Kukatwa kodi kwa mizigo

Sales93

Senior Member
Mar 5, 2014
146
73
Habarini wana jamvi, Ningependa kufahamu kama kuna suala la kukatwa kodi na TRA pale unapoagiza mzigo toka Ebay au Amazon, mizigo kama simu, nguo, perfumes N.K, nitashukuru sana kwa msaada wenu wenye experience na hiki kitu.
 
Swala la Kodi ndio lipo.

Pia kulipia kodi au koto lipia kodi (kwa baadhi ya bidhaa) hutegemea aina njia ya usafirishaji uliyotumia. Mfano KINDLE TAB ikija kwa dhl utalipia Kodi. Lakini hiyo hiyo kindle Tab ikija kwa njia ya posta Haulipii kodi. ( Hapa huwa nashindwa kuelewa vigezo vipi hutumika)
- Niliagiza Kindle PaperWhite - ilikuja kwa DHL, nililipa KODI
- Niliagiza Kindle Fire 7 - imekuja kwa njia ya posta sikulipa KODI

WP_20160807_09_27_02_Pro (2).jpg
 
View attachment 377258

Nashukuru kwa maelezo yako mkuu, nina maswali matatu ya mwisho
1. Kodi nitakayotakiwa kulipa kama nimetumia DHL au njia nyingine tofauti na posta ni asilimia ngapi?

2. Je kodi hii nalipia bandarini au pale nitakapopata mzigo wangu?
3. Nasikia hawa jamaa wa posta ni wezi sana wa mizigo kuna ukweli wowote hapo?maana naona wewe Kindle paperwhite yako uliipata salama.
 
SWALI 1: Kodi nitakayotakiwa kulipa kama nimetumia DHL au njia nyingine tofauti na posta ni asilimia ngapi?

Kodi hukokotolewa kutokana na Declared item value/ Assesses value
- Declared value - Hii hutoka kwa muuzaji wa bidhaa, huonyesha kiasi ulichonunulia
- Assessed Value - Hii hutokana na Maafisa wa ushuru wa forodha baada ya kukagua mzigo.
WP_20160807_12_39_10_Pro.jpg
1566400598069.png

(a) Iwapo atakubaliana na declared value, basi assessed value itakuwa ni hiyo hiyo ambayo iko kwenye invoice ilikuja na mzigo, KODI itakokotolewa kutegemea hiyo declared value

(b) Iwapo afisa ushuru wa forodha atakataa declared value, basi KODI itakokotolewa kutokana na thamani ya mzigo AUNAVYO YEYE, Assessed Value, hutumika hili neno "UPLIFT" - Yaani mfano declared value kwenye invoice ni dola 100, na wewe umelipia dola 100; Wakifanya uplift utaambiwa thamani ya mzigo wako, assesses valu, mfano ni dola 300 - Hivyo ukokotozi wa KODI utatokana na assessed value, Japokuwa wewe ulilipia dola 100 kwa bidhaa yako.

Hiki kipengele B ndicho huwaliza wengi.

MALIPO UTAKAYOLIPA (TOTAL TAXES)
- IMP - Import Duty ( 25% ya A )
- EX - Excise Duty ( _% )
- RDL - Railway Development levy ( 1.5% ya A )
- CPF - Customs processing fee ( 0.6% ya A )
- VAT - Value Added Tax ( 18% ya C)

EX, RDL na CPF - huwa ni kiasi kidogo fedha shida iko kwenye IMP & VAT

IMPORT DUTY Vs VAT
Mfano
A = Bei ya kitu pamoja na ghalama ya kusafirishia.

A X 25%= B ( kiasi utakachotozwa kama IMP )

A + B + (EX + CPF + RDL) = C (itatafutwa asilimia 18 yake)

C X 18% = G ( Ni kiasi cha VAT utakachotozwa )

TUANGALIE MFANO_1 WA BIDHAA NILIYONUNUA KWA DOLA 20 (SAWA NA TSH 43,819.60 KWA RATE YA 1USD=2,190.92TSH kwa Tarehe 05.03.2016)

Jinsi walivyo kokotoa KODI.
WP_20160807_12_39_40_Pro.jpg
1566400763324.png

MFANO_2 THAMANI YA BIDHAA KWA TSH NI 255,135.00
1566400798060.png

WP_20160807_12_40_04_Pro.jpg

NB
: Ukiangalia vyema picha ya kwanza ina EX (Excise Duty), ila ya pili Haina. Hivyo kodi kwa sasa hutegemea IMP + RDL + CPF + VAT

SWALI 2. Je kodi hii nalipia bandarini au pale nitakapopata mzigo wangu?

- Malipo yote hufanyika kabla ya kupewa mzigo.
- Kama kiasi cha kodi ni kidogo utalipa kupitia agents anayekuletea mzigo ofisini kwako au nyumbani - Hii hasa ni kwa DHL
- Kama malipo ya KODI ni kiasi kikubwa utapewa utaratibu wa malipo.
- Kuna njia zaidi ya moja ya kufanya malipo, waweza tumia menu ya MPESA, Maxmalipo, au Bank utapewa maelekezo na wahusika.

SWALI 3. Nasikia hawa jamaa wa posta ni wezi sana wa mizigo kuna ukweli wowote hapo?maana naona wewe Kindle paperwhite yako uliipata salama.

- Mizigo yangu yote iliyokuja kwa njia ya Post ilifika salama. Sijawahi kupoteza mzigo.
- Hilo swala la wizi watu husema, ila kwa mimi haijwahi kunitokea
- Kindle paperwhite yako uliipata salama? Ndio ilikuwa salama.
Nashukuru kwa maelezo yako mkuu, nina maswali matatu ya mwisho
1. Kodi nitakayotakiwa kulipa kama nimetumia DHL au njia nyingine tofauti na posta ni asilimia ngapi?
2. Je kodi hii nalipia bandarini au pale nitakapopata mzigo wangu?
3. Nasikia hawa jamaa wa posta ni wezi sana wa mizigo kuna ukweli wowote hapo?maana naona wewe Kindle paperwhite yako uliipata salama.
 
Swala la Kodi ndio lipo.

Pia kulipia kodi au koto lipia kodi (kwa baadhi ya bidhaa) hutegemea aina njia ya usafirishaji uliyotumia. Mfano KINDLE TAB ikija kwa dhl utalipia Kodi. Lakini hiyo hiyo kindle Tab ikija kwa njia ya posta Haulipii kodi. ( Hapa huwa nashindwa kuelewa vigezo vipi hutumika)
- Niliagiza Kindle PaperWhite - ilikuja kwa DHL, nililipa KODI
- Niliagiza Kindle Fire 7 - imekuja kwa njia ya posta sikulipa KODI

View attachment 377258
Nakumbuka niliwahi kugiza bidhaa zikaja kwa postal nikalipia baadhi na zingine sikulipa. Nilipowauliza ni kwamba kuna kiwango cha thamani ya bidhaa, ikizidi hiyo ndio kuna kodi. Nimesahau ni kiasi gani.
 
0718 55 300 3 Mwalimu RCT naomba unichek tufanyebiashara
NJIA ZA MAWASILIANO

Wasiliana nami kwa moja ya hizi njia
1. Kupiga simu/ Kutuma ujumbe: +255 (0) 788 203 160 au 0717 54 57 62
2. Barua Pepe (Email): mw1rct @ outlook.com
3. Whatsapp: +255 788 203 160
4. Skype: mw1rct
5. Telegram: @mw1rct

MUDA WA KUWASILIANA NAMI
1. 06:00 – 19:30hr (Saa 12:00 asubuhi HADI Saa 1:30 Usiku)– Simu/sms/whatsapp/telegram – utajibiwa hapo kwa hapo kwa hapo.
2. 19:30 – 06:00hr (Saa 1:30 usiku HADI Saa 12:00 asubuhi)– Niachie ujumbe wa simu (sms)/whatsapp/telegram/email, Na utajibiwa au kupigiwa simu kabla ya 08:00hr Kila siku.

THREAD YA REJEA
- www.v.ht/buy4me

KARIBU
 
nmeshindwa kuzoom hapo bro ila nina ndoto ya kununua gari flan hv used yenye thaman ya kama 1600dollar kwhy kaka ili ifike ni lazima niwe na kama 2400dollar kwa makadirio?
 
nmeshindwa kuzoom hapo bro ila nina ndoto ya kununua gari flan hv used yenye thaman ya kama 1600dollar kwhy kaka ili ifike ni lazima niwe na kama 2400dollar kwa makadirio?
Kwa swala la Gari - Ghalama ya kodi inatokana na vipengele vifuatavyo
  • Je gari husika ni ya mwaka gani?
  • Je ina cc ngapi?
  • Je CIF (Total Price) ni kiasi gani? etl
Kwa makadirio yake ya kodi ingia hapa: Tanzania Revenue Authority - Calculators & tools

upload_2016-12-15_14-44-56.png
 
Kwa upande wa electronics kama device yako inatumi sim card ndo utalipia inport duty ila kama ni v2 kama pc utalipia tu VAT
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom