Mangi Muitori
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 474
- 145
Peingine nyie ndio hamumumfahamu Lowassa, maana CCM wanamfahamu zaidi yenu mkimsoma katika magazeti tu, na wamemwaga. Kama angekuwa na nguvu hizo wasingethubutu ila walijua yote haya mapema sana na watu wake walitishiwa toka zamani kuwa akikosa Urais CCM atahamia CDM na bado CCM wamlimwaga - huwezi kufikiria hapo tu?
Pili, Lowassa akiwa Rais atakuwa rais wa Kundi lake yeye, na sio wa UKAWA maana Urais kautafuta kwa miaka 20 akiwa CCM kama ulivyosema, hao CDM wala NCCR hawakuwa naye wakati wote. Hilo kundi lake pekee kisha waahidi wizara na kushika mamlaka ya juu kabisa ya serikali yake ataweza vipi awaachie nyie ambao hamkuwa naye miaka yote?.. Na akisha apishwa akawa Rais ana kinga zote, Je,kimchagua Chenge waziri mkuu mtamfanya nini? hamtakuwa na la kusema ila kulalamika!..Ame Cross line kwa sababu ana uchu wa madaraka na huko CDM kumejaa mbumbumbu wachumia tumbo. Ebu fikiri moja kwanza Je akikosa Urais mtakuwa mtabakia na sura gani machoni mwa watu maana kuna kupata na kukosa!
Hizo Billioni mnazotegemea kupewa ili wabunge wenu waweze kuwa na fedha za kujitangaza hazitawasaidia chochote maana siku hizi watu wanakula mshiko kisha kura zao wanampa mtu mwingine. Sii wajinga hivyo na ndivyo alivyofanywa Lowassa kwenye vikao vya CC ya CCM watu walikula fedha na bado wakamwaga wengine wamesha mkimbia!...Imekula kwenu mkuu, tamaa ya fedha imewafikisha pabaya wala sii kutaka mageuzi ya kisiasa maana mngeweza hata bila yeye wala UKAWA kama mngejipanga na kusikiliza ushauri wa watu wanaojua Siasa..
Hivi alikatwa na CC au NEC au hukumsikiliza Nchimbi na Simba