Kukamilika Bwawa la JNHEPP

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,215
3,587
Taarifa ya gazeti la serikali la kila siku la Habari Leo toleo la tarehe 19 Disemba 2022 kwamba Bwawa la JNHEPP limekamilika, likimrejea Waziri wa Nishati kwamba kwa ujazo wa Bwawa linahitaji mvua za misimu miwili kujaa kwa kiwango chake hazina budi kupewa kongole.

Yafuatayo yanatishia mustakabali wa nchi ki-nishati na ki-hifadhi ya ikolojia yetu:-

1. Kwa takriban miezi michache iliyopita, baadhi ya vyombo vya habari vilinukuliwa vikiripoti kwamba chanzo cha maji cha Ihefu kimevamiwa upya.

2. Upungufu wa maji kwenye miji inayotumia maji ya mto Ruvu umechangiwa na watu kuvamia bonde la mto Ruvu na chanzo chake na sababu ya pili ikiwa ni kiangazi kinachoendelea na sababu zote mbili kusababisha mgawo wa maji na umeme.

Tulivyokwama.

Suala la uvamizi wa mabonde, maeneo chepe na vyanzo vya maji limekuwa sugu na taasisi kadhaa husika zimewahi kuendesha operesheni ya kuwaondoa wavamizi lakini kwa mafanikio kidogo sana.

Aidha, yapo baadhi ya maeneo hayo ambayo yanatambulika kuanzishwa kwa Sheria ya Bunge e.g. Mamlaka ya RUBADA na hata mengine pia kuanzishwa na kuhifadhiwa kisheria tangu serikali ya mkoloni chini ya Sir Richard Gordon Turnbull.

Serikali izingatie ushauri ufuatao:-

Kwa kuwa ardhi ya JMT iko chini ya uangalizi wa taasisi ya urais na kwa kuwa taasisi hii ndiyo inayoamuru majeshi ya ulinzi na usalama, ninaishauri serikali itangaze rasmi kukabidhi chini ya ulinzi wa JWTZ maeneo yote JMT ambayo ni vyanzo vya maji hususan maji yanayoingia kwenye Bwawa la JNHEPP, ikibidi hatimiliki ya maeneo hayo ipewe JWTZ ambayo nayo isiyatumie kwa shughuli yoyote zaidi ya kuyahifadhi tu ili Bwawa liweze kufua umeme muda wote mfululizo 24/7/30/365.

Wahifadhi wazuri JMT ni pamoja na TANAPA, TFS, TAWA na JWTZ.

Ushauri huu usipozingatiwa kwa uzito unaoustahili ifahamike kwamba hatuna mwarobaini mwingine isipokuwa kujiandaa kisaikolojia kumiliki Bwawa kubwa litalofua umeme kwa mgawo na hivyo ugavi wa nishati hiyo pia kuendelea kuwa wa mgawo, hii itakuwa ni mradi wa tembo mweupe (white elephant project) maana mradi hautakuwa na manufaa kwenye uchumi wa taifa.

Uchaguzi ni wetu kunyoa au kusuka.

Taswira ya msitu wa mvua wa kiikweta wa Congo kwa hisani ya google.
Screenshot_20221219-173523.jpg

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Taswira ya msitu wa mvua wa kiikweta wa Congo kwa hisani ya google.View attachment 2451921
Wasi wasi wangu kama mto Ruaha mkuu huwa unakauka maji, hayo maji ya kujaza hilo Bwawa, hata hiyo miaka/ Misimu miwili TUNADANGANYWA. Tujiandae kisaikolojia na huu WHITE ELEPHANT project
Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Fl8JYLCWQAAFsmN
 
Back
Top Bottom