Kukata kodi ya jengo kwenye LUKU, watakaokuwa walipaji wakuu ni wapangaji na si wamiliki tena

The lost

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,695
8,209
Uwezo wa viongozi wetu wa kufikiri una walakini. Wananchi masikini wanakwenda kubebeshwa mzigo wa malipo ya kodi ya majengo tena. Nasema hivi kwa kuwa nyumba nyingi wapangaji ndiyo wanaonunua umeme na wala si wamiliki.

Sasa kitendo cha kukata kodi ya pango la jengo kutoka kwenye umeme ni kuwaumiza wananchi masikini wa nchi hii huku wamiliki wa majengo hayo wakiendelea kuchukua kodi zao kama kawaida.

Bajeti mbaya kuwahi kutokea tangu Uhuru.
 
900099.jpg
 
Kabla ya kusema jambo lolote ni bora kujiridhisha walau kwa uchache, sina hakika kama kumbukumbu za mwenye nyumba (Mmiliki) zitaambatanishwa na mpangaji wa nyumba au jengo.

Waliopitia kama ni sheria au miongozo za namna ya ulipaji wa kodi za majengo watuletee ufafanuzi kidogo ili tuweke kwenye kumbukumbu.
 
Mita ya LUKU ina jina la mmiliki wa nyumba na siyo mpangaji, hata kama mpangaji atalipia bado itakuwa ni sehemu ya kodi
Kwa lugha nyingine, kodi yako itapungua kwa kiasi ulicholipia. Pia kodi hii inalipwa mara moja tuu kwa mwaka.
 
Anza kudai punguzo la buku kila mwezi toka kwa baba mwenye nyumba. Kwa Mwaka elfu 12,000. Au ukitaka acha kununua luku liwe jukumu la mwenye nyumba.

Binafsi nimefurahia urahisi wa kulipa kila mwezi elfu moja. Watu wa halmashauri kila siku walikuwaa wananiletea barua za ukumbusho kulipa lakini muda wa kwenda kupanga foleni TRA nilikuwa sina
 
Mbona ni rahisi tu hilo,ukishalipa umeme wako kama kuna kodi ya nyumba inakatwa,ni kumuonyesha tu risiti yako mwenye nyumba mnakuja kukatana kwenye kodi.
 
Mita ya LUKU ina jina la mmiliki wa nyumba na siyo mpangaji, hata kama mpangaji atalipia bado itakuwa ni sehemu ya kodi
Kwa lugha nyingine , kodi yako itapungua kwa kiasi ulicholipia. Pia kodi hii inalipwa mara moja tuu kwa mwaka
Ni 1000 kila mwezi. Kwa maana nyingine kwa mwaka ni 12000 tofauti na 10000 ya awali kwa hizi nyumba zetu za kawaida. In summary ni kwamba kodi ya majengo imepanda kwa 2000 zaidi.
 
Hadi nyumba za matope na nyasi, mabanda ya kuku,ngombe, zenye kuku zitalipiwa Kodi ya majengo. Jengo moja lenye luku 5 ,Kodi ya majengo ni mara Tano. Hii plan ninashauri ianzie Tanzania visiwani.
 
jamani ifike mahali tusiwe wepesi wa kulalamika kila kitu hivi jamani shilingi elfu moja kwa mwezi hata hao wapangaji wanaweza kulalamika kweli?elfu moja? elfu 12 kwa mwaka unamiliki nyumba au umepanga itakushinda mpaka uje ulalamike huku? sawa kama mpangaji ni mmoja basi mbona hesabu rahisi tu analipa elfukumi hiyo ya kodianakukata kwenye kodi simple tu
 
Vitu kama hivi Mwendazake alikua anjichukuliaga credit kwa wananchi kiulainiiii.

Mwigulu muda wa kufikiria vitu vidogo namna hii hana, always anawaza kuendelea kua ndani ya teuzi za Rais tu
 
Uwezo wa viongozi wetu wa kufikiri una walakini. Wananchi masikini wanakwenda kubebeshwa mzigo wa malipo ya kodi ya majengo tena. Nasema hivi kwa kuwa nyumba nyingi wapangaji ndiyo wanaonunua umeme na wala si wamiliki.

Sasa kitendo cha kukata kodi ya pango la jengo kutoka kwenye umeme ni kuwaumiza wananchi masikini wa nchi hii huku wamiliki wa majengo hayo wakiendelea kuchukua kodi zao kama kawaida.

Bajeti mbaya kuwahi kutokea tangu Uhuru.
Yaani Waziri na wizara yote nikama hawafai hizo nafasi ,kama alivyo sema ex cag Asad ,kwanza nimeshangaa sana Mwigulu amepataje muda wa kufikiri na kutunga mashairi ya kumuelezea Raisi Samia wakati amepokea wizara bajeti imeshapangwa na huku akitarajiwa kufanya mabadiliko muhimu !!?? Ukweli bora katiba mpya ije hizi nafasi za viongozi wajuu waziombe na kufanyiwa vetting kama kenya vile,vinginevyo ndio hii kuteua wavivu wakufikiria,
 
Uwezo wa viongozi wetu wa kufikiri una walakini. Wananchi masikini wanakwenda kubebeshwa mzigo wa malipo ya kodi ya majengo tena. Nasema hivi kwa kuwa nyumba nyingi wapangaji ndiyo wanaonunua umeme na wala si wamiliki.

Sasa kitendo cha kukata kodi ya pango la jengo kutoka kwenye umeme ni kuwaumiza wananchi masikini wa nchi hii huku wamiliki wa majengo hayo wakiendelea kuchukua kodi zao kama kawaida.

Bajeti mbaya kuwahi kutokea tangu Uhuru.
Ndiyo ujue akili za wabunge wa ccm. Na hakuna mpinzani kwa hiyo hiyo itapita tu kiulaini!!!
 
Uwezo wa viongozi wetu wa kufikiri una walakini. Wananchi masikini wanakwenda kubebeshwa mzigo wa malipo ya kodi ya majengo tena. Nasema hivi kwa kuwa nyumba nyingi wapangaji ndiyo wanaonunua umeme na wala si wamiliki.

Sasa kitendo cha kukata kodi ya pango la jengo kutoka kwenye umeme ni kuwaumiza wananchi masikini wa nchi hii huku wamiliki wa majengo hayo wakiendelea kuchukua kodi zao kama kawaida.

Bajeti mbaya kuwahi kutokea tangu Uhuru.
Na itapitishwa kwa kishindo na ma-nzi ya kijani
 
jamani ifike mahali tusiwe wepesi wa kulalamika kila kitu hivi jamani shilingi elfu moja kwa mwezi hata hao wapangaji wanaweza kulalamika kweli?elfu moja? elfu 12 kwa mwaka unamiliki nyumba au umepanga itakushinda mpaka uje ulalamike huku? sawa kama mpangaji ni mmoja basi mbona hesabu rahisi tu analipa elfukumi hiyo ya kodianakukata kwenye kodi simple tu
Huku ni kuwaza kinyume

Vipi kwenye nyumba yenye luku zaidi ya tano?
 
Hii haina maandalizi, ilitakiwa tanesco washirikishwe tangia mwanzo, ikiwa na pamoja na tanesco kuwa na database with recent images
 
Back
Top Bottom