Hute
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,537
- 6,463
Hivi wakuu,
Mtu akiwa nyumbani kwake, au kazini kwake anaendelea na shughuli zake, mara gari inasimama na kumwambia upo chini ya ulinzi, ingia kwenye gari, then wanaondoka naye, raia wa kawaida atajuaje kama hao wanaomweka kwenye ulinzi ni majambazi, ni usalama wa taifa, polisi au wanajeshi?
Na je kati ya hao, ni nani anayo mamlaka kukamata? Na wakati wa kukamata unatakiwa kupewa haki zipi?
Kama hawatatoa hizo haki labda kujitambulisha wao ni nani na wakakupatia muda uage wale uliokuwa nao na kuwapatia ujumbe kuwa umekamatwa na watu fulani either polisi etc na wafanye mpango kuja kukuwekea dhamana etc,
Kama hawatajitambulisha, hawatatoa haki, itakuwa kimyakimya tu si unaweza fikiri ni majambazi hayo? Na je, si bora kupambana nao kama uwezo unao? Au ndugu na jamaa waliokuzunguka si bora uombe msaada hata wa kuita mwizi ili waje wakusaidie kupambana na mtu anayekuteka bila kukuambia yeye ni nani na anakukamatia kwa kosa gani?
Hebu wanasheria kutaneni hapa toeni haki kwa raia, kuna siku hapa watu wenye vikundi vya kijambazi wataanza kujifanya polisi na kukamatwa watu ovyo kumbe sio polisi wana yao tu na kwasababu raia wanaogopa polisi na usalama wanaacha tu mtu anaondoka na wakienda kituo cha polisi askari hawana habari yeyote juu ya tukio hilo.
Si bora kupambana nao kufa kiume? Rusha jiwe, mwiko, ukuni chochote alimradi kutoa alarm kwa watu waje wakukomboe.