ryana fan
JF-Expert Member
- Apr 27, 2018
- 2,632
- 3,051
Siyo 18b ni 19.51B........hii ndiyo Tanzania bhanaCAG ameweka wazi kuwa tatizo kubwa la kukatika katika kwa umeme limesababisha mkandarasi anayejenga bwawa la stigler's kudai bil 18 Kama fidia ya hasara aliyoingia kutokana na TANESCO waliompa kazi kumkatia Katia umeme hivyo,
kukatwa katwa huko kwa umeme pia kumesababisha mradi kuchelewa pakubwa.
Hoja yangu ipo hapa, Kama hayo makampuni yanalipwa feza nyingi kutokana na madhila ya kukatika umeme je cc Wananchi ambao ndo tumeathirika pakubwa mno na mkatiko huo wa umeme ikiwemo, samaki kuoza, vifaa vya umeme kuungua, kulipa Kodi huku tunashindwa kuzalisha, kusimama uzalishaji. Na mengine mengi tu.
Nakuomba serikali Kama mtapampa mgeni posho ya bembelezo au athari za kukatika umeme na sisi Wananchi tunataka hiyo penalti mtulipe kwakushindwa kutupa umeme Kama mkataba baina yetu Kama wateja na TANESCO unavyotaka.
Lazma mtulipe, mabeberu mnawalipa hasara zao sisi je