
Kanisa la Utoto Mtakatifu kituo cha Hija
kilichopo Pugu jijini Dar es Salaam.
Pengo alisema kuwa viongozi wa
Kanisa Katoliki hawawezi kufumbia
macho uovu kwa kuwa hata viongozi
wa kanisa wanapofanya uovu
hukemewa bila uoga.
"Kamwe kanisa haliwezi kufumbia
macho uovu ili kundi moja liweze
kukaa kwenye mamlaka na uovu wao.
Hata kama mamlaka hiyo itatoa vitisho
kwa viongozi wakuu, Kanisa Katoliki
halitakaa kimya," alisema Pengo.
Alisema kuwa kukemea uovu
kusionekane kuwa ni udini na
ifahamike kuwa Kanisa Katoliki
halimsimiki mtu awe rais, diwani au
mbunge wa mahali popote, hivyo uovu
wowote unaofanywa na mamlaka
utaendelea kukemewa bila uoga.
"Katoliki linafahamu madhara
yanayoweza kujitokeza katika jamii
iwapo kanisa litampendekeza mtu
kuwa kiongozi," alisema Pengo.
"Tuliombee taifa letu liepushwe na
vitu vinavyotaka kuibuka katika taifa
na kamwe kanisa haliwezi
kumsimamisha mtu na kusema
mumpigie kura," alisema.
Alisema hawawezi kuwanyamazia
wanasiasa wakati hata maaskofu pia
wanakemeana wanapotenda uovu.
"Uovu lazima ukemewe, si kitu
ambacho mtu anafikiri kwamba mtu
anaweza kutishia kwamba maaskofu
wasikemee uovu," alisema Pengo.
Pengo alisema kuwa kutokana na
kumbukumbu ya hapo zamani wakati
wafalme walikuwa wakichaguliwa na
mapadri na maaskofu, madhara yake
yalijitokeza kwa kuwa jamii
ilichaguliwa kiongozi asiyekubalika.
"Viongozi wa Katoliki wataendelea
kukemea uovu huo kwa kuwa
unaweza kusababisha mafarakano
katika taifa linalotafuta ukweli na haki
kwa ajili ya wote,"alisema Pengo.
Katika taifa lililo na watu takriba
milioni 35 linaloundw ana idadi kubwa
ya Wakristo na Waislamu wanaoshi
pamoja, udini hauonekani kuwa silaha
ya ushindi kwenye siasa.
Lakini suala hilo lilizungumzwa sana,
hasa na viongozi wa chama tawala
 
Hao wanaosema kuhusu udini mbona hawamtaji mdini wa mfano ili ajulikane na ikiwezekana achukuliwe hatua?
You are right Baba Askofu , Mwadhama Cardinali Polycarp Pengo
 
Back
Top Bottom