Kukataliwa na kudharaulika kunavyoweza kumfanya mtu mwema akawa mtu mbaya

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,678
106,786
“A famous man once said We create our own Demons”
- Tony-stark (Iron man 3)

Wasomi wenye uelewe wa juu jinsi akili ya mwanadamu inavyofanya kazi (psychologist) wanasema kua mambo yote ambayo tunaona yanatisha maishani mwetu hua tunayatengezea vichwani mwetu, mfano unatembea usiku ukawa unaona uoga mara unahisi labda kitu kama kuna kitu kinakufuata kwa nyuma hua ni mambo ambayo tunayajenga kichwani sio halisi.Pengine upo ndani peke yako unaogopa hadi nguo ulizotundika ukutani unana kama vile ni mtu anakuangalia. Simply wanasema uoga/Hofu inaanza kutengenezwa vichwani mwetu, hvyo basi wanasema kua “We create our own Demon”.

Lakini pia hio sentensi ya We create our own demons ina maana kubwa katika maisha yetu ya kila siku, Mara nyingi tumekua tukitengeneza demons wengi maishani mwetu kutokana na matendo yetu ambao wanakuja kutu-haunt.
Namaanisha kwamba kutokana na matendo au maneno yetu ya kila siku bila kutegemea tumejikuta tukijitengezea maadui (Demons) wetu sisi wenyewe. Wahenga wanasema ni rahisi kumbadilisha mtu mwema akawa mtu mbaya zaidi kuliko kumbadilisha mtu mbaya kua mtu mwema, na ukimbadilisha mtu mwema akawa mtu mbaya ni ngumu san asana kumrudisha kua mtu mwema..Ukiinyambulisha hio sentesi ndio utapata ule semo kua there is a thin line between Love and Hate, hivyo ni rahisi sana mtu anayekupenda sana kumbadilisha akawa amekuchukia sana. Ni rrahisi sana mtu mwema ukamfanya akawa mtu mbaya.

Isaya 53: Alidharauliwa na kukataliwa na watu, mtu wa huzuni nyingi,ajuaye sikitiko; na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao,Alidharauliwa wala hatukumhesabu kitu

How do we make our Own Demons?

Ni kwanamna gani tunaweza kuwafanya watu wanaopenda kutenda mema kuwa wabaya au kuwafanya watu wanaotupenda sana wakawa wanatuchukia sana ? Dissapointment, yes kukatishana tama! Kumkatisha tamaa kwa maneno au matendo mtu anayekupenda au aliyetamani kufanya matendo mema ndio kunaweza kufanya watu hao wakabadilika na kua watu wabaya au wakatuchukia. Nitaelezea mifano michache

Kisa #1.
Mnamo mwaka 480BC mfalme wa Persia aitwae King Xerxes I alikua amepanga kuuvamia moja ya mji wa ugiriki uitwao Sparata ambao ulikua unatawaliwa na mfalme Leonidas, kipindi hicho Ugiriki ilikua kila mkoa unajitawala kivyake. Mfalme Leonidas alikusanya wanajeshi wake 300 tu kwenda vitani kupambana katika eneo liitwalo hotgate. Kulikua kuna mtu anaitwa Ephialtes huyu jamaa alikua anaulemavu wa kibyongo, alimfata mfalme Leonidas akamuomba ampe nafasi akajiunge jeshi aende vitani kupigana na wapersia ili kulipa kisasi cha baba yake. Kutokana na jinsi alivyokua mlemavu Mfalme Leonidas alimuonea huruma akamwambia hataweza kupambana, maana ili uende vitani inatakiwa uweze kushika ngao na mkuki uweze kujilinda wewe na kumlinda mwenzako mkiwa mnapambana.
Yule mlemavu alichukia sana kwa kukataliwa kutokana na ulemavu wake, alichoamua kufanya alienda kwa mfalme wa Persia akawapa mbinu za jinsi ya kuwazingila Leonidas na jeshi lake. Kilichotokea Leonidas na wanajeshi wake 300 walichinjwa wote kama kuku.( Mwaka uliofuata wa Persia walipigwa vibaya mno na mfale Themistocles kutoka Athens..Nishawahi andika uzi kuhusu hii vita)

Kisa #2
Mtu mmoja alikua anategemewa na watu wa eneo Fulani kutokana na msaada wa kupambana na watu waliokuja kupora mali za watu, muda mwingine alikua anawagawia chakula watu wa eneo hilo. Palitokea kijana mmoja akawa anampemda sana Yule mtu anayetoa msaada, siku zote alikua anatamani awe kama yeye. Mara nyingi alipokua akipambana na wezi waliokuja kuiba Yule kijana alikuja kumsaidia, muda mwingine alikua anamwomba kua aungane nae awe anamsaidia kufanya mambo yake ya kusaidia watu ila Yule mtu alimkatalia Yule kijana kabisa, anamwambia hawezi. Mwisho Yule kijana alikuja kua adui namba moja wa Yule mtu. Maana alikua alishamjua udhaifu wake.

Nachotaka kusema ni kwamba katika maisha yetu ya kila siku kamwe tusiwakatishe moyo watu wanaotamani kutenda vitu vyema, tusiwakatishe tamaa watu ambao wanatupenda. Kama mtu kakauambia wewe ni role model wake anataka kuungana nawe kufanya vitu ambavyo wewe unafanya kamwe usimkatishe tamaa kwa kumuambia kua hawezi, hata kama mtu huyo umemuona anaudhaifu Fulani katika kutenda jambo kama anatamani kutenda jambo hilo mpe nafasi afanye hata ile sehemu ndogo anayoweza. Super fan akiwa hater anakua hater kweli kweli, kuna watu tunawa-inspire kwa matendo yetu so mtu unayemu-inspire siku akikuomba nafasi afanye kila unachofanya wewe mruhusu usimkatishe tamaa.

Mtu akikuomba nafasi ya kufanya matendo kama unaweza kumsapoti fanaya hivo, ukimkatisha tama atajiona sio wa thamani..anaona anatamani kutenda mambo mema ila watu hawajali wema wake, bora awe mtu mbaya tu maana hakuna thamani ya kua mwema..
Kama mtu me/ke kakupenda sana na mwenyewe umethibitisha kua huyu mtu ananipenda kwa dahati ila wewe humpendi tafadhali usitumie nafasi hiyo kumuumiza watu wengi wanakua serial killers kwa ajili ya kukataliwa/oppressed na watu wanaowapenda kama wazazi au Crushes.

Mtu akikupenda usipompenda huna haja ya kumuambia kwa kashfa/kumsimanga kua humtaki , bora hata uwe unampa hata atumaini kwa hugs na maneno mazuri ya kutia moyo…Kuna watu wanapeda vibaya mno, mtu wa namna hiyo inatakiwa uchunge maneno ya kumjibu pindi mnapoongea. Maana ukimjibu majibu ya kumkashfu atajiona hana thamani duniani, ataona watu hawatakiwi kupendwa nakufanyia wema..mtu kama huyo anaweza kujidhuru au asipojidhuru basi anaweza kudhuru wengine. Hapa ndio wanatokea sasa wale wazee wa hit and run, anakuzalisha anakutelekeza, au anaweza kua muuaji (kuna kesi nyingi ajili hili).

Watu wabaya tunawatengeneza sisi wenye, hakuna anayezaliwa akiwa na roho mbaya. Kamwe usimwambie mtu hawezi kufanya kitu Fulani, hata kama unamuona hawezi kufanya jambo Fulani; Kuna watu wengine wakifanaya jambo Fulani likawashinda basi wanakua kila mtu akitaka kufanya jambo hilo wanamwambia kua hawezi Mtie moyo Mtu anapotaka kutenda jambo Fulani hata kama uanaona ni dhaifu…Tuheshimu watu wanye hisia za kweli nasi, tusapoti watu wanaotamani kuifanaya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.
-Ahsante
Da’Vinci
 
Ni kweli mkuu,

Ila hii kitu ya kumkatisha mtu tamaa/kutokujali hisia za watu wengine inaweza kutokea kwa kujua ama kutokujua.
Labda sababu ni ubinafsi, upendo wa kweli, uoga au huruma nk,

Kiukweli sipendi kumuona mtu anaumia au kuumizwa iwe kutokana na mimi au mtu mwingine, najaribu Kubalance hivi vitu viwili japo ni ngumu,

Mfano kwa mtu anayekupenda: huu ni mfano rahisi sababu wengi inawatokea hii(haijawahi kunitokea mimi teh teh).

Huyu binti amenipenda mimi na anataka nimuoe, Ila Mimi bado Sina Nia ya kuoa muda huu nataka nifanye mambo yangu kwa Uhuru,
Kwakua Mimi nina huruma na upendo wa dhati kwake, kwakua mimi sitaki kumpotezea muda wake sababu najua sina Nia kwake,
itabidi nimwambie ukweli, kwamba mimi siwezi kukuoa Sasa hivi sio kukuoa tu, siwezi hata kuishi na wewe sababu Nina mambo mengi ya kufanya, nikiwa na wewe tu, utasababisha nipoteze umakini kwenye mambo yangu na kuharibu kila kitu.
Sijui atachukua hatua gani huyu binti ila bila shaka atachukua maamuzi magumu au atanichukia kwa moyo wake wote, na atakua adui mkubwa tu,(Mara nyingi hutokea hivi).

Upande wa pili:
Ila ningekuwa naogopa kumuumiza hisia zake huyo mwanamke kutokana na huruma, lazima ningemuoa, na maisha yetu yasingekuwa na furaha sababu nilikuwa sina nia, na upendo lazima ushuke, ili kuupandisha itabidi muda mwingi nimfikirie yeye hiyo ingepelekea mimi kupoteza umakini na kuanguka kwa mipango yangu na kuharibu maisha yangu yote na yeye pia na watoto wetu na lazima tuishie pabaya.

Upande wa tatu:
Ok huyu binti amenipenda na anataka nimuoe.
Ila Mimi natambua kwamba sina nia ya kumuoa sababu Nina mambo yangu mengi ya kufanya hivyo nikimuoa tu nitapoteza umakini,
ila kwakua Mimi ni mbinafsi iwe kwa kujua ama kutokujua,
Nitamwambia,
Ok usijali nitakuoa.
Ukweli Sitomuoa kamwe, ila ataishia kupewa mimba, kumpotezea muda wake,kumchezea tu/ kumfanya sexy doll, kumuharibia future ya huyo Mwanamke, ila mambo yangu yataenda, ila yeye ndio basi tena.

Kwa mfano huo, inaonyesha haya mambo hayaepukiki na Ni magumu mno, unaweza ukafanya kitu chema kwa ajili yake ila anakipokea tofauti mtu huyo.

Mtu wa kwanza atachukuliwa ni mbinafsi na mwenye roho mbaya na katili asiyejali hisia za wengine, Kumbe Ni kinyume chake.

Mtu wa pili atachukuliwa kama mwenye upendo wa dhati na anayejali sana hisia za wengine, Kumbe ni muoga.

Mtu wa tatu atachukuliwa kama mwenye huruma na upendo wa dhati anayejali wengine, kumbe ni mbinafsi. (Wenyewe wanaita baharia)

Mifano iko mingi na yote inaleta matokeo tofauti.

Kumbuka ukifanya mambo kwa hisia lazima itakuharibia wewe, au yeye au wote kwa pamoja, na kukubaliana na matokeo ndio suluhisho pekee.

Mtu kubadilika kutoka mwema kuwa mbaya hakuwezi Kwisha na sio rahisi kuepukika, sababu zipo nyingi mno.

HAYA MAMBO SIO RAHISI KUEPUKIKA.
 
Mfano mwingine rahisi ni wa wapenzi. Mume na mkewe. Mwanzoni wanapendana, wanaaminiana, wanashirikishana kila jambo. Mambo yanaenda kuwa sivyo ndiyo taratibu, anayekengeuka anaonywa na mwenza wake, ataomba msamaha, maisha yanaendelea. Anarudia tena, na tena, kiasi kwamba mapenzi kutoka kwa mwenza yanapotea, na kinachofuata ni kisasi. Kisasi kinakuwa vyovyote, mpaka kudhuriana na kuhatarishiana maisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi mzuri! Unafikirisha!

mimi naamini kuwa mwanadamu ili atende ubaya haitaji motivation( Hamasa) kiasili tu yeye anakuwa ni mwovu( evil) ila anapata sababu ya kuegemea( justification)

Kwa nini naamini hivyo? Kwa sababu wapo wanaotendewa vibaya zaidi lakini huwa hawabadiliki
 
This satanic woman disappointed me big time. She is here and I know she will read it, I am planning a sweet revenge, designed for you! I will hurt you psycho logically....!! Time will Tell

Don't make a promise you can't fulfill...
 
Daaah! msome Tony hapo hii roho ya kisasi ikutoke, pengine umeepushwa na jambo baya sana, maradhi?? mikosi? mafumanizi??
Ila pia najua unajua roho ya kisasi ni roho dhaifu ya kutoka kwa shetani, don’t act that low.
 
Mada nzuri sana.Mfano wa hii mada niliuona kwenye Movie ya FAN ya Sharrukh Khan.Dogo mmoja alikuwa amefanana sana na alikuwa shabiki wa kutupwa wa Sharrukh Khan.Alijichanga nauli na kusafiri kwenda mjini ili akaonane na Role Model wake.Alifanikiwa kuonana na Sharrukh Khan lakini Sharrukh hakumpokea vizuri, alimsema na kumfokea sana dogo.Akamwambia dogo aishi maisha yake na asimfatilie.Kuanzia hapo Dogo akawa adui namba moja wa Sharrukh.Akawa anasafiri nchi kibao kumuharibia Sharrukh.Sharrukh akiwa na event, dogo anafika mapema kabla yake na kumchafua sanaa.FAN ni movie nzuri sana yenye mafunzo kama ya mtoa mada.Tuwe makini na kauli zetu hasa kwa watu wanaotujali na kutupenda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaah! msome Tony hapo hii roho ya kisasi ikutoke, pengine umeepushwa na jambo baya sana, maradhi?? mikosi? mafumanizi??
Ila pia najua unajua roho ya kisasi ni roho dhaifu ya kutoka kwa shetani, don’t act that low.
Client3
 
Ni kweli mkuu,

Ila hii kitu ya kumkatisha mtu tamaa/kutokujali hisia za watu wengine inaweza kutokea kwa kujua ama kutokujua.
Labda sababu ni ubinafsi, upendo wa kweli, uoga au huruma nk,

Kiukweli sipendi kumuona mtu anaumia au kuumizwa iwe kutokana na mimi au mtu mwingine, najaribu Kubalance hivi vitu viwili japo ni ngumu,

Mfano kwa mtu anayekupenda: huu ni mfano rahisi sababu wengi inawatokea hii(haijawahi kunitokea mimi teh teh).

Huyu binti amenipenda mimi na anataka nimuoe, Ila Mimi bado Sina Nia ya kuoa muda huu nataka nifanye mambo yangu kwa Uhuru,
Kwakua Mimi nina huruma na upendo wa dhati kwake, kwakua mimi sitaki kumpotezea muda wake sababu najua sina Nia kwake,
itabidi nimwambie ukweli, kwamba mimi siwezi kukuoa Sasa hivi sio kukuoa tu, siwezi hata kuishi na wewe sababu Nina mambo mengi ya kufanya, nikiwa na wewe tu, utasababisha nipoteze umakini kwenye mambo yangu na kuharibu kila kitu.
Sijui atachukua hatua gani huyu binti ila bila shaka atachukua maamuzi magumu au atanichukia kwa moyo wake wote, na atakua adui mkubwa tu,(Mara nyingi hutoke hivi).

Upande wa pili:
Ila ningekuwa naogopa kumuumiza hisia zake huyo mwanamke kutokana na huruma, lazima ningemuoa, na maisha yetu yasingekuwa na furaha sababu nilikuwa sina nia, na upendo lazima ushuke, ili kuupandisha itabidi muda mwingi nimfikirie yeye hiyo ingepelekea mimi kupoteza umakini na kuanguka kwa mipango yangu na kuharibu maisha yangu yote na yeye pia na watoto wetu na lazima tuishie pabaya.

Upande wa tatu:
Ok huyu binti amenipenda na anataka nimuoe.
Ila Mimi natambua kwamba sina nia ya kumuoa sababu Nina mambo yangu mengi ya kufanya hivyo nikimuoa tu nitapoteza umakini,
ila kwakua Mimi ni mbinafsi iwe kwa kujua ama kutokujua,
Nitamwambia,
Ok usijali nitakuoa.
Ukweli Sitomuoa kamwe, ila ataishia kupewa mimba, kumpotezea muda wake,kumchezea tu/ kumfanya sexy doll, kumuharibia future ya huyo Mwanamke, ila mambo yangu yataenda, ila yeye ndio basi tena.

Kwa mfano huo, inaonyesha haya mambo hayaepukiki na Ni magumu mno, unaweza ukafanya kitu chema kwa ajili yake ila anakipokea tofauti mtu huyo.

Mtu wa kwanza atachukuliwa ni mbinafsi na mwenye roho mbaya na katili asiyejali hisia za wengine, Kumbe Ni kinyume chake.

Mtu wa pili atachukuliwa kama mwenye upendo wa dhati na anayejali sana hisia za wengine, Kumbe ni muoga.

Mtu wa tatu atachukuliwa kama mwenye huruma na upendo wa dhati anayejali wengine, kumbe ni mbinafsi. (Wenyewe wanaita baharia)

Mifano iko mingi na yote inaleta matokeo tofauti.

Kumbuka ukifanya mambo kwa hisia lazima itakuharibia wewe, au yeye au wote kwa pamoja, na kukubaliana na matokeo ndio suluhisho pekee.

HAYA MAMBO SIO RAHISI KUEPUKIKA.
Big brain. Hongera genius Tony stark.
So tuseme kua ili mtu abadilike itstegemeana na tabia/nature ya mtu huyo.?

Btw kiss #2 nimekitoa kwenye animation muvi ya The incredible 2004. In case you missed it
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom