Kukataa Serikali tatu ni kuikataa Rasimu nzima. Je, wabunge wana uhalali wa kukataa rasimu?

Kitila Mkumbo

JF-Expert Member
Feb 25, 2006
3,354
1,943
Msingi wa Rasimu ya Katiba ni muundo wa Muungano. Wabunge wakikataa muundo wa muungano unaopendekezwa Rasimu hii inakufa kwa sababu karibu ibara zingine zote zimewekwa kwa kuzingatia muundo huu wa muungano. Kwa kifupi kukataa muundo wa muungano unaopendekezwa ni kuikataa rasimu yenyewe.

Swali, ni je wabunge wakiikataa rasimu hii wana uhalali wa kuendelea kujadili? Kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba, kazi ya bunge maalumu la katiba ni kujadili na kupitisha rasimu ya katiba. Sheria haikutoa nafasi ya kuikataa rasimu hii. Kazi ya kuikubali au kuikataa wameachiwa wananchi wakati wa referundum.

Kwa wale kama mimi ambapo ni wazoefu wa kujadili na kupitisha proposals mbalimbali tunajua kwamba ukiikataa proposal fulani haimanishi kwamba unachukua jukumu la kuiandika hiyo proposal. Unachofanya ni kutoa mapendekezo ya kuboresha na unamrudishia mwandishi akaiboreshe proposal yake kutokana na mapendekezo uliyompa. Mantiki ni hiyo hiyo.

Kama wabunge wetu wataikataa rasimu (proposal) ya katiba hawawezi kujivika jukumu la kuandika rasimu ingine. Hiyo itakuwa sawa na kuipokonya tume kazi yake. Ambacho wangeweza kufanya ni kupitisha mapendekezo na kuirudishia tume iyaingiza mapendekezo hayo. Kwa mfano, wakikataa muundo wa serikali tatu na wakaamua muundo wa serikali mbili, wangepaswa kuwarudishia rasimu tume ili wabadilishe huo muundo. Bahati mbaya sheria haitoi mwanya huo.

Hapa ndipo tunapoona deadlock itakayosababishwa na uking'ang'anizi wa CCM wa kutaka serikali mbili. Unaweza ukaona kwamba zoezi zima hili ni kutwanga maji. Ndio maana mie naona wale wanaokesha kuombea swala hili la katiba wanapaswa kumuomba Mungu awalainishe na kuwalegeza CCM ili wakubaliane na mapendekezo ya tume.
 
Wairudishie tume wakat bwana katiba kesha ivunja! Tuombe tu mungu ili ktk kuipigania katiba mpya tusife wengi zaidi ya kenya tufe japo 1000 tu.
 
Wairudishie tume wakat bwana katiba kesha ivunja! Tuombe tu mungu ili ktk kuipigania katiba mpya tusife wengi zaidi ya kenya tufe japo 1000 tu.

Hata tukizidi poa tu mkuu kwa ujinga wa majangili
 
Mkuu, ngona yote iko kwenye sura ya tano katika ibara ya 25(1) ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, namba 8 ya mwaka 2011 inayosema,
25.-(1) Bunge Maalum litakuwa na mamlaka ya kujadili na kupitisha masharti ya katiba inayopendekezwa, kutunga masharti ya mpito na masharti yatokanayo kama Bunge Maalum litakavyoona inafaa.

Hii sentensi ni ndogo lakini imebeba mstakabali wa Taifa kwa ujumla!.
 
Masharti yatokanayo kama bunge la katiba litakavyoona inafaa ... ( watakoona inafaa ni wabungee wa bunge maalumu la katiba yaani wajumbe )

Masharti hayo yanapitishwa vip ili kuleta maana ya kuonekana sharti hilo linafaa .

1. kwa hoja kuwekwa na kupigiwa makofi .
2. kwa mfumo wa upigaji kura (siri na wazi).
3. kwa kuwahoji (wanaosema ndio ........ wanaosema hapanaaaaa... )
 
Hapo hapo kwenye muundo wa Muungano. Tume ya Warioba ilikuja na facts zilizotokana na maoni ya wananchi japo wengine wanadai waliotoa maoni "walikuwa wachache mno". Ningependa kujua endapo Bunge Maalum litakuja na "muundo mbadala" watakuwa wame-base kwenye facts zipi? Au, "busara" ya Wajumbe wasiozidi 629 ni kubwa na ya maana kuliko maelfu (machache) ya wananchi waliopendekeza muundo ulioko kwenye Rasimu? Yetu macho.
 
Sincerely the blunder that is being moduled by CCM will lead ccm and JK into an everlasting regret. Nilishajikatia tamaa na hicho kinachoitwa katiba mpya tangu zoezi la kuteua wabunge wa bunge maalum kuanza, maana vijembe vilanza sambamba na uteuzi ili kujenga mazingira ya kulazimisha mawazo ya chama tawala yapite bila kupingwa.

Sasa baada ya kutambua kwamba watanzania wengi wanajua kutafakari na kujenga hoja tofauti na 1964, viongozi na ccm sasa wameteka nyara jambo lote na kutaka kusini kuitwe kusini piga ua garagaza na kutumia vitisho kwamba jeshi limekaa mkao wa kupindua nchi endapo serili tatu itapita.

Tena wanatumia vyombo vya habari vya umma kwa kuwa ni rahisi kwao kuvifinyanga watakavyo ili vifanane sura na dude walitakalo. Watanzania tuungane na kuona ujangili wa viongozi wetu na chama chao katika kupora haki hii.

Kama wanasema kweli, kwamba wanayo nia nzuri ya kudumisha Muungano, basi waendeleze mawazo ya waasisi, Zanzibar ifute katiba yao na kisha Tanzania iwe nchi moja, Unguja na Pemba iwe mikoa. SHort of that, serikali tatu kweli ni inevitable - kama sio leo sio mbali.
 
Kifungu cha 25 (1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba (English Version) imetoa uhuru wa Bunge Maalum la Katiba kuifumua hiyo Rasimu na kuandika chochote wajumbe wanachoona kinafaa!
 
Kifungu cha 25 (1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba (English Version) imetoa uhuru wa Bunge Maalum la Katiba kuifumua hiyo Rasimu na kuandika chochote wajumbe wanachoona kinafaa!


haya bhana. na version ya kiswahili haijatoa uhuru huo?
 
Daaaaah kweli siasa ni kitu kingine na imewatia upofu wa akili watu wengi,
.
.
Mtu yuleyule leo haamini yale aliyoyanena kwa kinywa chake sababu tu ya siasa.
 
Back
Top Bottom