Kukatisha maisha kwasababu ya Penzi

royna

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
479
335
Salaaam wana JF
Leo, humu JF nimesoma mdada wa India aliyejiua kwasababu ya mpenzi aliyemcheat, mdada wa kazi aliyejiua kwasababu ya Chris na mdada mwingine aliomba ushauri akitamani kujiua kwasababu ya mume anayemabuse!

Ndugu zangu kwanza niwape hongera wale ambao hawajawahi kusalitiwa na wapenzi, na ninawaombea isiwatokee. Pili niwape hongera wale ambao waliwahi kuumizwa wakaheal na kuendelea na maisha yao.

Tatu, naowaombea kwa Mungu wote ambao wana uchungu sasa na wanawaza wafanyaje.

Katika haya yote, ninawaombea na kuwashauri wahanga wote wa mapenzi kuwa usikubali kufa wala kuruhusu wazo la kufa likujie kwa sababu ya mpenzi because:
1. Anaweza akawa alikuwa anakupenda sana, ila tu akaghafirika njiani, so ukijiua unampa adhabu mara mbili
2. Anaweza akawa hakuwa serious from day 1, so kujiua kwako kunaweza kusiwe na maana yoyote kwako
3. Ni kwasababu hujakutana na mwingine, ukikubali yaishe na kujipa muda, unaweza shangaa, umepata mpenzi mwingine, mpaka ukajiuliza ulipotezaje muda huyo mwingine, kiasi hicho
4. Huyo mpenzi si wa thamani hivyo kulinganisha na wazazi wako, na ndugu wengine, kiasi cha kufanya wengine wote wakukose kwasababu yake
5. Yamkini Mungu anakuepusha na ndoa jela kwa kuruhusu uumie kwa kumkosa huyo kwa muda huu
6.Mwisho, kama wewe hukujiumba, huwezi kujikatisha maisha kwasababu aliyekuumba anajua sababu ya wewe kuishi duniani, hivyo acha Mungu akusaidie kukamilisha kusudi lake duniani.
 
Aisee kama unampenda mtu wako kwa dhati halafu ikatokea hitilafu hasa ya kuwa na mpenzi mwingine ni chungu kuliko kitu chochote. Inahitaji uwe na moyo wa ziada. Ndiyo maana nashauri sana usiamini sana na kupenda kupindukia maana kuna siku kunakuwa na mageuzi tu. Nilishaumia mara moja kwa hiyo huwa siruhusu tena ujinga. Napenda kawaida nikijuwa kuwa binadamu hubadilika, tena waliokula viapo sembuse boyfriend/girlfriend? Tujifunze kupenda kwa kiasi.
 
Every day wadada why does it mean Wanaume hawa face those problems or mwanamke anajali kuliko mwanaume
 
royna uliyoyasema ni kweli.
lakini kubwa kila mtu na ajifunze kutomtenda mwenzie jambo asilopenda kutendewa. Pole sana kwa wafiwa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom