Kukamatwa Mbowe balaa tupu Dar; CUF waungana na CHADEMA, watangaza maandamano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukamatwa Mbowe balaa tupu Dar; CUF waungana na CHADEMA, watangaza maandamano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 6, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Kukamatwa Mbowe balaa tupu Dar  *Wafuasi waandamana, watawanywa, watatu mbaroni
  *Dkt. Slaa asema 'ukondoo' wao umefika kikomo
  *CUF waungana na CHADEMA, watangaza maandamano

  Na Benjamin Masese

  Kauli ya Dkt. Slaa

  CHADEMA kimesema kuwa 'ukondoo wao' na uvumilivu dhidi ya udhalilishaji na unyanyasaji unaofanywa na jeshi la polisi kwa viongozi na wabunge wake umefikia kikomo na sasa kitaanza kufanya maamuzi mazito muda wowote.

  Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Willibrod Slaa alisemsa hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kulaani kitendo cha polisi kumshikilia Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe huku wakijua wazi ndiye Waziri Mkuu Kivuli na mwakilishi wa Kambi ya Upinzani kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge inayotrarajia kukutana leo Dodoma.

  Dkt. Slaa alisema kuwa uvumilivu wao umefikia mwisho wa kuona serikali kupitia Jeshi la Polisi ikiendelea na mkakati wa kuwadhalilisha na kuwadhoofisha wabunge na viongozi kwa kuwakamata bila kufuata taratibu husika, tofauti na wenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Alisema kutokana na hali hiyo CHADEMA kimetoa maazimio yao kwamba muda wowote kinaingia barabarani kuidhabu serikali kwa kutumia nguvu ya umma, ikiwa Bw. Mbowe ataendelea kushikiliwa na kushindwa kuhudhuria vikao vya bunge.

  Pia alisema kuwa wabunge wote wa CHADEMA hawatashiriki katika bunge lijalo na hata vikao vinavyoanza leo mkoani Dodoma.

  Dkt. Slaa alisema chama hicho kisitupiwe lawama ikiwa machafuko yatatokea nchini bali lawama zielekezwe kwa Rais Jakaya Kikwete pamoja na jeshi lake la polisi na taarifa tayari zimefikishwa sehemu zote husika ndani na nje ya nchi.

  Alisema kuwa kitendo cha serikali kudai kwamba CHADEMA inaendesha uchochezi unaohatarisha amani nchini katika mikutano yao si kweli, bali imeona chama hicho kinatoa elimu kwa wananchi ili kujua haki zao ndio maana imeanzisha mkakati wa 'kamata kamata na dhalilisha'.

  Dkt. Slaa alisema hivi sasa anaendelea na mawasiliano na viongozi wa Chadema katika mikoa yote nchini ili kujipanga kuiadhibu serikali kwa kuwa tangu matukio yatokee hakuna kauli yoyote ilitolewa na Rais Kikwete au Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda kuomba radhi au kutoa pole kwa mauaji yalitokea mkoani Mara.

  Wakati mkutano huo ukiendelea tayari mamia ya vijana walikuwa wamejikusanya makao makuu ya chama hicho wakisubiri kupewa amri ya kuingia barabarani lakini Dkt. Slaa aliwaomba kuwa na subira ili kuimarisha mawasiliano sehemu zote za nchi.

  "Napigiwa simu na RCO kila mara akinitaka kuwatuliza vijana wangu ambao wengine tayari wamefika kituoni lakini ninachomueleza na kumsisitizia ni kwamba ninaendelea kuwasiliana na wengine nchi nzima ili kuongeza nguvu... na hili tusilaumiwe kamwe," alisisitiza na kushangaliwa na vijana wakitaka kupewa ruksa muda huo.

  Baadhi ya viongozi wa chama hicho na upinzani walifika katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam anakoshikiliwa Bw. Mbowe ili kujua hatma yake na kufanya kikao na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Bw. Suleiman Kova.

  Waliofika hapo ni Mbunge wa Ubungo, Bw. John Mnyika, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na wengine ambao walitoa mapendekezo yao.

  Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka kwenye kikao hicho, Profesa Lipumba alisema kuwa lengo la kufika hapo ni kutaka kumwekea dhamana Bw. Mbowe kwa kuwa ni tegemeo lao katika Kambi ya Upinzania na hasa bunge lijalo.

  "Nimestushwa sana na kitendo cha Mbowe kukamatwa kipindi hiki wakati akiwa katika maandalizi ya hoja za Bunge la bajeti, na hii ni kuminya demokrasia, na kitendo cha kuendelea kumshikilia kinaongeza hasira ukizingatia hivi sasa hakuna heshima tena kwa wabunge wa upinzani, isitoshe spika yupo kimya, hatukubaliani na hili," alisema.

  Alisema kuwa wapinzani watakutana muda wowote ili kutoa tamko la pamoja kwa kuwa tayari imeonesha wazi sheria hazifuatwi katika kesi hii badala yake siasa zimechukua nafasi kubwa.

  "Kuna wezi wa mabilioni wanatembea barabarani hadi sasa na hawakamatwi na polisi, lakini jeshi la polisi limeonekana kufanya oporesheni ya kuwamakata wabunge, sasa tunaondoa tofauti zetu na sasa tunaungana kupinga vitendo hivi," alisema.

  Naye Bw. Mnyika alisema katika kikao hicho walimuomba Bw. Kova kuwa hakuna sababu ya kumpeleka Bw. Mbowe Arusha, aachiwe huru ili ahudhuria bungeni, na kama anapelekwa asipelekwe chini ya ulinzi kwa kuwa wananchi wanaweza kusababisha machafuko.

  Hata hivyo, alisema licha ya mazungumzo yao ya muda mrefu na Bw. Kova, afande huyo alisisitiza kwamba polisi kama chombo cha ulinzi kinatekeleza amri iliyolewa na mahakama.

  Bw. Kova alilieleza majira kuwa jeshi la polisi limejiandaa kumpeleka Bw. Mbowe mkoani Arusha muda wowote ili kufikishwa mahakamani leo.

  Alisema kuwa taratibu za kumsafirisha zimekamilika na kutoa mwito kwa wananchi kuwa watulivu na kuiachia mahakama ifanya kazi zake.

  Bw. Kova alisema kuwa jeshi la polisi halina nafasi ya kujadilia amri ya mahakama, hivyo lazima Bw. Mbowe afikishwe mahakamani na tayari ulinzi umeimarishwa hapo Arusha.


  Kauli ya Chadema Mara

  Mwandishi wetu Hellena Magabe anaripoti kutoka Musoma kuwa Chadema mkoani Mara imesema kufikia leo saa nne asubuhi inataka kumwona Bw. Mbowe ameachiwa huru bila masharti yoyote.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara, Bw. Charles Kayere alisema wanamtaka Spika wa Bunge atoe tamko juu ya kinga ya wabunge kukamatwa ovyo ovyo na kudhalilishwa, hasa wale wa upinzani.

  Alilaani kitendo cha polisi kumkamata kiongozi huyo siku ambazo si za kazi ili asote mahabusu, akisema ni cha kinyama na kitasababisha uzalendo uwashinde.

  Aliongeza kuwa mahakama imekuwa ikitaja kesi hiyo ovyo kabla ya upelelezi kukamilika, jambo ambalo linawatia mashaka kuwa hujuma inafanyika ili kuwadhalilisha wabunge hao wa Chadema.


  CUF kupinga kwa maandamano

  Chama cha Wananchi (CUF), kimetangaza kufanya maandamano ya amani kupinga udhalilishwaji wanaofanyiwa wabunge kwa kukamatwa wakiwa katika majukumu yao na mauaji ya raia wasiokuwa na hatia unaofanywa na Jeshi la Polisi nchini.

  Kaimu Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa mipango, uchaguzi na Bunge, Shaweji Mketo, alisema jana kuwa chama hicho kitafanya maandamano Juni 12, mwaka huu yakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba.

  Alisema maandamano hayo yatakayoanzia Ubungo Mataa na kuishia katika viwanja vya Manzese Bakharesa kwa mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya taifa.

  Mketo, alisema Jeshi la Polisi hivi sasa limekuwa likiwadhalilisha wabunge na kuwaua wananchi wasio na hatia hasa pindi wanapokuwa wanadai haki zao za kimsingi kwa mujibu wa katiba ya nchi.

  "Sote tumekuwa mashahidi kwa hili raia wanauawa na polisi bila hatia, lakini bado kumekuwa na tabia iliyojengeka ya
  kuwadhalilisha wabunge hasa kutoka vyama vya upinzani. Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu na tunawaomba wanaharakati na wananachi wote kwa ujumla watuunge mkono kwa hili," alisema Mketo.

  Aidha CUF imelaani kitendo cha polisi kuwakamata waandishi wa habari wakiwa katika majukumu yao ya kazi katika Kijiji cha Nyamongo, wilayani Tarime kwani si kitendo cha kiungwana na kinakwenda kinyume cha katiba na tamko la haki za binadamu ambalo Tanzania imeridhia.

  Alisema kitendo cha kuwakamata wabunge hao ni udhalilishaji wa wazi na kutoheshimu hadhi ya mbunge na madaraka ya bunge.

  Wabunge waliokamatwa ni pamoja , Bi Magdalena Sakayana (Viti Maalumu-CUF_, Bw. Tundu Lissu (Singida Mashariki-CHADEMA), Bi. Ester Matiko (Viti Maalumu-CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe-CHADEMA.

  Pamoja na hatu hiyo alisema CUF inalaani kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwanyima dhamana wajumbe wake wa Baraza Kuu akiwemo Zainabu Nyumba, ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino).

  Alisema mbali na kuwanyima dhamana viongozi hao, Jeshi la Polisi limeendelea kuwakatama wananchi katika Jimbo la Urambo Magharibi na kufikia 30 hadi kufikia juzi.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  khaaaa ,,,nimesisimka sana baada ya kusoma hii kitu...haya ngoja tuone nini kinakuja maana hili nchi linakaribia kupasuka
   
 3. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Maandamano mnayotaka kuyafanya Polisi waliisha yazuia, sasa kama slaa ana ubavu aamrishe watu na yeye aone kama yaliyo mpata Mbowe !
   
 4. M

  Murrah Senior Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa wapenda haki yatafanyika endelea ni upuuzi wako
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  CUF bara washaamka yakhe. CUF bara wanajua fika muafaka uliofikiwa kati yao na CCM si ndoa bali unyumba, aka nyumba ndogo. Wabara wameshtukia deal na kuwaacha wazenj na wapemba kuwa nyumba ndogo ya CCM. Unamsikia Maalim Seif?: Jibu la hasha, hawezi kupingana na sugar dad, asijekosa vitafunio.
   
 6. samito

  samito JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 621
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hao CUF walikuwaga wap siku zote? ivi CUF ni upinzani kweli au ni sub-party ya CCM?
   
Loading...