Kukatika tena daraja la Kiyegeya: Rais Magufuli afika Morogoro, awasimamisha kazi wahandisi 12. Awapa onyo la mwisho Mfugale, Kamwelwe

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,067
4,061
Wakuu,

Nipo nasikiliza hapa redio na imehabarisha kwamba kutokana na daraja la Kiyegeya linalounganisha kati ya Morogoro na Dodoma kusombwa tena na maji, mzee baba kaamua kwenda mwenyewe kujua mbivu na mbichi. Amenukuliwa akisema kwamba kwa wahusika wote wajihesabu hawana kazi na ameitaka TANROADS kuhakikisha hakuna barabara inayounganisha kati ya mkoa na mkoa,mji na mji ikisombwa na maji kwa namna yoyote.

Nitaendelea kusasisha kutokana na taarifa ninavyozipata.

Pia soma
Daraja linalounganisha Dodoma na Morogoro limevunjika, hakuna mawasiliano ya barabara
Kubomoka kwa daraja la Kiyegeya: Meneja Tanroads Morogoro arudishwa Wizarani
Mawasiliano kati ya Dodoma na Morogoro yamekatika tena

UPDATE
Rais Magufuli awasimamisha kazi wahandisi 12 wa TANROADS Morogoro na kuwapa onyo la mwisho Waziri wa Ujenzi Mhandisi Isack Kamwelwe, Mtendaji Mkuu TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale na Mkurugenzi wa matengenezo wa wakala huo kwa uzembe daraja la Kiegeya.
 
Wakuu,

Nipo nasikiliza hapa redio na imehabarisha kwamba kutokana na daraja la Kiyegeya linalounganisha kati ya Morogoro na Dodoma kusombwa tena na maji, mzee baba kaamua kwenda mwenyewe kujua mbivu na mbichi. Amenukuliwa akisema kwamba kwa wahusika wote wajihesabu hawana kazi na ameitaka TANROADS kuhakikisha hakuna barabara inayounganisha kati ya mkoa na mkoa,mji na mji ikisombwa na maji kwa namna yoyote.

Nitaendelea kusasisha kutokana na taarifa ninavyozipata.

Pia soma
Daraja linalounganisha Dodoma na Morogoro limevunjika, hakuna mawasiliano ya barabara
Kubomoka kwa daraja la Kiyegeya: Meneja Tanroads Morogoro arudishwa Wizarani
Mawasiliano kati ya Dodoma na Morogoro yamekatika tena

Stori hizo umeshawahi sikia kawahi tumbua wizara yake,hawezi mgusa Mfugale hio ni ndoto
 
Huu mfumo wa uongozi siyo mzuri, yaani ili kila kitu kifanyike ni lazima Rais ndiyo ashughulike!! Viongozi wahusika hawana nguvu, hawasikilizwi au hawana uwezo hii ni ajabu

Mbona PM alienda imeshindikana au, Rais atashughulikia mangapi nchi hii yote kama kila kitu ni lazima aseme

Huu mfumo ni vyema urekebishwe kila kiongozi atimize wajibu wake kikamilifu na hatua zichukuliwe kukiwa na uzembe
 
Daraja ndio limepewa kipaumbele, lakini maafa kama mafuriko, tetemeko na vimbunga yanayo ondoa maisha ya watu kwake hayana umuhimu kwenda.
Ziko dalili kuwa bado anahisi ni Waziri wa Ujenzi

Sent using Jamii Forums mobile app

hilo lipo wazi, lawana wapewe kina lodi rofa na jk kumuweka huyu mtu wizara moja miaka nenda rudi,
huyu alipaswa kuwa anabadilishwa wizara kila baada ya muda fulani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hajaenda kuwajulia hali akina Ester Bulaya na Halima Mdee waliovunjwa miguu na mikono?
 
Back
Top Bottom