Kukatia maji JWTZ tuone fahari au wazimu?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,742
40,873
Hivi tuna akili timamu au ndio kufikiri tunaweza sana? Hivi wanaweza kuikatia maji Ikulu? Hivi serikali yetu tukutu/fu imeshindwa kupata "tu"shilingi milioni 276 mahali "fulani" wakati waliweza kushindanda kupata milioni 400 kwa ajili ya Taifa Stars?

mimi nasema wazimu wa daraja la kwanza, kuna mtu hajakaa chini kufikiri. Yaani Mwandosya, Mwinyi, Mwamunyange wameshindwa kukaa chini na kumaliza hili? Laana nyingine ni za kujitakia!!
 
Mwanakijiji,

Hii inaonyesha wazi ni jinsi gani Serikali yetu ilivyo mbovu na kujkanyaga kama si wazembe wa makusudi na kupotoka. Hivi leo twawakatia maji, je ilikuwa ni shida gani kwa Mwandosya kumpigia simu Hussein Mwinyi au Nchimbi akawaambia walipie maji?

Jee ofisi ya Rais au Waziri Mkuu zikichelewa kulipia maji, Ikulu itakatiwa maji?

Matatizo mengine tunajitakia bila kuwa makini kufikiri. Jeshi limekaa kimya huku Serikali ikiwa wazembe na kutafuna Richmond, Buzwagi na BOT EPA, leo mwaenda wakatia maji?

Are we looking for mutiny or coup?

Talk about disfunctional and disorganized goverment!
 
kuna wakati yule mtu aliyegundua DNA aliwahi kusema maneno hapa watu wakamsakama kuwa ni mbaguzi,wakati mwingine mie naungana naye kabisa. Tumetumia Miliion 500 kwenye sherehe za miaka 46 ya uhuru eti kuyafanya maadhimisho hayo kuwa ya kihistoria,huu ni wenda wazimu. Halafu leo watu wanatunisha misuli kwanini tunakatiwa maji sisi watu wa taasisi nyeti? huu ni ukichaa mwingine,hakuna aliyejuu ya sheria,huduma inayotolewa lazima ilipiwe na kila mtu,ukisema mimi mjeshi lazima nilipiwe na sisi madaktari tukidai haki zetu tutafika wapi. Kila mtu atimize wajibu wake
 
Mkuu mwanakijiji hapa ndio linapokuja tatizo ambalo tunasema Tanzania hatuna priorities. Kama tunaprioty ya kuzungusha mawaziri wote nchi nzima sijui walitumia kiasi gani cha pesa na kushindwa kulipa huduma ya maji si ni uenda wazimu? priority is needed, yet priority criteria not likely to be much important but sequencing may be more important. Hili ndilo tatizo kubwa letu.

Hivi hili sirika lijiendeshe je kama serikali haitaki kulipa? kama jeshi hawataki kulipa? Hivi ingekuwa ni private company unavamia na kupia wafanyakazi wake ingekuwa je? wafanyakazi wenyewe nadhani hata insuarence hawana. Huu upuuzi ndio uliifikisha Tanesco hapo ilipo sasa. Ndio maana mashirika mengi yalikufa.

Unajua wanajeshe wanajifanyaga wako juu ya sheria sana na hii inasababishwa na umbumbu wao. Unakuta mwanajeshi anayelipwa mshahara hataki kulipa nauli lakini mwanafunzi wa chekechea analiapa. Jamani inatubidi tubadilike sasa kila mtu anaumuhimu wake, madakitari wanaumuhimu wao, mabar maid wanaumuhimu wao na madereva daladala wanaumuhimu wao hakua aliye bora zaidi. Huo nii mgawanyiko tu wa kazi. Mwanakijiji hivi ingekuwa wewe ndio wale waandishi wa habari halafu unapatiwa kichapo au wale wafanyakazi walipigwa na kudhalilishwa mbele za familia zao ungefanya je? Nadhani jamaa waliohusika wanatakiwa wawajibishwe iwe fundisho kwa wengine maana wanajeshi wamezidi kuonea raia.
 
Serikali ya SISEMU wamenatuona sisi wananchi wajinga na sasa wameanza kuvuka mipaka na kuwaona wanajeshi pia ni wajinga wa kuja na pengine hawana shukurani.
Kwa vile wao SISIEMU wana fedha nyingi sana mifukoni mwao wanaona kwamba Jeshi lipo kwa sababu wao SISIEMU wapo,
Na si kwamba SISIEMU ipo kwa sababu jeshi lipo na linawalinda.

Uzuri wa kuikumbatia rushwa na ufisadi ni kwamba unasahau hata watu muhimu na sehemu muhimu za kuzipa kipa umbele.

Nadhni zoezi la kukatia maji wanajeshi ni zoezi zuri tu, wanajaribu kuwaonyesha wao SISIEMU na JWTZ nani zaidi. Tena wasiishie hapo JWTZ tu nadhani ni vema waende hata ukonga nako wawakatie maji FFU ili tujue kwamba wamepania kwa dhati kukusaja madeni ya wadaiwa sugu bila kujali umuhimu wao.

Wamesha sahau kabisaa kwamba kuna wakati ilibidi Makepteni wa JWTZ wawatulize kwa mikopo ya Hyundai??

Kwa vile umuhimu wao unazidi kushuka kwa sababu SISIEMU sasa wana fedha hawawahitaji wanajeshi ni bora wawaonyeshe kwa kuwakatia maji???

Shuguli hiini pevu.
 
Sherehe za aina yake wakati kila siku watoto wqanakufa na malaria na taasisi za srrikali zina madeni kibao ya umeme , maji na simu ?
 
Hivi hiyo bajeti inayopitishwa kila mwaka haijumuishi matumizi kama haya? Kama pesa zinatengwa kwa ajili ya kulipia maji na huduma nyingine, kwa nini hazitumiwi inavyopaswa? Na kama ni hivyo, hao auditors wanafanya nini? Swali lingine, ni kweli hiyo huduma wanaipata inavyopaswa? Au ndiyo mambo ya mgao tena? Haya ni matokeo ya kuendekeza uzembe!
 
Tumekuwa wendawazimu mno, hatuna priority. vipaumbele kwetu ni vitu kama sherehe, warsha na mikutano ya ulaji. hii inatisha sana, inadhihirisha ni kwa jinsigani serikalini wa hawana utaratibu wa kufanya kazi, kila kiongozi anahamua chake kwa muda anaopenda yeye.Na kwa kuwa hatuna vipaumbele, siogaopi kusema hata jeshi inawezekana ktk bajeti yao waliyotenewa, pesa wameandalia warsha na vikao vya ulaji, huku wakiipa mgongo vitu kama bill ya maji, umeme na kadhalika. Bongo imekuwa ya kuchota, kila mtu anaangalia kitambi chake tu, tunakurupuka sana,tumepoza kabisa uwezo wa kufikiri. jeshi wanatumia silaha zetu kutunyanyasa, viongozi tuliowachagua wanatumia madaraka tuliyowapa kutuwahisha kwenda kaburini hata kabla ya muda aliyotupangia Mola haijatimia,wanajichotea pesa zetu, tena kwa ubabe huku tukiwaona.Nikiifikiria sana nchi yangu najihisi kama vile nimekuwa mfu, mbele giza tupu tena sana.Tanzania tumekuwa wanafiki sana, hatuna viongozi. HAKIKA TUMEKUWA WENDAWAZIMU!!!!!!
 
Kuna ishu mbili hapa.
  1. Serikali haioni umuhimu wa jeshi kuwa na maji na pia DAWASA/DAWASCO kuweza kujiendesha. Katika hili siku nikisikia Ikulu wamekatiwa maji kwa kutokulipa bili (au kutokufanya mawasiano kwa wakati muafaka), sitawaona watoa huduma ya maji ni wabaya, ila hapo wasiojua wajibu wao ni hao Ikulu. Kwa sasa naona jeshi (serikali?) haijui wajibu wake.
  2. Kuna ishu ya uelewa wa wanajeshi wetu kuhusu masuala mbalimbali (jeshi sio vita peke yake). Kwa mfano binadamu akigongwa na gari, itakua ni kitu cha ajabu sana gari likiadhibiwa badala ya dereva au mwingine aliyehusika na ajali hiyo. Wanajeshi wetu wana upungufu mkubwa sana wa uelewa wa taratibu na sheria ambazo ndizo zimeunda jeshi lenyewe!
 
DAWASA deserv salute for that, if they can't pay their bills then they don't diserv to have a service. That is the way to go.

Leo hii DAWASA wakitaka kwenda kusecure loan kutoka kwenye financial institution chakwanza watu wanakwenda kuangalia Balance Sheet yako, then wana fanya uses and source of fund analysis, imagine wewe banker unaona big number ya account receivable, lakini days za kulipa kwenye A/R payout ratio inaonyesha more than 12 month, you cant give them any loan. Then madhara yake ni kwamba they can't invest in big projects, they can't hire more people, they cant produce in efficenct way.

Good Job DAWASA
So, kama mdaiwa mkubwa ni serikali, DAWASA inatakiwa kukata maji pasipo kuangalia rangi wala sura.
 
Kama Jeshi hawalipi maji wakatiwe, kama ikulu hawalipi maji ni haki yao wakatie. Kwani hao DAWASCO watajiendeshaje? Yeyote ambaye hayuko tayari kulipa tena jamaa waliwapa muda wakulipa deni hawakulipa basi wakikatiwa ni sawa. Nawapongeza DAWASCO na hao wanajeshe walitakiwa wachukuliwe hatua. Kama ingekuwa private company wasingelipa? waache nao wakatiwe next time watalipa na uhakika kwenye budget yao wanapewa.
 
Tatizo 'watu' bado tupo kwenye transition ya F(R)EE kwenda kwenye FEE.

Ili kuwakumbusha wadau wote ikiwa pamoja na mawaziri na wanajeshi kuwa ile era ya free haipo na sasa tupo kwenye kipindi cha 'Fees for services', action kama hizo ni muhimu.

Hongera DAWASCO kwa hiyo action ya kukatia watu maji, lakini na nyie mtoe huduma halali kwa malipo mnayopokea. Sio mambo ya estimates, maji yanatoka mara nne kwa mwezi tena usiku wa manane kwa dk 30 halafu unatakiwa ulipe bill ya mwezi eg Tsh 15,000.
 
Ni haki ya maafande wetu kuwa na huduma ya maji kama ilivyo kwa wananchi wa kawaida. Ni wajibu wa maafande kulipia maji hayo, kama zilivyo huduma nyingine za jamii ambazo wanapaswa kuzilipia. Binafsi naona DAWASCO wamefanya kazi yao inavyostahili, kwa hiyo kitendo cha maafande hao kuwashushia kipigo watumishi hao kwa kutekeleza wajibu wao ni uharamia kama ilivyo kwa uharamia mwingine wowote ule, na ni haki kuwapatiliza maafande hao maharamia.
Siafiki kabisa uonevu wa maafande.
 
DAWASA deserv salute for that, if they can't pay their bills then they don't diserv to have a service. That is the way to go.

Leo hii DAWASA wakitaka kwenda kusecure loan kutoka kwenye financial institution chakwanza watu wanakwenda kuangalia Balance Sheet yako, then wana fanya uses and source of fund analysis, imagine wewe banker unaona big number ya account receivable, lakini days za kulipa kwenye A/R payout ratio inaonyesha more than 12 month, you cant give them any loan. Then madhara yake ni kwamba they can't invest in big projects, they can't hire more people, they cant produce in efficenct way.

Good Job DAWASA
So, kama mdaiwa mkubwa ni serikali, DAWASA inatakiwa kukata maji pasipo kuangalia rangi wala sura.

They could have done it more diplomatically though, maana when you mess with those guys, you play with our National Security. Also wanasahau kuwa in order for Dawasco to request money for expenditures and stuff it has to go through the cabinet kabla ya kwenda bungeni, sasa kama wanawasumbua watu wa ulinzi, si Mwinyi anaweza kugoma kidogo kule...this should have been handled more diplomatically. Dawasco wangemuambia Prof kwanza, "Mzee ongea na Mwinyi maana wale jamaa wanatuchezea..."

Ila naamini kwamba fujo zilifanywa na watu wa chini ambao hawakutumwa na mtu na watashughulikiwa.

Kuhusu kupatikana Milioni 400 za mpira, hiyo si order ya bwana mkubwa ambaye anavalue mpira na mbwebwe kuliko basic huduma kwa wananchi. Seikali kutoa hela kwa huduma ni process ngumu sana, ila nenda ukaombe pesa za mradi fixi and you promise an official a commission, uone utapata pesa gani.
 
They could have done it more diplomatically though, maana when you mess with those guys, you play with our National Security

...diplomatically my a$$$...walipe bill au hakuna maji na hiyo national security ife tuu tutaunda nyingine inayoweza kulipa bill za maji sio hii ya kupiga watu wanaofanya kazi zao.
 
Hii ndio inaonyesha upuuzi wa utendaji wetu Tanzania. Hatuna ujanja turudishe wakoloni waje watutawale tena, na sasa tuwaombe waje kututawala kama tufanyavyo tunapowaomba kuja kuwekeza. Ndio, hatuwezi.
 
kuna wakati yule mtu aliyegundua DNA aliwahi kusema maneno hapa watu wakamsakama kuwa ni mbaguzi,wakati mwingine mie naungana naye kabisa. Tumetumia Miliion 500 kwenye sherehe za miaka 46 ya uhuru eti kuyafanya maadhimisho hayo kuwa ya kihistoria,huu ni wenda wazimu. Halafu leo watu wanatunisha misuli kwanini tunakatiwa maji sisi watu wa taasisi nyeti? huu ni ukichaa mwingine,hakuna aliyejuu ya sheria,huduma inayotolewa lazima ilipiwe na kila mtu,ukisema mimi mjeshi lazima nilipiwe na sisi madaktari tukidai haki zetu tutafika wapi. Kila mtu atimize wajibu wake

Nafikiri ndo tafsiri ya maisha bora kwa kila mtanzania kwa siku moja sababu haiingii akilini serikali kukosa vipaumbele vya maendeleo.
 
Kuna taarifa zinasema Edo amefanya hujuma ya jeshi kukatiwa maji ili serikali ifedheheke. Hakuna connection ya maana zaidi inayotolewa kama ushahidi wa hizi shutuma zaidi ya yafuatayo:

1. Edo anawatumia Kaaya na Badra kupitishia ajenda yake hiyo.

2. Ingawa Allocation ya fedha za jeshi kwa malipo ya maji hazitoshi, lakini jeshi limekuwa likilipia maji fedha zote zinazopatikana.

3. Hadi maji yanakatwa, jeshi halikuwa linadaiwa kiasi cha fedha cha kutisha hadi maji yakatwe.

4. Tukio la kukatwa maji limewafedhehesha sana viongozi wa jeshi

5. Ilikuwa ni makusudi yasiyo lazima Kaaya kuambatana na press kwenda kukata maji, kwa kutimiza lengo la ku create bad public image and potray governance failure.

Sina hakika sana na haya, lakini ni kutoka vyanzo vya kuaminika, na naomba tusaidiane kuyaangalia kwa undani.
 
Hivi wakati Jeshi wamekatiwa maji, halafu mkasikia kuna uvamizi wa nchi sehemu za Mashariki au kuna bomu limelipuka katikati ya jiji la Dar.. wangewarudishia hayo maji au wangetaka walipe kwanza?

Hivi nadharia ya "military readiness" imeanza kuondolewa Tanzania lini? Ingawa watu wote wenye madeni wanatakiwa wawe wamelipia hilo ni kweli lakini kuna vyombo ambavyo havitakiwi kuwa na madeni ya vitu muhimu kama umeme, maji, na simu. Hivi Muhimbili wakatiwe maji kwa sababu ya DAWASA wanakusanya bili zao, na watu wakafa au mlipuko wa magonjwa ukatokea kweli tutasema "Hongera Dawasa"?

Aliyefanya uamuzi wa kulikatia jeshi maji siyo tu kafanya uamuzi wa kipumbavu (and I mean "pumbavu") ambao siyo tu ni wahatari lakini uliolenga kulidhalilisha Jeshi mbele ya wananchi na kuliumbua na hivyo kuwapa faida maadui wetu. Na ninaweze kwenda mbali zaidi na kusema kuwa kitendo hicho kisipokemewa mara moja kinapakana na usaliti.

Kwa sisi ambao tumekulia ndani ya jeshi hilo (kwenye kambi ya Kikosi cha Chuo cha Ulinzi wa Anga kule Tanga) na baadaye kikosi cha Rada nje ya Dodoma najikuta sina jinsi bali kukiri kufedheheka na kuchukizwa na kitendo hicho cha DAWASA ambacho hakikuwa na ulazima wowote wala sababu ya kufanyika.

DAWASA kwa hili wakemewe.

That said; Serikali isisabishe madeni haya ya kijinga kwa JWTZ. Ushauri wangu ni rahisi; Jeshi linajua kwa wastani linatumia kiasi gani kulipia maji na umeme kwa mwezi. Sasa, waandike cheki ya kulipia miezi yote iliyosalia na ukifika mwisho wa mwaka, kiasi chochote kilichozidi DAWASA wakirudishe au kicarry over na hivyo kuondokana na ulazima huu wa kulipia maji au umeme kila mwezi. Kama hawawezi kulipia kwa miezi iliyosalia, walipia a month in advance. Hivi ndivyo wengine tunafanya na vibili vyetu vya hapa kijijini.
 
Back
Top Bottom