Kukatika umeme bungeni, ni hatari. Chochote chaweza fanyika kwa wanaowindwa kudhuriwa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukatika umeme bungeni, ni hatari. Chochote chaweza fanyika kwa wanaowindwa kudhuriwa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Jul 12, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ni aibu kubwa sana kwa serikali hii kuahirisha bunge kwa sababu ya kukatika kwa umeme. Binafsi nashawishika kuona kuwa hiyo inaweza kuwa ni mbinu ya kujaribu kuwafanyia umafia baadhi ya wabunge machachari wanaoisumbua serikali. Wakati wa giza chochote chaweza kutokea. Hizo ndiyo mbinu za hali ya juu katika kukamilisha uovu. Siamini kama ukumbi wa bunge unakosa chanzo cha umeme wa ziada. Haingii akilini hata kidogo.
   
 2. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Ina maana hakuna hata jenereta za kuaminika !
   
 3. Y

  Yetuwote Senior Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeona, nashindwa kuamini.
   
 4. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  A state of art, and a masterpiece, an icon and landmark of Dodoma ikose backup power? :loco:
   
 5. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Inakupa picha halisi ya UOZO KATIKA UTENDAJI KAZI WA SERIKALI YETU; TAASISI ZAKE na kupoteza hata AKILI KIDOGO TUU YA MSINGI katika watendaji!!!!

  Sehemu kama JENGO LA BUNGE hakuna hata jenereta......Kama hata kwenye mjengo wao wanasahau chombo muhimu kama hicho TUSITEGEE WAKUMBUKE YANAYOTUHUSU SISI WAPIGA KURA!!!
   
 6. a

  afwe JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Serikali ya Magamba haina aibu. Ndio maana wamesikika wakisema CDM wamechakachua umeme bungeni wakati kila kitu kinasimamiwa na taasisi zao
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  hii ndo serikali mnayoitegemea iwafikishe kwenye maendeleo. kweli wa TZ tumelogwa
   
 8. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,426
  Trophy Points: 280
  Aibu kubwa sana kwa nchi
   
 9. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hili linahitaji mjadala wa kina. Na kwa nini naibu spika aahirishe kikao haraka haraka badala ya kutafuta ufumbuzi kwanza? Ni kama tukio lililokuwa limepangwa.
   
 10. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Hapa mwanza jana toka asubuhi hamna umeme,na leo maeneo ya mecco toka asbuhi hadi saa hii hamna umeme,kwa hiyo kama na mjengoni hamna umeme ngoma draw,ccm hoyeeee
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,953
  Trophy Points: 280
  Mkuu Excellent serikali DHAIFU haina uwezo
   
 12. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  BAK ni aibu sana aisee,high school niliyowahi kusoma umeme ukikatika jenereta inawashwa na mambo yanaendelea,jengo la bunge ni sehem yenye heshima kubwa sana
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,953
  Trophy Points: 280
  Zipo pesa za DHAIFU kwenda kubembea majuu.
   
 14. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #14
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Leo ndiyo ilikuwa siku ya kutoweka na lile rungu la dhahabu.
   
 15. D

  Doreen22 JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 475
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nina shaka na hilo pia, si ajabu wajifanye kukata umeme, hata wakarudia hivyo na siku nyingine tena, kwenye hilo giza, wakawafumulia kina Mnyika gesi ya sumu, kuwachoma sindano za sumu, kuwachoma na ule mwavuli wa sumu au kuwagonga na kitu kizito kisha waseme amejigonga bahati mbaya kwenye kiti or mlangoni wakati wa kutoka nje
   
 16. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Parliament in Tanzania forced to stop its session due to absence of power backup. Ndivyo international newsheadlines zitakavyosomeka. Aibu tupu
   
 17. GP

  GP JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  ilikua wazee wa kazi wafanye umafia wao kwa wabunge wa CDM, mbona mi nilikua mtaani makole huku umeme wala haukukatika, iweje ukatike mjengoni tu??
   
 18. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Mbona hiyo ilishatokea siku nyingi tangu Bunge lilipogeuzwa kuwa jumba la maonesho ya ze comedy za siasa. Hakuna mtu ye yote nje ya tanzania anaweza kushangaa. Ni wabongo pekee ambao bado tumeaminishwa au tumejiaminisha (unajua tena tu watu wa matumaini) kuwa pale ni mahali pa heshima na kufanyia maamuzi mazito kuhusu mustakabali wa jamii yetu.
   
 19. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hawa jamaa ni lazima kuna kitu mbaya wanataka kufanya .chezea magamba weye.
   
 20. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #20
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Dah! Mkuu umenitajia makole umenikumbusha mbali sana. Nakumbuka nilikuwa napaki mkoko wangu kama bubu pale CBE. Aisee!
   
Loading...