Kukamilika Bandari ya Kabwe, kukuza biashara Kongo

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1126966

MKOA wa Rukwa, unatarajiwa kukuza biashara ya mazao ya chakula katika nchi za Demokrasia ya Kongo, Burundi na Zambia, kufuatia kukamilika kwa bandari ya kisasa ya Kabwe inayojengwa na Mamlaka ya Bandari (TPA) kwa Sh. bilioni 7.498.


Wananchi wa mkoa huo, wamekuwa wakisafirisha mchele, mahindi, maharage, unga na sukari kwenda nchi hizo kwa kutumia mitumbwi lakini baada ya ujenzi wa bandari hiyo kukalimika watasafirisha kwa kutumia meli. Meneja wa Bandari ya Kigoma ambaye pia anasimamia bandari zote za Ziwa Tanganyika, Ajuaye Msese, akizungumza na waandishi wa habari waliotembela bandari hiyo jana, amesema ujenzi wake umefikia asilimia 50 na unatarajiwa kukamilika Aprili 2020.
1126968


"Kama mnavyoona bandari hii tunayojenga ya kisasa, itaenda kufungua uchumi wa wakazi wa mkoa wa Rukwa, kwa sababu wanategemea sana biashara ya kuuza mazao yao katika nchi za Congo na Burundi," amesema Msese.

Ameeleza kuwa, bandari ndogo iliyopo ina kina kifupi hivyo haiwezi kupakia mizigo mingi na ya kutosha mahitaji ya nchi hizo ndio sababu ya TPA kuanza kutekeleza mradi huo.

Msese amesema mbali na kujenga gati la kisasa lenye kina kirefu, pia wanajenga barabara na maegesho ya magari unaotekelezwa na Mkandarasi Sumry's Enterprises Ltd kwa gharama za TPA. Amesema mradi huo pia unajumuisha jengo la kupumzikia abiria, jengo la mgahawa, ghala la kuhifadhia mizigo, nyumba za wafanyakazi na uzilishaji.

Msese amesema mbali na miradi hiyo pia wamejenga ofisi za taasisi za Serikali katika bandari hiyo na zote nchini ili kudhibiti uingiaji wa bidhaa feki na wahamiaji haramu.

Amesema mamlaka ya Bandari inafanya kazi na Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) na Shirika la Viwango Tanzania(TBS) ili kudhibiti uhalifu katika mipaka hiyo.
 
Bandari ya kasanga ipo miaka mingi sana hakuna hicho kinachoitwa kufunguka kwa biashara sababu ni kwamba drc ya mwambao mwa ziwa haina mali wala watu wengi kama kusini Lubumbashi na kaskazini Bukavu/Goma ko unakuta volume ya biashara ni ndogo
Pengine Congo nayo iweke miundombinu ya kuunganisha miji yao mikubwa iliyoko interior na bandari zao ndio biashara itachangamka
 
Wamechelewa saaanaa...

Hadi leo!? Rukwa kweli ilirukwa.
Huu mkoa hauna viongozi wakubwa na wasomi ndio maana unarukwa
Yaani ndio mkoa una halmashauri/wilaya chache Tzn wakati jiografia yake ilifaa uwe na wilaya/halmashauri nyingi ili kuwafikia wananchi kihuduma ikizingatiwa una miundombinu duni
Bonde la Rukwa lilifaa iwe wilaya inayojitegea halikadhalika kabwe kule wangeigawa Mkasi ili watu wa mwambao wa ziwa Tangangika wasogezewe huduma
Katavi wenzao Pinda ameupa mkoa na halmashauri tano wakati ilikuwa wilaya moja,Kamwelwe anajenga barabara za lami kama zote kila kona
 
Back
Top Bottom