Kukatia maji JWTZ tuone fahari au wazimu?

YournameisMINE

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
2,256
1,225
wewe una amini kama ni kweli ilikuwa misunderstanding?? dawasa wamebanwa "korodani" wameamua kukubali yaishe!! halafu siku kampuni ikifa, wewe ndio utakuwa wa kwanza kupiga makelele.
 

Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,817
0
ni upuuzi, jeshi linakatiwa maji linaenda kupiga wafanyakazi wa dawasa!
haingii akilini kabisa, kuwa hao ndio tuliowapa dhamana ya usalama wetu, watu wenye kututisha sisi wenyewe. naona wamesahau kuwa ujeshi ni kazi kama nyengine.

unafikiri kulikuwa na misunderstanging? my take, dawasa imelazimishwa kufungua maji na serikali, isitoshe baada kupigwa na majeshi kwa wafanyakazi wake, hata ungekuwa wewe mkubwa wa dawasa ungesema na wafunguliwe maji.
 

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
684
0
ni upuuzi, jeshi linakatiwa maji linaenda kupiga wafanyakazi wa dawasa!
haingii akilini kabisa, kuwa hao ndio tuliowapa dhamana ya usalama wetu, watu wenye kututisha sisi wenyewe. naona wamesahau kuwa ujeshi ni kazi kama nyengine.

unafikiri kulikuwa na misunderstanging? my take, dawasa imelazimishwa kufungua maji na serikali, isitoshe baada kupigwa na majeshi kwa wafanyakazi wake, hata ungekuwa wewe mkubwa wa dawasa ungesema na wafunguliwe maji.

Naamini kuwa DAWASA hawakwenda kukata maji tuu hivi hivi. Ukisikiliza maelezo ya yule afisa ni kuwa wameandika barua nyingi kukumbushia deni lao lakini Jeshi walipuuza na kudharau.

Kitendo cha wanajeshi kupiga wananchi ni cha kulaaniwa Mwkjj. Hakuna kazi ambayo haina unyeti wake. Hata wafagiaji wa jiji wana umuhimu wao kama jeshi lilivyo is just division of labor.

Hivi leo DAWASCO wakishindwa kujiendesha nani alaumiwe? maana wakishindwa kujiendesha ni kuwa hata huko Jeshini kutakuwa hamna maji. Unategemea kama indekuwa ni kampuni binafsi Jeshi wasingelipa? Najua jeshi wana budget yao ya kujiendesha ambayo inalipa maji, simu etc. Inakuwaje waweze jaza mafuta kwenye magari yao na washindwe kulipa maji?

Hawa wanajeshi wetu bado wana ulimbukeni wa kubebwa, wakisha amka na kwenda kufyeka kidogo they call it siku. Nadhani Jeshi kwanza linataakiwa liwe jeshi la kujenga uchumi kwa sasa maana ni mzigo. Wafanye kazi za engenering, utafiti, construction, etc na sio kuja kupiga wananchi.
 

Pundit

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
3,738
1,225
It is sad to see brutal force and barbaric bullyism prevails over reason and economic common sense.The armed forces are supposed to serve Tanzanians, not bully our service providers with their mighty force.

Nobody is above the law, the due procedures must be followed.This business of hooliganism must be condemned whether the perpetrator is a John Doe or the Chief of Staff.Wrong is wrong, army or no army.
 

Code X

Member
Feb 18, 2008
30
0
I hate to burst your bubble... DAWASA wamewarudishia maji JWTZ.. ilikuwa ni "misunderstanding"...

Mkuu,

Bajeti ya serikali kwa ajili ya jeshi kulipa maji nchi nzima ni sh 1.2 billion. DAWASA, kati yahizo wamelipwa sh milioni 690. Zilizobaki zikapelekwa mikoani kwa ajili ya kulipia maji kule.

Kwa hali ya uchumi wetu, na misingi ya kibiashara, sitarajii kama DAWASCO watakosa kuwakopesha wateja wao.

Wana JF wengi naona wamekuwa wakijadili hili suala kwa kuacha uhalisia wa tatizo lenyewe, na kuanza kushambulia jeshi. Bila shaka, kitendo cha kuwapiga raia ni cha utovu wa nidhamu na sikitetei, lakini nasi tuangalie kwa makini motives za DAWASA kukata maji kwa mteja ambaye aliwahi kulipa milioni 690 miezi miwili iliyopita, na sasa amebakiza hizo.

Nahisi kuna zaidi ya tunalolifahamu juu ya mzozo huu, na siku si nyingi tutaujua ukweli.
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
6,297
2,000
Nadhani hatukumtendea haki aliyeleta mada hii kwa kuona kuwa anawatetea JWTZ kwa fujo walizofanya. Tatizo la haya mashirika yetu ya huduma bado hayajatambua umuhimu wa mteja. Wao wanachojua ni kutuma barua halafu kukata huduma. Wanaona it is beneath them kujaribu kuwasiliana na mteja. Tunakumbuka wote saga ya Tanga cement na Tanesco. Tanga Cement walijaribu kuwasiliana na mkubwa Tanesco ili kutatua ishu yenyewe juu ya meza wakakataliwa na kukaziwa uzi kuwa walipe tuu! Huyu alikuwa ni mteja anayemlipa Tanesco mamia ya mamilioni kwa mwezi lakini wakubwa hawakuona tatizo kumkatia kwa deni (alilokuwa akipinga uhalali wake) la milioni chini ya hamsini! Kwa hawa Dawasco, bila shaka JWTZ ni wateja wakubwa na wanastahili heshima. Mbali ya mawasiliano ya barua walijaribu kuwaona wakubwa wahusika ikashindikana? Kwa wenzetu, mashirika haya yangekuwa na mawasiliano ya karibu na wateja wao wakubwa ili kuhakikisha hawawapotezi. Sasa hao wanajeshi wakifuata ushauri wa wengi, wakachimba visima na kujitoa kwenye network ya Dawasco watamlilia nani? Kwa nini hawaigi wenzao wa TRA ambao wamewafungulia kituo wateja wao wakubwa! Wakati umefika hawa wenzetu watambue kuwa monopoly yao haina muda mrefu itakwisha. Hapo ndipo watajua kama kweli wanapendwa au la! Kwa wenzetu hata mteja mdogo ukikwama shirika linakuwa tayari kujadili na wewe namna utakavyoweza kulipa deni bila kuathirika sana. Kukata huduma ni hatua ya mwisho.
 

YournameisMINE

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
2,256
1,225
jaribu kuniwazia nini nitafanya!!

kila kitu kwako wewe ni mashindano!!!!! hili suala ni la kulipa bills, sasa kama wewe unaona vinginevyo haya.................sina haja ya kufikiria kwa niaba yako, kwani umesahau kuwa wewe ni "Genius/Nyerere" wa JF??!!!...........JWTZ wawe wanapata huduma zooooooooooote bure, kwasababu wao ni wanajeshi.!!!!!!
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,179
2,000
kila kitu kwako wewe ni mashindano!!!!! hili suala ni la kulipa bills, sasa kama wewe unaona vinginevyo haya.................sina haja ya kufikiria kwa niaba yako, kwani umesahau kuwa wewe ni "Genius/Nyerere" wa JF??!!!...........JWTZ wawe wanapata huduma zooooooooooote bure, kwasababu wao ni wanajeshi.!!!!!!

endelea kunipachika vyeo unavyofikiri ninavyo na hilo la JWTZ kupata huduma bure ndiyo inaitwa stretching an argument to absurdity! ... but then, that is you it seems unajua sana nini nafikiria, na nini nitafanya. So kati ya mimi na wewe, it seems wewe ni "the all knowing" being..!
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
6,297
2,000
kila kitu kwako wewe ni mashindano!!!!! hili suala ni la kulipa bills, sasa kama wewe unaona vinginevyo haya.................sina haja ya kufikiria kwa niaba yako, kwani umesahau kuwa wewe ni "Genius/Nyerere" wa JF??!!!...........JWTZ wawe wanapata huduma zooooooooooote bure, kwasababu wao ni wanajeshi.!!!!!!

Mkuu, kweli kulikuwa na haja ya ku'personalise' ishu hii? Imeshindikana kweli kushindana kwa hoja ili sisi wengine tuelimishwe?
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,528
2,000
Sometimes nafikiri humu ndani tunakosa kuwa na busara katika kufikiri na kuangalia na kupima mambo.

Ndio ni lazima kila mteja na mtumiaji alipie ada au deni! Lakini busara inahitajika sana katika baadhi ya mambo yanayofanyika. Wengine mmesema mtaelewa kuwa Muhimbili can be an exception maana kuna uhai. je jeshini si wana hospitali pale Lugalo? Je ikiwa Jeshi wangekuwa na kiwanda cha kutengenezea silaha kali na maji ndio kutumika kupoozea mchakato mzima na Dawasco kuwakatia maji kabla ya vyuma kupoa na kutokea mlipuko mngesema Dawasco was right?

Jeshi, Polisi Uhamiaji, uwanja wa ndege, Bandari magereza na taasisi nyingine pamoja na kuwa zinalazimika kulipia madeni yao, lakini panahitajika busara kufanya kazi ya ukusanyaji madeni na si papara za kijinga zilizoonyeshwa na Dawasco.

That was extremely dangerous to cut the water supply to army. I repeat extremely dangerous!

Leo tunadai eti jeshi limejenga shule ngapi au zahanati, is it their responsibility? Wengine wenu hapa mlipigia bango ile mada ya JKT sasa mnataka JWTZ ijenge shule?

We need to use wisdom on some of things we do however unsound some descicions can be. Leo Wanajeshi wangeamua kusema enough is enough ka kugeuza kibao kwa kupindua nchi maana wamechoka uozo na uzembe wa Serikali would we have been chanting JWTZ hoyee?

People need to think deeply and not rush into this "moral" talk without wisdom!
 

YournameisMINE

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
2,256
1,225
Mkuu, kweli kulikuwa na haja ya ku'personalise' ishu hii? Imeshindikana kweli kushindana kwa hoja ili sisi wengine tuelimishwe?

wewe kwani ni msemaji wa mkjj? angalia hiyo post nilomjibu hapo juu, kisha sema usemavyo kwa kuni-point mimi!!! usichukue sides kwa ushabiki tu uncle!!.
kwanza I don't care much kuhusu nini kinafanyika in TZ.....ila hii issue ni common sense, and I was trying to point tht out!! ndugu yako yeye anashindana, anasema, "HATUOMBI KIBALI, USHINDI NI LAZIMA." is it about winning or doing the right thing!!?? kaaaaazi kweli.
 

YournameisMINE

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
2,256
1,225
No payments, no services, no exceptions..........kinyume cha hapo ni UFISADI!!! anaye kubali akubali na anayebisha shauri lake, ukweli ni kwamba dunia nzima ndio mambo yanavyoendeshwa!!! hamna cha busara hapa, busara ni kulipa bills on due date....hivi uswahili huu mnaoufagilia utaisha lini?? kwahiyo wao JWTZ baada ya kukatiwa umeme, kitendo chao cha kupiga watu kilikuwa ni cha busara?? halafu wamekuwa rewarded kwa kurudishiwa maji bila malipo.....eti misunderstanding, halafu mtu huyo huyo kila siku hapa anajifanya anapenda TZ na mabadiliko for good!! yatatoka wapi kama watu wanashindwa kuwajibika, halafu wewe huyo huyo unashabikia udekezwaji wao!!! You must be insane!!.
 

Bin Maryam

JF-Expert Member
Oct 22, 2007
685
0
Bajeti ya serikali kwa wizara zake inajumlisha matumizi ya maji na umeme. Matengenezo ya majumba na vitu vingine.

Ndio JWTZ ni walinzi wa nchi na priorities zao zipo juu kuliko taasisi zingine. Lakini muhimu wa priorities zao ni lazima uonyeshwe katika matumizi yao ya pesa.

Ni matumizi mazuri ya pesa yanayofanya waweze kununua rada za kisasa. Ni matumizi yao mazuri pesa yatakayofanya wawe na hospitali nzuri.

Ni mambo ya kizamani ya kuliachia jeshi kutumia bila kuwajibika kwa madai ya kuwa wao ni walinzi.
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,528
2,000
Pick your battles! It was un necessary for Dawasco to storm Jeshi ground to cut off the water supply period! same with the way they have been cutting mabomba ya watu!
 

YournameisMINE

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
2,256
1,225
Pick your battles! It was un necessary for Dawasco to storm Jeshi ground to cut off the water supply period! same with the way they have been cutting mabomba ya watu!

tatizo la wanasiasa!! wewe unaangalia suala hili kisiasa.....mimi/sisi tunaangalia ktk angle ya common sense na business. common sense hapa ni kwamba unalipa bills kama itakiwavyo(hakuna stories), huo ulikuwa wajibu wa JWTZ. Kiabiashara ni kuwa, yes ninyi ni JWTZ, ni ndugu zetu na walinzi wetu...lakini biashara hii ya maji hailijui hilo!!!! Pesa mbele, hakuna pesa, hakuna huduma!!.
 

Koba

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
6,137
1,500
Rev Kishoka naona kwenye hii issue umechemsha ile mbaya,nadhani unataka DAWASCO ife na mji mzima ukose maji labda utafikiria tena unachotetea.
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
6,297
2,000
tatizo la wanasiasa!! wewe unaangalia suala hili kisiasa.....mimi/sisi tunaangalia ktk angle ya common sense na business. common sense hapa ni kwamba unalipa bills kama itakiwavyo(hakuna stories), huo ulikuwa wajibu wa JWTZ. Kiabiashara ni kuwa, yes ninyi ni JWTZ, ni ndugu zetu na walinzi wetu...lakini biashara hii ya maji hailijui hilo!!!! Pesa mbele, hakuna pesa, hakuna huduma!!.

Mkuu, sina ubavu wa kumsemea Mzee Mwanakijiji. Tatizo la kuingiza uhasama wa binafsi kwenye mada, mtatuboa wengine. Yeye kujiona Genius/Nyerere wa JF kunahusiana nini na mada hii?

With all due respect, nyinyi ndio hamna mtazamo wa kibiashara. Haya mambo ya kutishana, kukatiana huduma yote ni mazao ya monopolies zilizotokana na siasa yetu. Umesikia wapi ambako mteja mkubwa anatendewa hivi? Wameshindwa hata kwenda kuonana nao na kulitatua tatizo? Kwa wenzetu mabepari, mteja ni mfalme. Mteja mkubwa ndiyo basi. Kama nilivyosema, kibishara, kukata huduma ni hatua ya mwisho. Sasa hawa wafanyabiashara walifanya jitihada gani za kuwasiliana na mteja zaidi ya barua? Mteja anayetumia maji ya karibu bilioni moja ni wa kumlea na si kumdhalilisha. Ndio biashara na si siasa. Biashara unayozungumzia ni ya daladala.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom