Kukatika kwa Umeme na ukimya wa Maharagwe, Makamba na Rais Samia

UMeme unapokatwa kwenye ofisi za serikali, vyuoni na maeneo mengine ambapo kuna shughuli za kufanya kwa udharura. Akili ya kawaida inaniambia wahusika lazima wahamishie shughuli hizo hotelini kwa sababu maeneo yao hayapewi masurufu ya kujitosheleza kupata nishati ya umeme kwa njia ya jenerata au solar panels.

Hizo hoteli hazimilikiwi na serikali. Zinamilikiwa na watu binafsi na makampuni ya binafsi. Wamiliki hawa Sitaki mniulize wanauhusiano gani na baadhi ya viongozi! Jiongeze.

Hii ni dhania moja zipo nyingine nyingi!
Baadhi ya watu kuzuiwa kusema haikuwa bahati mbaya.

Hata hivyo bado naamini utaendelea kupigwa wakutosha baada ya rabsha ndogo ndogo kama hizi.
 
Kwa miezi takribani 4 sasa umeme umekuwa unakatwa kwa makusudi na watu wa Tanesco kwa kile kinachoitwa upungufu wa umeme nchini.

Tanzania inazalisha umeme toka vyanzo mbali mbali na moja ya chanzo ni umemewa maji ambapo kama mvua zipo nzuri hutupatia takribani 560MW .

Kwa miaka karibu 15 sasa Tanzania imekuwa inapitia kwenye mgawo wa umeme kutokana na uhaba wa mvua kutokana na madiriko ya Tabia nchi .

Tangu utawala wa JK .. kumekuwa na jitihada na makisudi za kupunguza athari ya mgao kutokana na kupungua kwa mvua.

Hata enzi ya Makufuli kulifanyika jitahada za makusudi kupunguza makali ya mgao wa umeme.

Lakini awamu hii chini ya Maharagwe - MD Tanesco, Makamba - Waziri wa Nishati na hata Mama Mh Samia -Rais .. Kila mtu yupo kimya kama kila kitu kiko sawa.

Mbaya Zaidi wananchi ndio wapo kimya zaidi kama vile kila kitu kiko sawa.

Naambiwa kwa week mbili zijazo hali ya kukatika kwa umeme itakuwa mbaya zaidi.

Wanatakiwa kutoka na kutuambia nini wanafanya kupunguza au kutatua hali hii.

Muona Mambo
Ukimya wao haumaanishi kuwa hakuna wanalolifanya kuhusiana na umeme.
 
Kuna uzi special wa Tanesco humu ndani ungeipeleka hii taarifa

Correction : Makufuli = Magufuli
 
Tatizo la umeme halielezeki,haka kamvua ka siku mbili tatu ndio kabisa,wale wateuliwa vijana wanatafuna maisha.
 
Wananchi tusilale, Mkwere, Mzanzibari na Makamba wanataka warudishe makampuni yao ya kifisadi, ili kuhujumu uchumi wetu
Warudishe mara ngapi? Wapo tayari, lazima kizazi hiki kikamuliwe kama ng'ombe.
 
Hapa ndipo hua namkubali master J wa bss huyu ni electrical engeeneer Tena toka uingereza vyuo vyahuko mama ake akiwa nibalozi wakudumi UN ,alichomoa katakata kufanya kaZi na serikali iliyomlea mama ake mzazi yaani mama yetu ,serikali ya ccm haitakagi wataalamu inaogopaga wataalamu hivyo inakwepa gharama au shida niwapi
 
Mliambiwa hata majina mnayowapa watoto muangalie maana zake maana kila unalokusudia kwa mtoto wako ndilo linatokea , sasa maharagwe na umeme wapi na wapi jamani, loh
 
Wananchi tusilale, Mkwere, Mzanzibari na Makamba wanataka warudishe makampuni yao ya kifisadi, ili kuhujumu uchumi wetu
Hii nchi imejaa wajinga sana, wataturudisha huko and there's nothing we can do, vyombo nchii vilitakiwa kulinda nchi na maslahi mapana ya taifa ila naona wameamua kuwaacha wanasiasa wafanye wanalotaka
 
Back
Top Bottom