Kukata kimeo ni tiba mbadala kwa magonjwa yote?

Tyupa

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
802
653
Hapa Visiga kwa Kipofu wilayani Kibaha kuna mganga wa kienyeji mmoja maarufu sana kwa kutibu magonjwa yote kwa kukata VIMEO tu. Kwa wale waliokwenda wanasema anavyo vibali vyote vya serkali vya kuendesha kazi hiyo tu ya kukata vimeo kwa magonjwa yote ambayo mtu anayo.Kuna msusururu wa wagonjwa kutoka sehemu zote za mkoa wa Pwani na Dar es Salaam na sehemu zingine.

Mgonjwa ambae anakohoa kwa sababu ya TB, Pneumonia, Bronchitis, Allergies, Homa kali na hata wenye virusi ambao wanateswa na magonjwa nyemelezi wakifika pale dawa ni moja tu ya kung'oa vimeo.Mganga mkuu wa wilaya ya Kibaha mwenye dhamana na afya za watu wote wilayani humu tunamwomba atuthibitishie hii tiba ili kila mwenye hitaji aweze kuwahi kupata huduma hii ya aina yake.

Gharama kwa kila kimeo ni Tsh.10,000 na huduma hiyo hutumia takrbani dakika tatu.Kwa mintarafu hii serkali inapaswa kufuatilia kujua kwa kina kama huduma hii ina tija au la kwa sababu isije ikaonekana mtoa huduma lengo lake kuu ni kujipatia kipato na si kutokomeza magonjwa.

Mashuhuda na huduma hii wanasema pesa zinazokusanywa ni nyingi mno ambazo pengine ndizo zenye kusudiwa na si tija katika huduma yenyewe.
 
Hapa Visiga kwa Kipofu wilayani Kibaha kuna mganga wa kienyeji mmoja maarufu sana kwa kutibu magonjwa yote kwa kukata VIMEO tu. Kwa wale waliokwenda wanasema anavyo vibali vyote vya serkali vya kuendesha kazi hiyo tu ya kukata vimeo kwa magonjwa yote ambayo mtu anayo.Kuna msusururu wa wagonjwa kutoka sehemu zote za mkoa wa Pwani na Dar es Salaam na sehemu zingine.Mgonjwa ambae anakohoa kwa sababu ya TB, Pneumonia, Bronchitis, Allergies, Homa kali na hata wenye virusi ambao wanateswa na magonjwa nyemelezi wakifika pale dawa ni moja tu ya kung'oa vimeo.Mganga mkuu wa wilaya ya Kibaha mwenye dhamana na afya za watu wote wilayani humu tunamwomba atuthibitishie hii tiba ili kila mwenye hitaji aweze kuwahi kupata huduma hii ya aina yake.Gharama kwa kila kimeo ni Tsh.10,000 na huduma hiyo hutumia takrbani dakika tatu.Kwa mintarafu hii serkali inapaswa kufuatilia kujua kwa kina kama huduma hii ina tija au la kwa sababu isije ikaonekana mtoa huduma lengo lake kuu ni kujipatia kipato na si kutokomeza magonjwa.Mashuhuda na huduma hii wanasema pesa zinazokusanywa ni nyingi mno ambazo pengine ndizo zenye kusudiwa na si tija katika huduma yenyewe.
 
Watu wanatafuta tiba mbadala kwakuwa huduma za afya zinazotolewa na serikali haziwafikii wananchi na pia gharama za matibabu ziko juu
 
Mtoa mada kwanza lipia tangazo. Alafu umekuja kutoa tangazo kama vile we siyo muhusika eti
 
Kwa wale mnaoulizia kimeo

Ukifunua mdomo kuna kitu kinaning'inia huku kwenye koo kwa juu kushuka chini kirefu refu hivi hiko ndio kimeo
 
Back
Top Bottom